Kampuni ya Anesa Co.,Ltd
kupitia biashara yake tanzu ya Fresh Farms(T); kwa kushirikiana na kikundi cha “Rudisha
Uumbaji wa Mungu kwa Kupanda Miti (RUMM)-Kilolo;” tukiwa mkoani Iringa,
tumezindua programu maalumu iliyolenga kuwawezesha watanzania wengi kuwekeza na
kumiliki mashamba ya miti ya mbao na nguzo kwa urahisi kabisa.
1. Progamu hii inaitwa “GREEN THE WORLD and BECOME RICH” ambapo
tunauza mashamba yenye miti (miti pamoja na ardhi) kwa utaratibu wa mtu kulipa
kidogo kidogo kwa kadiri ya kipato chake. Kiwango cha chini cha kununua ni
ekari tano, ambapo utatakiwa kulipa walau asilimia 50% ya bei yote; kisha fedha
inayobaki utaendelea kuilipa kwa awamu kwa kadiri utakavyokubaliana na kampuni
2. Tupo Iringa mjini na Kilolo (kijiji cha Mwatasi), na mashamba
yapo maeneo mbalimbali katika wilaya za Mufindi na Kilolo. Yapo mashamba yenye
miti kuanzia ya mwaka mmoja hadi minne, na bei zake ni kuanzia tsh.
700,000(laki saba) hadi 2,000,000 (milioni mbili) kutegemeana na umri wa miti
husika. Bei zote zinajumuisha (miti pamoja na ardhi)
3. Miti ya mbao inachukua miaka kati ya 7 hadi 10 tangu kupandwa
hadi kuvunwa. Wastani wa faida unayoweza kupata kwa ekari moja ya miti
iliyokomaa ni tsh milioni tisa hadi kumi na tano (kama ungekuwa unauza leo).
Gharama ya kuhudumia ekari moja kwa mwaka haizidi laki mbili. NOTE KWA WALE
WAGENI KUHUSU KILIMO HIKI CHA MITI: Pamoja na taarifa hizi, kampuni
inahamasisha watu ambao ni wageni kabisa na taarifa zihusuzo miti; kutafuta
taarifa zaidi na zaidi kutoka vyanzo mbalimbali kuhusu kilimo-biashara hiki;
ili kujiridhisha kabla ya kufanya maamuzi ya kiuwekezaji.
4. Mnunuzi akishafika na kuyatazama mashamba (au kama anayafahamu
mazingira yalipo mashamba); akishajiridhisha, atasaini mkataba wa makubaliano
ya kimalipo kati yake na kampuni, kisha ataanza malipo mara moja. Baada ya
kukamilisha malipo yake, utafanyika utaratibu wa kupata hati za kimila/mikataba
ya kiumiliki kutoka mamlaka ya baraza la ardhi la kata/kijiji kwa mujibu wa
sheria ya umiliki wa ardhi ya vijiji ya mwaka 1999.
5. Fresh Farms(T) tukiwa na falsafa ya “Greening the world and
Feeding People”; lengo letu ni kuhakikisha tunawasaidia mamia ya watanzania
kutumia fursa ya uboreshaji mazingira; kwa kuwekeza vitega uchumi vya mashamba
vinavyowahakikishia kipato kikubwa sasa na siku za usoni.
6 Kampuni itaendelea kutoa usaidizi wa uangalizi na
utunzaji wa mashamba yote yanayonunuliwa kutoka kwetu kwa utaratibu rahisi na
nafuu kabisa. Nia yetu ni kuona kuwa kila anayewekeza; avune faida ya uwekezaji
wake. Hivyo, hauhitaji kuhofu juu ya usalama wa shamba utakalonunua, popote
utakapokuwepo utajihakikishia kuwa “investment” yako inafanyiwa juhudi kubwa
kuhakikisha inakua.
7. Programu na ofa hii ni ya muda maalumu,
imeanza tarehe 15, Februari, 2013 na itamalizika, Aprili, 14, 2013. Programu
hii inaweza kukoma kabla ya tarehe ya ukomo, ikiwa ekari zilizotengwa zitaisha
mapema. Hivyo kwa yeyote anayehitaji tunashauri kuwasiliana nasi mapema.
Mawasiliano:
Iringa:
Mkurugenzi,
Albert Sanga (0719 127 901, 0766 742 414), albertnyaluke@yahoo.com
Dar es Salaam: Meneja Masoko, Markus Mpangala (0764936655),
mwanazuoni27@gmail.com
No comments:
Post a Comment
Maoni yako