Dorine Otinga |
Na
Dorine Otinga, Eldoret, Kenya
MDAHALO
ulimalizika vizuri mapema Jumatatu wiki iliyopita hapa Kenya, huku wagombea
wote wakionyesha uwezo mkubwa.
Martha
Karua, Raila Odinga, Peter Kenneth, Uhuru Kenyatta ni wagombea waliovuta hisia
za wananchi wa Kenya kutokana na uwezo wao wa kujibu hoja na kuelezea sera zao
iwapo watafanikiwa kushika madaraka.
Takribani
wananchi 328 waliotazama mdahalo huo kwa njia ya runinga wanakubali kuwa
ushindani wa wagombea umekuwa mkubwa. Pia
mdahalo umeboresha uelewa wananchi wa Kenya kujua ni mgombea gani anafaa kuwa
rais badala ya Mwai Kibaki.Siku
chache zilizopita baada ya mdahalo, Taasisi mbalimbali za utafiti ziliendesha
zoezi la kura za maoni juu ya uamuzi wa wakenya kuchagua rais Machi 4, mwaka
huu.
Watu
92% wamekubali kuwa mdahalo kwa njia ya runinga ulisaidia kujua mbinu na uwezo
wa kujieleza wa wagombea wao. Wengine 24% walilazimika kubadili mawazo yao
kwaajili ya wagombea waliodhani watawachagua. Kwahiyo,
mdahalo umeleta changamoto kwa wagombea kuweza kuwapata wapigakura sahihi ili
kuibuka na ushindi. Wapigakura hawa 34% ina maana wamebadili mawazo kutoka kwa
mgombea mmoja kwenda kwa mwingine.
Uhuru Kenyatta |
Pengine
wapo waliopanga kumchagua Musalia Mudavadi au Raila Odinga na Uhuru Kenyatta,
lakini kutokana na kuwatazama na kuwasikiliza kupitia mdahalo, ni wazi wananchi
wamebadili mitazamo juu ya wagombea hao. Profesa
James Kiyiapi alitangaza mageuzi ya elimu ya hapa Kenya. Raila Odinga
alitangaza mageuzi 18 ya kimaendeleo ambayo atayafanyia kazi ipindi akingia
madarakani kuongoza wakenya; elimu bure, afya, na uwajibikaji sekta ya umma. Naye
Martha Karua amekusudia kupambana na ufisadi unaolitafuta taifa letu kwa miaka
mingi sasa. Kwenye mdahalo huo wagombea ambao hawakufua dafu ni Musalia
Mudavadi, Paul Muite na Mohamed Abduba Diba.
Mvuto
wao kwa wapigakura bado dhaifu, haitegemewi kama wataweza kumudu ushindani wa
Uhuru na Odinga. Wakenya 27% wanadhani Uhuru Kenyatta atashinda uchaguzi. Wakenya
26% wanaamini Peter Kenneth atashinda kutokana na kufanya vizuri kwenye
mdahalo. Vilevile 22% ya wakenya wanaamini Raila Odinga atashinda uchaguzi na yeye
ndiye bingwa wa ushawishi hadi sasa akiwa na mgombea mwenza, Kalonzo Musyoka.
Halafu
kuna 12% wanapenda kuona Martha Karua akishinda kuchukua uongozi. Sasa baada ya
kuona hiyo, na sasa tuone suala nyeti ambalo linagusa sana wagombea wa urais hapa
Kenya. Kwanza,
suala la kisiwa cha Migingo ambalo limeleta ugomvi na Uganda ya Yoweri Museven.
Kenya na Uganda zingeweza kuingia vitani kutokana na kuzozania kisiwa cha
Migingo ambacho kimsingi ni chetu hapa Kenya.
Yoweri
Museven alinuia kupeleka majeshi kisiwani Migingo, lakini alisahau kuwa hata
sisi Kenya tunaweza hilo. Mwai Kibaki alilaumiwa kupuuza sana suala la kisiwa
cha Migingo lakini ni vema anaondoka madarakani huku mapigano baina ya Kenya na
Uganda hayakutokea. Suala
hili linachukuliwa kama hatua nzuri ya kulinda amani, lakini haieleweki iwapo
mshindi wa urais Machi 4 atavumilia kama Mwai Kibaki alivyofanya kwa kisiwa cha
Migingo.
Hili
ni suala la nje ya mipaka ya Kenya yetu, lakini yapo mengine yanashiria kuleta
mapigano baada ya uchaguzi. Hofu hii imejaa kwa wengi miongoni mwa wakenya.
Dalili
mojawapo ni mapigano ya kikabila kule Tana River ambako watu 140 walifariki
dunia kutokana na ugomvi wa kuwania mifugo. Hili la Tana River lazima itakuwa
moja ya dalili za kutoelewana kwa wakenya hivyo ukabila kuchukua nafasi hata
kwenye uchaguzi huu. Yapo maeneo ambayo yanaongoza suala la kabila hapa Kenya.
Raila Odinga |
Mfano,
ingawa si sehemu zote, lakini Rift Valley Province kuna ukabila sana. Hofu ni
vita baada ya uchaguzi kutokana na makabila kutoelewana kabisa. Kwa
Rift Valley Province ina makabila nyingi, lakini kabila lenye watu wengi ni
Kalenjin na Wakikuyu, ambao hawajawahi kusikizana kabisa.
Sasa
hawa Wakalenjin na Wakikuyu wamekuwa mwiba kwa miaka mingi kila mmoja akiona
yeye ni bora kuliko kabila lingine. Eneo jingine ni Nyanza Province ambalo kuna
kabila la Wajaluo. Nyanza
hasa eneo la Kisumu City huwa machafuko makubwa yanatokea kwani wenyeji wake
wamekuwa wakifukuza makabila wasiyotaka pamoja na kuchoma maduka ya wahindi.
Kule
Nyanza Province Wahindi ni wahanga wa kwanza wa machafuko kwani maeneo yao ya
biashara yamekuwa yakiharibiwa sana. Imekuwa hivi kwa miaka mingi na sasa
Wahindi hawa wanaona ufikapo uchaguzi ni nyakati zao za kufunga biashara kwa
wale wenye uwezo wanahama kabisa Kenya yetu.
Wengine
huenda huko India na wengine huishi nchi za kigeni kwa muda na uchaguzi
ukimalizika kwa amani wanarejea. Eneo jingine ni Eldoret ambalo lipo Western
Kenya. Kwanza
hapa huwa na hali mbaya zaidi. Hapa Eldoret inasemekana kuna watu wamekusanya
silaha na kujiandaa kwa mapigano baada ya uchaguzi Machi 4. Sio
Al Shabab wala magaidi wowote bali ni watu wa kabila la Kalenjin wanasemekana
kuhifadhi silaha kuwadhuru makabila mengine baada ya uchaguzi iwapo kutakuwa na
ukosefu wa amani.
Martha Karua |
Haya
maeneo mawili Rift Valley Province na Nyanza Provine yanakuwa na machafuko
sana, inatia hofu sisi wananchi wa Kenya namna gani tutaweza kuishi. Wakenya
wenyewe hawapo tayari kuona wanamaliza uchaguzi halafu wanaingia kwenye
machafuko kama mwaka 2007 baada ya uchaguzi. Hatupo
tayari kuwa na machafuko ila kwa dalili zilizopo inatia hofu hatima ya uchaguzi
itakuwaje mwaka huu. Kingine ni hata wagombea kuamiani kuwa kutegemea makabila
yao ndio siri ya ushindi, huku wakisahau inaleta picha mbaya na kusababisha
machafuko.
Raila
Odinga anawafuasi wengi na anategemewa kushinda uchaguzi. Uhuru Kenyatta ndiye
anampa ushindani mkubwa manake ‘ruuning mate’ wake William Ruto hushawishi
Wakalenjin wenzake kumuunga mkono Uhuru Kenyatta. Ruto
hatumii sera ya kushawishi kwa Wakalenjin bali anatumia ukabila wake ili
kuwashawishi Wakalenjin waweze kumchagua Uhuru Kenyatta. Mimi
natokea kabla la Luhya, lakini kura yangu iko wazi nitampa Uuru Kenyatta na ‘running
mate’ wake Willaim Ruto ili waweze kushinda bila kujali, Uhuru ni kabila la
Embu na Ruto kabila la Kalenjin.
Sisi
Luhya tunatokea eneo la Western Kenya kama nilivyosema kuhusu Nyanza Province
na hofu ya machafuko. Raila Odinga anazo sera nzuri kwa wakenya, lakini Uhuru
Kenyatta anaweza kumtisha kwani ameleta sera ambayo itamfanya aungwe mkono na
wasomi wengi wa Kenya, kuanzia wanafunzi wa vyuo vikuu, wahadhiri, na watu wa
sekta ya elimu kwa ujumla.
Uhuru
Kenyatta atapata kura yangu sababu ameahidi akishinda ataondoa Parallel Program
kwa University ili wanafunzi wote waliofuzu walipe pesa sawa. Parallel
program ni mwanafunzi ambaye hakupata alama B ya pointi 61 lakini anafuzu kuwa
University anajilipia zaidi ya laki moja kama karo chuoni. Kwa sera hii Uhuru
Kenyatta anapata kura yangu na atafanikiwa kupata kura nyingi za watu wa sekta
ya elimu kwani atawaondolea ubaguzi wakenya katika elimu.
Wengi
wanakosa kulipiwa karo sababu hawana alama Ba, hivyo hujilipia kiasi cha pesa
wenyewe chuoni. Ninaamini Raila Odinga anaweza kushinda uchaguzi huu, ingawa
wakati uliopita tuliamini na hakushinda kwani ilisemekana Mwai Kibaki aliiba
kura.
Lakini
ushindani anaotoa Uhuru Kenyatta si uchwara kwani amekuwa mwerevu kuelezea
makusudio yake pindi akiingia madarakani, ambayo yanaonyesha kabisa
kuwaunganisha wakenya.
William Ruto |
Kuna
jambo lingine limejitokeza siku chache zilizopita kabla ya uchaguzi ambalo
linatia hofu ya machafuko. Kama kura zinaibwa maana yake itachochea machafuko,
mfano juzi gari ya Mkuu wa IEBC (Electoral and Boundaries Commission), Isaac
Hassan alipigwa risasi, uzuri hakuwa ndani hivyo hilo nalo linaashiria kuna
mambo yatajitokeza baada ya uchaguzi hasa hawa Wakikuyu na Kalenjin wanapenda
fujo na hawajawahi kuelewana.
Sasa
ukiangalia mapigano ya Tana River, watu 140 wamekufa sababu za kikabila na
kugombea mifugo. Halafu hali mbaya ya mji wa Garrissa mpakani mwa Somalia na
hapa Kenya, kisha miji ya Kisumu na Siaya pamoja na eneo la Kibera mjini
Nairobi, ni dalili za wazi kuna mambo uchaguzi ujao.Ni
eneo la Kiberra kule Nairobi ndipo machafuko yalipoanzia mwaka 2008,
tunakumbuka hili na Wakikuyu walikuwa na chokochoko dhidi ya Wakalenjin. Mzee
Daniel Arap Moi naye ni mkalenjin amekuwa akisisitiza wakalenjin waache
mapigano dhidi ya wakikuyu lakini hakuna dalili za kumaliza suala hili.
Moi
anakula pensheni yake ya randi milioni 2.5 sawa na pauni 175,000 anamuunga
mkono Musalia Mudavadi, badala ya Uhuru Kenyatta ambaye alimuunga mkono mwaka
2002.
Kubadilika
kwa Moi kumuunga mkono Mudavadi wa kabila la Luhya ni wazi ameamua kubadili
mbinu za kisiasa baada ya kuona hakuungwi mkono na wagombea wengine. Moi pamoja
na hotuba zake, lakini hawezi kumaliza hofu ya machafuko baada ya uchaguzi.
Na
kwakuwa nitakuwa Voters Clerk uchaguzi wa Machi 4, nadhani nitapata wasaa mzuri
zaidi kuyasoma mawazo ya wapigakura na mwenendo mzima wa uchaguzi wetu hapa
Kenya.
Lakini
hofu kubwa itakuwa kwa wafuasi wa Uhuru Kenyatta na Raila Odinga, kati ya
Wakalenjin, Wajaluo na Wkikuyu. Kuna hofu ya mchafuko hapa. Kwa mfano, Februari
15, Raila Odinga alitembelea watu wa jamii ya Embu ambako ni kabila la Uhuru
Kenyatta, kulitokea rabsha, kama si juhudi za Polisi, basi Odinga angetimuliwa
kwani wanamtaka Uhuru Kenyatta tu.
Dorine
Otinga ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Egerton nchini Kenya na atakuwa miongoni
mwa wasimamizi wa uchaguzi ujao.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako