January 18, 2018

KABWILI ASINGEKUBALI KUFUNGWA PENATI TANO ZA URA.

Na. HONORIUS MPANGALA
MIONGONI mwa utofauti ambao binadamu tunao ni jinsi ya kuzitumia akili zetu. Utofauti huo huweza kumtofautisha yule mwenye uwezo mkubwa katika kubaini jambo na kutafuta ufumbuzi na mwingine kubaini jambo kunachukua muda na kulifanyia ufumbuzi. Licha kuaminika kuwa tuko sawa lakini katika baadhinya nyanja hatuwezi kuwa sawa ndo maana wako warefu na wemgine wafupi ukiwalinganisha hao unapata utofauti. 

Yanga moja ya akili kubwa waliyoitumia kufanikisha saini ya Ramadhani Awam Kabwili Kwa mkataba Wa miaka mitano. Sijajua nani alisimamia kusaini Kwa Yohana Nkomola maana nilifikiri nae wangemalizana nae Kwa mtindo kama Wa Kabwili. Hata hivyo Kwa vile yuko katika milki yao wataweza kutenda jambo nae siku za usoni.


Licha ya mashaka makubwa wanayokuwa nayo mashabiki dhidi ya wachezaji vijana katika vikosi mbalimbali vya timu,ila hao ndio watu makini sana katika kitenda licha ya kwamba kuamua jambo kwao kunaweza kuwa na wasiwasi Wa hofu ya kuogoa kukosea. Wapo ambao wanakuzwa katika misingi ya kuamua Kwa kutenda Kwa wakati na kuamua Kwa ufasaha licha ya umri wao kuwa mdogo.

Katika umri Wa miaka 17 Mashabiki Wa Atletico Madrid walitia shaka dhidi ya David De Gea kulinda lango lao katika ligi Kuu ya Hispania. Katika umri huo huo mashabiki Wa Ac Milan nao walijikuta wakiingia katika hofu ya kimaamuzi Kwa kipa wao Gianluigi Donnarrumma. Pia Atletico nyakati hizi wakawa kidogo mashaka yamewapungua wakaona Kocha akimpa nafasi Thibaut Cortous. 

Hofu mashabiki inakuja kutibiwa na maamuzi yenye msimamo ma yasiyoyumbishwa na kocha wenye elimu ya soka na mwenye kujiamini na kazi yake bila kuhofia kelele za mashabiki. Katika mazingira hayo hayo Manchester United ikafanikiwa kunasa saini ya David De Gea akiwa na umri Wa miaka 19. Kujiamini Kwa Ferguson pamoja na benchi lake LA ufundi ndiko kulikowafanya waamue kumpa nafasi kipa Huyo. Na uzuri wa mashabiki wa ulaya ni wenye kuheshimu na wanaojali taaluma ya mtu 'professionalism'. Hapa ndipo uatakapoona utofauti wa mashabiki wetu na makocha wetu katika soka.

Kwa kiasi kikubwa maamuzi makubwa yanayofanywa na makocha wetu yanakuwa na mihemko ya mashabiki. Hii inatokana na kufanya kazi Kwa kusoma akili za mashabiki wa timu zao zilivyo Mara pale mambo yanapokuwa tofauti. Mfano wakati wa mashindano ya Mapinduzi mashabiki wengi wa Yanga walimuulizia sana Obrey Chirwa na kudiriki kusema nafasi wanazotengeneza laiti angekuwa nyota wao huyo basi wasingeweza kusumbuliwa na Zimamoto,au hata JKU. 

Hii ni kutokana na imani yao Kwa mchezaji wao katika kutumia nafasi.Sasa kukosa Kwa penati na mchezaji Huyo katika mechi ya nusu fainali kukaibuka picha na kejeli zilizomhusu Chirwa Kwa kuambiwa Kwa kipindi alichokuwa kwao Zambia alikuwa shambani akilima Mahindi.Sitaki kumlaumu Chirwa katika kuoneka timu yao kaitoa katika nusu fainali Mimi jicho langu limeenda Kwa mlinda mlango wao Youthe Rostand.

Kwa makipa kutoka nje ya nchi ambao wamekuwa na Bahati na jina lao kuimbwa na mashabiki wa Yanga inapokujs suala la penati basi ni Mghana Yaw Berko. Kipa huyo alizijulia haswa penati. Pia makipa wazalendo kama Deo Munishi ambaye katika hali ya mchezo ilikuws huwezi kumfunga penati tano zote.

Licha ya kuonekana mdogo Kwa umri lakini akili yake ni kubwa sana kijana huyu Kabwili. Uwezo wa kimaamuzi na jinsi anavyoweza kuongea na wachezaji wake wakati mchezo ndipo unapoona ukubwa wa akili ya Kabwili katika kuwamudu wachezaji wa Yanga licha ya yeye kuwa mdogo kiumri.
Iliwahi kumuwia vigumu Kwa David De Gea kuweza kuongea na mabeki kama Rio Ferdinand na Nemanja vidic lakini alizoea na hatimaye akaweza. Hivyo hivyo ilikuwa ngumu Kwa Kabwili kuongea na 'watu chuma' kama Kelvin Yondani na Nadir Horoub 'Cannavaro'. 

Wakati mapinduzi inaanza asilimia kubwa watu ya wapenzi hata Kwa wataalamu wa soka waliamini kuwa ni nafasi Kwa wale ambao hawakutumika katika michezo ya ligi Kuu. Jambo pekee lililotakiwa kufanyika ni makocha wa hizo timu kwenda kufanya maamuzi ambayo yangekuwa ni ya faida Kwa klabu zao.

Wachezaji ambao ambao walipaswa kucheza mashindano Yale Kwa uoande wa Yanga ni pamoja na bwana mdogo Kabwili hakukuwa na ulazima wa kumtumia Rostand katika mashindano yale. Katika jambo hilo pia usingeweza kuona Kwa Kabwili kufungwa penati zote tano dhidi ya URA Kwa jinsi alivyo mwepesi katika 'javellin' Kwa kila upande.

Kipa wa Yanga aliigiwa penati nyepesi sana wakati yule wa URA alipigiwa penati nngumu sana. Sio kama nawasifia wapigaji wa Yanga kirahisi hapana ila wale wapigaji walijua kipa wa URA ni mzuri sana langoni kwake hivyo angeweza kufanya kama alichokifanya Kwa Chirwa Kwa wachezaji wengine.
Ingelikuwa maamuzi mazuri Shadrack Nsajigwa na wenzake kuamua kumwacha Kabwili acheze michuano yote hadi mwisho. Hata penati ambazo zilipogwa dhidi ya URA ninahakika Kabwili asingekubali zote zipenye katika manega na kwapa zake.

Kwa afya ya Yanga ni vyema wakaitazama upya nafasi ya Kabwili. Udogo wake wa umri haumfanyi akashindwa kuitumikia klabu hata kwenye mashindano makubwa. Nimefuatilia na kugundua Rostand anafungwa magoli mepesi na yale mazingira magumu huwa anafanya vyema . lakini Kabwili ana uwiano wa kimatukio katika mchezo nyakati zote awapo uwanjani.

Wakati Alex Ferguson jicho lake likiwa Kwa golikipa Manuel Neuer wakati akiwa Schalke 04 basi mmoja wa maskauti wa Man utd alikuwa amemuona De Gea na kumweleza Ferguson kuwa asisumbuke Kwa Neuer. Alisema hayo akijiamini Kwa kutazama miaka mingi mbele kuwa atakuja kuwa kipa bora sana duniani kulingana na uwezo wake wa kumudu mechi akiwa katika umri mdogo kama ule aliomuona wa miaka 18. 

Kitu pekee kinachohitaji Kwa vijana hawa ni kuwapa nafasi na pia mashabiki watambue vijana wanamuda wa kujifunza ili kuwapa faida. Kila Mwana Yanga anakumbuka jinsi alivyozomewa Simon Msuva siku za mwanzo lakini Leo hii ameondoka kola mmoja anasema wazi pengo la Msuva ni ngumu kuliziba,wameamini kuwa walikuwa wanakosea kumzoea mapema vile.

Kabwili anaweza kuwa mzuri sana kuliko hata Rostand ,ila jambo pekee analozidiwa nalo ni umri Na mwili na mmoja kutoka Cameroon na mwingine Tanzania lakini uwezo wao Mimi naamini Kabwili ni zaidi ya Rostand. Uwezo wa Rostand akiwa African Lyon nauona ni toauti na huu yawezekana alikuwa sokoni ili apate timu kubwa na acheze Kwa kupumzika tu.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako