September 28, 2017

SOKO MAARUFU LA MWANGA KIGOMA MJINI.



Nilikuwepo tutaonana siku nyingine mungu akinirejesha tena katika Ardhi hii ambayo nafurahi kuijua,hakuna tofauti na kwetu Songea kijiografia na hata hali ya hewa kama nyumbani Lundu, Nyasa.

Nawaandalia bonge la makala kuhusu soka la Mkoa wa Kigoma baada ya kukutana na Mdau mkubwa NASSORO HAMDUNI,mwamuzi na diwani wa manispaa ya Kigoma/Ujiji..

Na Honorius Mpangala

September 27, 2017

SOMO LA LEO

Usiwadharau wasaidizi wako.... Maana ni wao wanatengeneza sehemu ya sifa yako bila kujali unao uwezo mkubwa au mdogo. Wanaweza kukusitiri au kukuangusha.

UHONDO WA KITABU

Wahenga wanasema kitabu ni sila. Mwanamke huyu alikutwa akisoma kitabu ndani ya Basi la Mwendokasi kati ya Mbezi-Posta kupitia barabara ya Morogoro jijini Dar es salaam. 
Usomaji wa vitabu huongeza maarifa.

Mwanamke huyu alikutwa akichagua kitabu cha kujisomea katika eneo la Mbezi jijini Dar es salaam.

Huyu alitafuta eneo zuri kwake linalomwezesha kusoma kitabu kwa utuvuli.

PICHA ZOTE NA KIZITO MPANGALA
 

MAKAZI DUNI

Hii sehemu mojawapo iliyopo jijini Dar es salaam. Ni eneo la makazi duni yaliyopo katika jiji hilo.

MASHUJAA SONGEA

Mwanazuoni Edgar Mwandemani akiwa katika mnara wa askari ulipo katika uwanja wa Mashujaa mjini Songea.

KAMATI KUU CCM KIKAONI LEO IKULU




Mwenyekiti wa CCM, John Magufuli ameongoza kikao cha Kamati Kuu leo Ikulu jijini Dar es slaa. 


SALUM MWALIMU ASHINDA KESI



BARIADI: Kesi Na. 158/2016 iliyokuwa inamkabili Naibu Katibu Mkuu (CHADEMA) Zanzibar ndugu Salum Mwalimu na wenzake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bariadi imetupiliwa mbali, hivyo basi washtakiwa wote wako huru kwanzia leo 27 Septemba 2017.

HOJA 10 ZA WABUNGE WA CHAMA CHA NRM


KAMPALA, UGANDA

1. Acha "Mamlaka ya Raia" iamue. Kuweka ukomo wa umri ni kuwanyang'anya ni kuwanyima mamlaka yao ya Kikatiba.
2. Uhuru wa Raia kuchagua wampendae uheshimiwe. Kama hawampendi kura zitaamua.

UCHAMBUZI WA KITABU CHA THOMAS FRIEDMAN



KITABU: HOT, FLAT AND CROWDED
MWANDISHI: THOMAS L. FRIEDMAN
MCHAMBUZI: MARKUS MPANGALA

SUALA la mabadiliko ya tabia nchi ni nyeti duniani. Kutoka na unyeti huo Thomas L Friedman aliandika kitabu hiki cha “Hot,Flat and Crowded”. Kitabu hiki kilichapishwa Septemba mwaka 2008 na kampuni ya Farrar, Straus and Giroux na kikapewa nambari ISBN 978-0-374-16685-4.

Thomas L. Friedman aliandika kwa kwa namna tofauti na kitabu cha kwanza alichozungumzia dhana ya utandawazi yaani .The World Is Flat’. Akiongelea mapinduzi ya teknolojia. Ndani ya kitabu cha “Hot,Flat and Crowded” anazungumzia mabadiliko ya hali ya hewa yaani Tabia-nchi na kuibuka kwa ushindani wa nguvu za nishati ambazo huleta madhara makubwa kwa afya za wanadamu duniani.

ADHABU KWA MWENDESHA BAISKELI




Jana mchana mwendesha Baiskeli alipita kwa kasi katika makutano ya barabara ya Bibi Mohammed na Morogoro bila kuruhusiwa na taa za kuongoza magari. Wakati anapiga taa zilionyesha magari yapite, na yalikuwa yakipita kwa mwendo kasi mno, kiasi kwamba ingetokea gari linalopita basi angegongwa na kusababisha matatizo makubwa.

September 25, 2017

MAPIGANO YAENDELEA KATI YA WANAMGAMBO WA MAIMAI NA JESHI LA TAIFA

MAPAMBANO MAKALI yanaripotiwa kati ya jeshi ya Congo FARDC na waasi wa maima wa YAKUTUMBA katika maeneo ya wilaya ya Tanganika tarafani fizi, Katika mkoa wa Kivu ya kusini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Taarifa zenye uhakika zaeleza kuwa waasi hao wamevizibiti vijiji kadhaa ikiwemo mji wa Mboko.
 
Hofu na wasiwasi unazidi kutanda kwa raia wamaeneo ya Lusenda,mboko ,a hata SWAIMA ambapo jeshi lataifa FARDC linakabiliana na wapiganaji wa kundi la Maimai CNPS linaloongozwa na Yakutumba. Duru zenye kuaminika zaeleza kuwa makabiliano yalianza hio jana mapema alfajiri,wakati wapiganaji hao wa maimai waliposhambulia ngome kadhaa za jeshi la taifa katika mji wa Mboko na kuuzibiti. 

UCHAMBUZI WA KITABU; BUSARA ZA MZEE


KITABU: BUSARA ZA MZEE
MWANDISHI: TITUS AMIGU
MCHAMBUZI: KIZITO MPANGALA

BUSARA ZA MZEE ni kitabu chenye mkusanyiko wa aya mbalimbali ambazo zimekusanywa katika nyakati tofauti na kuwekwa kitabuni. Ni kiatabu ambacho kimechapishwa na Moccony Printing Press jijini Dar es salaam, Tanzania na kupata namba ya usajili ISBN 978 9987 9639 7 3 ambapo kimechapishwa katika kurasa 281.

Mwandishi anasema busara hizi amezikusanya na kuzieleza, na zile zinazoeleweka moja kwa moja basi ameziandika bila maelezo. Buasara hizi amezipata sehemu mbalimbali; amezipata kwa kuwasikia watu wakizungumza mara kwa mara, zingine amezipata kwenye magari alipokuwa akisafiri katika safari mbalimbali akiwasikia abiria wenzake wakipeana michapo, zingine amezipata vilabuni, zingine amezipata kwenye nguo kama vile kanga, zingine amezipata kwenye mabango ya pikipiki na bajaji na kadhalika. Zote ni busara.

Mwandishi amenuia kusema busara mbalimbali kwa watu wote kwa ujumla katika ulimwengu huu ili waweze kupata mafundisho ambayo hawatajutia kuyapata. Ni mafunzo yenye nia njema na yenye kujaa tafakari mbalimbali kulingana na ujumbe unaopatikana katika busara husika. Kwanza mwandishi anawaasa watu wote kumkalibia muumba wa mbingu na dunia hii ili wajazwe furaha na amani zaidi katika maisha yao.

Mwandishi ameandika busara nyingi, ni ngumu kuzieleza zote kila moja kwa nafasi yake. Lakini tutapata baadhi tu. Mwandishi anasema kama mtu anafanya jambo fulani lenye manufaa katika maisha yake basi alifanye kwa morali zaidi ili afaidi matunda yatokanayo na jambo hili kwa furaha na amani.



September 23, 2017

TANZANIA IS RAPIDLY CLOSING ITS ECONOMIC GAP WITH KENYA



BY GABRIEL MWANG’ONDA

Kenya’s status as East Africa’s economic powerhouse is at stake as Tanzania races closely behind, with a higher growth rate that is increasingly narrowing the gap between the two economies.
Tanzania has added impetus to its economic firepower, growing by an impressive seven per cent over the past five years compared to Kenya’s growth of just above five per cent.

The latest International Monetary Fund (IMF) data shows that Tanzania’s economy expanded seven times in the past 20 years while Kenya’s output grew five times since 1997 with the trend expected in coming years, weakening Nairobi’s future dominance. The same data shows that there were times in the past when Kenya’s economy would be as many as four times as large as that of Uganda.
However, such a big gap has not been reached in many years and is has remained mostly below three times.

HONGERA DKT ASHA-ROSE MTENGETI MIGIRO.


UN-High Level Advisory Board on Mediation ni nini?
Siku ya tarehe 13/09/2017 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ndugu Antonio Guterrez alitangaza kuanzisha bodi mpya ambayo inaitwa Bodi ya Ushauri ya Masuala ya Upatanishi ya Umoja wa Mataifa-UN.

BODI HII NI NINI HASA?
High Level Advisory Board on Mediation ni bodi iliyoanzishwa kwa lengo la kumshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya juhudi za upatanishi sambamba na kumpa mrejesho juu ya upatanishi duniani.
Bodi hii inaundwa na wajumbe 18 wakiwemo viongozi wa sasa na wastaafu, maafisa wa ngazi za juu na wataalamu mbalimbali kwa lengo la kuunganisha uzoefu, mbinu, maarifa na mawasiliano.

Wajumbe wake ni hawa wafuatao;
(1) Rais Michelle Bachelet wa Chile.
(2) Radhika Coomaraswamy-Mwanasheria wa Kimataifa wa Sri Lanka.
(3) Leymah Gbowe-Mshindi wa Nobel toka Liberia
(4) Jean-Marie Guehenno-Mwanadiplomasia wa Ufaransa
(5) Tarja Halonen-Rais wa kwanza mwanamke wa Finland 2000-2012
(6) David Harland-Mkurugenzi Mtendaji Centre for Humanitarian Dialogue.
(7) Noeleen Heyzer-Mjumbe Bodi ya wadhamini Chuo Kikuu cha Singapore 2013-to date.
(8) Nasser Judeh-Seneta Bunge la Jordan.
(9) Ramtane Lamamra-Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria 2013-2017.
(10) Graça Machel-Mpigania Uhuru wa Msumbiji...
(11) Asha-Rose Migiro-Balozi wa Tanzania UK
(12) Roden Muhammad Marty Muliana Natalalegawa-Indonesia
(13) Olusegun Obasanjo-Rais Nigeria 1999-2007.
(14) Roza Otunbayeva-Rais Mstaafu Kyrgyzstan.
(15) Michel Pierre-Louis- Haiti
(16) Jose Manuel Ramos-Horta- Timor ya Mashariki
(17) Gert Rosenthal-Ujerumani
(18) Justin Welby-UK
Ni imani yetu kuwa migogoro mingi itapata upatanishi wa haraka na wa kudumu.

©Uwanja wa Diplomasia.

September 22, 2017

USHAURI WA BURE KWA TFF

NA SAMWEL CHITANYA

MOJA kati ya nchi za Afrika ambazo raia wake wanapenda sana mchezo wa kandanda  duniani ni Tanzania. Watanzania wanaupenda sana mchezo Wa kabumbu. Ni mchezo unaopendwa na watu wengi duniani kote. Unaongoza kwa kupendwa.

Bahati mbaya sana pamoja na Watanzania kuupenda mchezo huu bado hawana mipango madhubuti ya kuufanya mchezo huu uwe wenye tija kwao. Mipango yao mingi ni yakucheza mpila na Siyo Mpira kama wenzetu wanavyo Fanya.

Timu yetu ya taifa huwa inashiriki katika kupigania nafasi ya kushiriki mashindano mbalimbali kama vile Kombe la dunia, kombe la mataifa Afrika na kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji Wa ligi za ndani.

Timu yetu hushiriki kikamilifu katika kuwania nafasi zote hizo. Tunajiamini kuwa Tuna timu bora ambayo inaweza kufanikiwa kufuzu mashindano yote hayo. Kujiamini siyo jambo baya lakini jitazame na uwezo wako kwanza.
Mara ya mwisho Tanzania kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika ilikuwa mwaka 1980. Miaka thelathini na saba(37) sasa imepita tangu tushiriki mashindano makubwa zaidi ya soka katika bara letu.
Kiungo mkabaji wa Taifa Stars, Himid Mao Mkami 

NIMEWATEMBELEA WAKONGO NA BURUNDI LEO


Fredy Msumba anasema , "Leo niliona niwatembelee ndugu zetu wa Kongo na Waburundi, maisha ndo hayo, big up Tanzania, I love Tanzania. Karibu Kigoma bado nipo. Nakuambia kaka, ukija huku hutatamani kurudi Dar es salaam, ndio maana hawa jamaa hawataki kurudi kwao, kuzuri sana huku.