Na KIZITO MPANGALA
Kila mmoja anatamani kuendeleza
siri kubwa ya taarifa zake katika simu yake au tarakilishi (kompyuta) yake ili
zisijulikane na wengine. Ulizni wa taarifa hizo husaidiwa na nywila (password).
Nywila (password) inaweza kuwa ya haerufu tupu, namba tupu au mchanganyiko wa
herufi pamoja na namba na baadhi ya alama za uandishi kama vile mkwaju (/) na
kadhalika. Nywila ina umuhimu mkubwa katika ulimwengu huu wa Sayansi na
Teknolojia ingawa ilianza kutumika zamani ila siyo kwa kiwango kikubwa kama
ilivyo sasa.
Kabla ya kuboreshwa kwa
teknolojia ya mawasiliano, zamani password ilijulikana kama “passphrases.”
Kwa hiyo nywila ni ufunguo unaolinda lango la kuingilia katika kuzijua taarifa
zako ili zisivamiwe na wengine (hackers). Hii ni kwa ajili ya usalama wa
mawasiliano yako. Kila mmoja duniani ambaye anatumia tovuti au kurasa
mbalimbali hukutana na kipengele cha kuingiza password ili apate
anachokihitaji. Malengo ya nywila (password) ni:
1. Kukupa
ruhusa ya kuingia kwenye akaunti husika unayaotembelea,iwe ya kwako au ya mtu
mwingine au kikundi au kampuni.
2. Kuipa
ruhusa barua pepe ifunguke ili kuona taarifa zilizomo. Baruapepe inaweza kuwa
ya kwako au ya mtu mwingine kadiri ya maelewano kati yenu.
3. Kulinda
vifaa vya kielektroniki ili visitumiwe na wengine ikiwa mmiliki hapendi
vitumiwe na wengine. Vifaa hivyo ni kama vile simu, tarakilishi (kompyuta),
tarakilishi mpakato (laptop), ubamba (tablets) na kadhalika.
4. Kupata
mtandao (network) ikiwa itahitajika kutumia password.
5. Kulinda
tovuti ili isiingiliwe na wengine (hackers)
6. Ulinzi
wa data binafsi, za kikundi au za kampuni fulani.