November 15, 2017

G40 HOI. GRACE MUGABE AKIMBIA NCHI



Kwa mujibu wa taarifa ya Kituo cha Skynews kimesema kuwa Mke wa Rais Robert Mugabe,  Bi.Grace Mugabe ameondoka nchini Zimbabwe na kuelekea Namibia ikiwa ni saa chache baada ya Jeshi la Nchi hiyo chini ya Jenerali Costatino Chiwenga kuchukua madaraka kwa muda. 

Grace ambaye alikuwa kiongozi kundi maarufu la wanasiasa la G40 ndani ya chama cha ZANU-PF na kusababisha mgogoro mkubwa wa madaraka, ameondoka huku wenzake watatu wakishikiliwa na Jeshi (hata majina hayajatajwa).
Aidha, Grace alikuwa na uchu wa kuingia mdarakani, na ametajwa kuwa kiini cha kutilimuliwa makamu wa rais, Joice Mujuru na Emmerson Mnangagwa.
Grace Ntombizodwa “Mugabe”  alizaliwa mwaka 1965 nchini Afrika Kusini na kuolewa na Mugabe mnamo 1996. Wawili hao walibarikiwa na watoto 3. Watoto wawili wa kiume na mmoja wa  kike. Aliwahi kuolewa na rubani Stanley Goreraza.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako