Showing posts with label Kilimo. Show all posts
Showing posts with label Kilimo. Show all posts

January 06, 2018

NYASA NI MAARUFU KWA KILIMO CHA MATUNDA

 
Hapa ni kijiji cha Ndengele katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma tulimkuta kijana anauza ndizi mkungu mzima shilingi 2000 tu.


Katika eneo la Liuli tulikuta mananasi matatu yanauzwa shilingi 1000.

NB; Albano Midelo

November 16, 2017

MV NJOMBE INAVYOFUNGUA FURSA KWA WAKAZI ZIWA NYASA.


Honorius Mpangala, 0628994409

NA. HONORIUS MPANGALA
AKIWA katika kampeni za urais mwaka 2005 Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete katika ardhi ya Kyela Mkoani Mbeya alihaidi meli. Alirudia tena kauli hiyo alipokuwa katika ardhi ya Mbamba Bay Mkoani Ruvuma. Baada ya kipindi cha utawala wake hatimaye meli alizoahidi tayari zimeonwa na Wanyasa. 

MV Njombe imekamilika na kufanikiwa safari moja ya majaribio kutoka Bandari ya Itungi hadi Mbamba Bay.  Yapo mambo ambayo ni fursa kwa wakazi wa Nyasa kutokana Meli hii. Kama inavyoitwa ni meli ya mizigo ni chombo kitakachoweza kuwainua kiuchumi wakaza wa Nyasa kama watakitumika ipasavyo. Kuinuka kiuchumi kutatokana na kujikita katika shughuli ambazo wakazi wake watajishughulisha na shughuli kama ilivyo kilimo biashara na hata ufugaji wa kisasa na wenye tija katika maisha ya leo.
Kilimo cha biashara ni moja ya ujasiriamali ambao watu wengi wamekuwa wakijishughulisha nao. Katika mwambao wa Ziwa Nyasa hususani wilaya Nyasa yapo mabonde ambayo yanaweza kufanyika kilimo cha mazao ya muda mfupi na kwa mfumo wa kilimo cha umwagiliaji, na kile cha kutegema mvua na kuleta tija.


November 15, 2017

MANISPAA YA SONGEA KUNUNUA MAHINDI TANI 400

NA MWANDISHI WETU, SONGEA
 
HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imepangiwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula(NFRA) katika msimu huu kununua mahindi tani 400.
Picha kwa Hisani ya Manispaa ya Songea.
Afisa Kilimo wa Manispaa ya Songea Mushoborozi Christian amesema Halmashauri hiyo imepokea barua toka NFRA inayotoa maelekezo ya ununuzi wa mahindi katika awamu ya tatu msimu wa mwaka 2017/2018.

October 17, 2017

TAKWIMU MUHIMU ZA WILAYA YA NYASA HADI OKTOBA 2017


1. Total Number of Hamlets in the District = 425

2. Total Number of Households for Nyasa dc = 31,146

3. Total Female Population for Nyasa dc = 74,768.


4.Total Male Population for Nyasa dc = 71,392.

5. Total Population for Nyasa dc = 146,160.

6. Total Number of Secondary school = 14

7. Total Number of Primary School = 106
Total Number of Villages = 84


8. Total Number of Ward = 20

9. Total Number of Division = 3

CHANZO: Nyasa dc statistics

December 23, 2014

BAADHI YA MANDHARI YA WILAYA NYASA





Picha na 
Cuthbert Zillale


August 24, 2014

"CHANGAMOTO ZA KILIMO NA WAKULIMA - NYASA"


Na Vitus Matembo, Mbamba Bay
MBOLEA YA RUZUKU: Wakulima wengi wa Nyasa hawaitumii mbolea ya Ruzuku ya Serikali, na kuwaachia watu toka Mbinga kuja kuichukua. AJABU, Mtu akitumia na akapata mavuno mengi. Wanafikiria ni WIZI WA KISHIRIKINA.
UVIVU: Namnukuu Mkuu wa Wilaya, Mh.ERNEST KAHINDI, huwa anasema daima "Wakulima wengi ukanda wa Ziwa Nyasa ni Wavivu kwakuwa hufanya kazi kwa muda mfupi, yaani toka saa 12.00 asubuhi hadi saa 3:00 asubuhi. Tofauti na maeneo mengne wanaotegemea Kilimo".
NYANYA TOKA NYASA HAZINA UBORA NA HUOZA MAPEMA: Wakulima wengi wanajitahidi kulima Nyanya ila kutozihudumia ipasavyo na madawa husababisha wafanyabiashara toka Nyasa kununua Nyanya toka Mbinga na Songea. Wakati Nyasa kuna mito na ardhi nzuri.

KILIMO CHA KOROSHO: Nakumbuka Meja Generali Mstaafu S.S.KALEMBO aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma alihimiza sana Wanyasa tulime zao la Korosho kwakuwa ardhi ya Nyasa ni nzuri kwa kilimo hicho kama ilivyo Tunduru, Lindi na Mtwara. Ila sijajua tatzo nini?.

KILIMO CHA MIWA NA KIWANDA CHA SUKARI LUNDO JAMANI KIMEKUFAJE.

KILIMO CHA TUMBAKU SIJUI KIMEFIA WAPI KULE RUHEKEI.

January 29, 2014

UGAWAJI VIWANJA ZAIDI YA 200 KILOSA KWA WAFANYAKAZI WILAYANI NYASA




Na Vitus Matembo, Kilosa
Halimshauri ya wilaya imeendelea na mchakato wake wa kuuza baadhi ya maeneo kwa wananchi ambao watakuwa tayari kuyanunua. Uuzaji huo umelenga kuyaweka maeneo ya wilaya katika vipimo na mipango miji ambayo itasaidia kuepukana na majanga.

Kwa sasa Nyasa kuna viwanja vinagawiwa kwa wafanyakazi wa Serikali. Wanaanza wa Halmashauri na Mkuu wa Wilaya, sasa walimu. Nakusihi wewe Mnyasa uliye Mbali kama ni mfanyakazi wa Serikalini andika barua ya maombi kwa Mkurugenzi wa wilaya Nyasa. Gharama haizidi shilingi 80,000.