Showing posts with label maisha. Show all posts
Showing posts with label maisha. Show all posts

March 07, 2018

JOSEPH BOIMANDA: MTAJI WA MILIONI HAMSINI SERIKALI HAWANA MUDA WA KUKUFUATILIA

NA.HONORIUS MPANGALA
MAISHA popote unaweza kusema hivyo kwani waliofikiria katika hoja hii walikuwa na sababu za msingi zilizokuwa na maana kiuhalisia. Wakati kipato ndio sababu hasa zilizopelekea kukawa na maneno kama haya ambayo yanasadifu uhalisia wa maisha. Katika mazungumzo yangu na mmoja ya watanzania waishio nchini Afrika kusini ilinifanya nistaajabu kile anachonieleza ambacho ndio uhalisisa wa maisha ya huko.

Ni rafiki yangu na ndugu yangu Joseph Boimanda alinifanya nistaajabu pale aliposema mtaji wa milioni hamsini za kitanzania ukiwa Afrika Kusini sio lolote kwa serikali ya huko. Maisha yamekuwa yenye uhuru na amani ya kutosha kwa raia.
Wakati nataka kuyajua haya ananieleza kuwa mamlaka ya mapato ya huko haina muda wa kufuatilia mfanyabiashara wa kati.Kama inatokea mtu anataka kulipa mapato serikalini basi ni hiari yake,hii ni kwa wale wafanyabiashara wadogo na wa kati amabao mtaji yao ni kitu kidigo kwa serikali yao. 

February 28, 2018

NAFASI ZA KAZI MAMLAKA YA BARABARA VIJIJINI "TARURA" MKOA WA RUVUMA

 
 

February 26, 2018

WAMACHINGA WA KIZUNGU NDANI YA MJI WA MOROGORO

Nimewanasa mwenyeeeeewee kwa kamera yangu. Msamvu Morogoro,wanauzia bidhaa abiria Wa kwenye magari. Jana nilimnasa mmoja katika mgahawa uliopo maeneo Stand ya daladala ya mjini kati moro nami nikawa mmoja wa wateja wake. Wakati sisi tukiwashangaa wenzetu wanapiga hela wanaondoka. Vyuma vimepata grisi ya kizungu.
 PICHA; Honorius Mpangala

February 16, 2018

MBUFU NI AINA YA SAMAKI KUTOKA HAPA KWETU NYASA


Upikaji wa samaki hawa hauhitaji kitunguu wala nyanya au mafuta. Wanapikwa na kulika vizuri, hawahitaji mafuta ya kupikia, nyanya wala vitunguu na vikorombwezo vingine vya mapishi. Ukitumia viungo hivyo basi utakuwa umeharibu kabisa ladha yake na kupoteza asili yake. Ni samaki watamu mno.

February 14, 2018

TAULO ZA KIKE

NA MAUNDU MWINGIZI
LEO nimekumbuka moja kati ya matukio yaliyopata kuniumiza sana hapo zamani. Nakumbuka nilikuwa darasa la sita, Shule ya Mazoezi Mwenge, mkoani Tabora.

Siku hiyo, nikiwa nimeketi dawati la mbele kabisa darasani, lilizuka kama zogo maeneo ya katikati ya darasa; wanafunzi wakawa wamesimama; wengine wakicheka, wengine wakionekana kufadhaika. Kusogea eneo la tukio, nikamwona binti mmoja (jina ninalihifadhi) akiwa ameketi juu ya dawati ilhali wenziye wakiwa wima wamemzunguka.


Nikiwa sijatanabahi juu ya kilichotokea, baadhi ya wasichana wakamwinua mwenzao, kisha wakamfunga sweta kiunoni ili limsitiri sehemu ya nyuma. Aliposimama, ndipo nikaona kilichotokea. Damu ilienea kwenye sketi yake huku nyingine ikibaki kwenye dawati. Wenziye kadhaa wakaungana naye kumsindikiza nje ili kumpa nguvu. Lakini mambo ya kitoto, bila kujua hofu na fadhaa vilivyomuathiri kisaikolojia mwenzetu, baadhi (hususan wavulana) wakawa wakishangilia na kumcheka.

February 10, 2018

MIAKA 72 NA UBORA WA WAHANDISI WA KIJERUMANI PAMOJA NA WAASHI WA TANGANYIKA KIJIJINI LUNDU

NA KIZITO MPANGALA
MIAKA 72 tangu jengo hili la kiroho liliponengwa halijaleta usumbufu kiujenzi. Msingi wake ni imara. Ni mwaka 2005 pekee jengo hili liliathiriwa na kimbunga (chinangunga) ambapo ni paa pekee liliharibiwa na ni sehemu ndogo sana iliyoathiriwa. Ilikarabatiwa kwa muda mfupi na kukamilika. Boriti zake kwenye paa hata watu 10 boriti moja hawawezi kunyanyua. Huu ni uhandisi wa Wajerumani.

Tazama upande wa juu kuna msitari mweusi umenyooka ukutani hapo. Hii siyo rangi kusema kwamba imepakwa. Hayo ni matofali yaliyoiva na kuzidi viwango vya ubora, na ni ngumu kwa matofali haya kuvunjika kirahisi. Hivyo msitari huo hapo juu ni urembo tu kiujenzi.

Kuni ambazo ni bora sana kuchomea matofali ni Miyombo. Miti hii ipo katika vinasaba vilivyopo kwenye makundi mawili. Kuna Myombo ambao mara nyingi huzalisha aina fulani ya kamba (mighoyi) ambazo zina matumizi makubwa sana katika jamii ya watu wa Nyasa. Aina ya pili ni Myombo unaoitwa "Mpangala", mti huu pia ni dawa nzuri sana endapo utasumbuliwa na tumbo hasa kwa wanaoharisha. Mimi ninatumia sana dawa hii pamoja na Mwarobaini.

January 28, 2018

UTAFITI: SIGARA MOJA HUSABABISHA UGONJWA WA MOYO NA KIHARUSI

WATU watu wanaovuta Sigara angalau moja kwa siku wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya moyo kwa asilimia 50, huku wengine wakiwa na uwezekano wa kupata ugonjwa wa Kiharusi kwa asilimia 30 kuliko wale wasiovuta kabisa.
 
Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na Taasisi ya Saratani ya Chuo Kikuu cha London, umeonyesha kuwa hakuna kiwango cha usalama kati ya uvutaji wa sigara na kupata magonjwa tajwa. lakini umeeleza kuwa mtu anayeachana na uvutaji wa sigara hayupo katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo au Kiharusi.
Wamesema, asilimia 48 ya vijana wanaovuta sigara wanakabiliwa na magonjwa ya kuganda damu, kuharibu mapafu, pamoja na matatizo ya mishipa mwilini.  Magonjwa hayo yanayotokana na uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya ya mtu yeyote kwani husababisha hata kifo.

January 19, 2018

HAPO NI ENEO LA LWIKA KATIKA KIJIJI CHA LUNDO

Leo hii hakuna Mawasiliano ya Barabara toka Mbamba Bay to Kilosa....Bus zilizotoka   Mbinga na Songea Zimeishia shell pale Tambachi Kuna Calvart Limekwenda na maji watu wanahangaika hawajui cha kufanya.Hali ya mawasiliano kwa njia barabara ilikuwa mbaya sana siku ya tarehe 18/1/2017.

January 18, 2018

HAKUNA CHAMA KINACHOENDESHA MAISHA YA MPIGA KURA.

NA HONORIUS MPANGALA, BAHI
NILIPOKUWA mdogo niliamini maisha ni jambo ambalo liko tofauti na la kuogofya sana katika jamii. Sababu kubwa ni pale nilipokuwa nayasikia maneno kama “Usicheze na maisha”. Fikra zangu zilinipeleka kuwa maisha ni jitu linalotisha sana katika jamii.

Baada ya makuzi nikapata misemo kama “Maisha yenyewe ndiyo haya haya” nikaanza kutambua kumbe mwenendo wa kuanzia asubuhi unaamka hadi usiku unaingia kulala hizi harakati zote ufanyazo ndiyo maisha yenyewe.

Katika vipindi ambavyo wapiga kura na wananchi wa kawaida toka vyama vya siasa wanajiona kama na wao ni wenyechama basi ni katika kampeni za uchaguzi. Kipindi hiki kila mwanachama anajiita ni mwenyechama. Ni kipindi ambacho watu hao hudiriki kunukuu maneno ya wagombea wao na kuiaminisha hadhira aliyonayo kuwa chama chetu kitatekeleza mambo kadha wa kadha.

January 01, 2018

HERI YA MWAKA MPYA 2018! NGUVU YA HABARI


“Kama habari zozote ziwe nzuri au mbaya za sehemu yoyote hazisemwi au kutangazwa maana yake ni upenyo kwa wenye mamlaka “kutojali” kwasababu watasema, “nani atajua”. Kama habari mbaya zikisemwa maana yake inawazindua wenye mamlaka au watu wengine kufahamu kinachoendelea sehemu hiyo. 

"Kama habari nzuri zikisemwa maana yake zinavutia wengine kama fursa na mwelekeo mpya wa kijamii au kiuchumi. Tumia nyenzo yoyote kuhabarisha hata ikiwafikia marafiki zako watano tu inatosha sana kwasababu nguvu zake kubwa kuliko kubaki na fikra duni kuwa "nani anazitaka". 

"Kanda ya kusini ingali na nguvu ndogo sana katika habari. Mkondo wa habari Kanda ya kusini umekuwa duni kwasababu zifuatazo: wapashaji habari wachache wenye nguvu katika taasisi, wapashaji habari binafsi hawaoni umuhimu (sawa na kusema nina mambo yangu nyeti), miundombinu hafifu, kutojali au baadhi kukosa nyenzo. Lakini suluhisho lipo; hizi ni zama za Uandishi wa raia (Citizen Journalism), ambapo mitandao ya kijamii (Blog, Facebook, Instagram, Twitter, Tagged, Badoo, LinkedIn, Vk, Connect, YouTube, Vimeo, Skype, Tumblr,Flickr, WhatsApp, inachukua mkondo mkubwa wa habari kama ilivyokuwa Blogu miaka ya mwanzoni mwa 2000.

December 27, 2017

IJUE ASILI YA LIKUNGU AU NGUNGA (LAKE NYASA FLIES)

NA PROF. MARK MWANDOSYA, MATEMA BEACH, KYELA.
UKIKAA ufukweni Matema wakati Ziwa Nyasa likiwa limetulia, kwenye upeo, kwa mbali kabisa unaweza kuona umbile kama vile moshi unaobaki nyuma kama meli imepita. Mara ya kwanza nilibishana na wenyeji wangu nikiwaambia meli ya MV Songea ilikuwa ikipita kwa mbali kutoka bandari ndogo zilizo mwambao wa Ziwa. 

December 09, 2017

SOMO LA LEO: BENKI YA WANAWAKE NCHINI HOI

“Benki ya Wanawake haifanyi vizuri, nikiwaficha nitakuwa mnafiki, tangu kuanzishwa na mtaji kupewa na serikali ‘performance’ yake ni ‘very poor’ na wakopaji wengi ni wanaume. Nataka niwaeleze, wala si wanawake wanaokopa pale na ‘interest’ ni kubwa kweli kwa wanawake, sasa unakuwa na benki ya wanawake lakini inawaumiza wanawake. Kwahiyo tutaiangalia vizuri kwa ushindani wa kisasa, hili lazima kina Mama niwaeleze kwani msema kweli mpenzi wa Mungu na katika taratibu za sasa za benki  ambayo itashindwa kujiendesha inakwenda,”
 
-Rais John Magufuli, Dodoma, Desemba 8/2017

December 04, 2017

UJENZI BARABARA YA MBINGA-MBAMBA BAY WAKARIBIA

NA MWANDISHI WETU, SONGEA
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema ujenzi wa barabara ya lami nzito toka Mbinga wilayani Mbinga hadi mjini Mbambabay Wilayani Nyasa unatarajia kuanza hivi karibuni. 

BONYEZA HAPA KUTAZAMA VIDEO YA RC MDEME
Mndeme amesema hayo wakati akitoa taarifa ya kufungua kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Ruvuma, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea Novemba 29 mwaka huu, wiki iliyopita. 


December 01, 2017

NYASA: TUNAISHI KWA MIFANO, KUSEMA NA KUTENDA

Ilikuwa siku muhimu ya kukumbuka mambo niliyopita utotoni, kabla ya kugeukia elimu za darasani. Lakini pia hata nilipokuwa na elimu ya darasani bado nina mapenzi makubwa na mazingira haya yaliyonikuza.
Karibuni Nyasa.

Mhariri wa Blogu hii, Markus Mpangala akiwa katika Forodha ya Chivanga iliyopo kijiji cha Lundu. Picha hizi zinaonyesha mazingira halisi ya Nyasa yalivyo mazuri na utulivu wa Ziwa Nyasa. Siku hii ilikuwa ya kupalaza mtumbwi ili kukumbuka makuzi yangu miaka ya 1990. 
Tunaishi kwa mifano. Tunasema na kutenda kwani ndiyo msingi wa NISHANI MEDIA inayomiliki blogu hii pamoja na shughuli zingine. 
“KARIBUNI NYASA”.

MACHO VITABUNI


NAAM! Mara kadhaa ninapotembelea jiji la Dar es salaam wengi hutuita  wageni kama “watu wa mikoani”. Lakini ninachokiona wakati mwingine ni kuzikali fursa ikiwemo ya kutembelea maduka ya vitabu.

Wahenga wanasema ni heri ukatekwa nyara, kushikiliwa mateka kwa muda fulani katika duka la vitabu kwani unakuwa umehiari mwenyewe. Pia wanasisitiza kitabu ni silaha. 

November 30, 2017

SAFARI YAO YA MAISHA


Kuna dhiki na shida. Safari yao ina milima na mabonde. Sauti zao hazisikiki kokote. Hawajui itikadi zenu bali wanatafuta shibe zao. Mazingira yao hayavutii, lakini hawachokii kuyatumia kupata matumaini na kipato. LAKINI wanaishi kwenye nchi yenye utajiri pomoni. Hawana amana benki watakuwaje na amani?  Hawana chakula nyumbani watakuwaje na utulivu?
Tafakari makuzi ya mtoto huyu....
 Tafakari mwelekeo wake na hitimisho lake. Atarudishaje faida kwa jamii iliyomtenga kiasi hiki? Nani anajali hisia zake? Nani anajali hatima yake? Nani anagusa moyo wake?
Sauti zao zisikike!

©Picha kwa hisani ya Musa Makongoro. Imepigwa katika eneo la Mburahati, jijini Dar es salaam

November 20, 2017

KONGAMANO LA KUMBUKIZI YA FIDEL CASTRO


Jukwaa la Wajamaa Tanzania, Taasisi ya Usomaji na Maendeleo "Soma" na Rastafarai United Front wanashirikiana kuandaa kongamano la kumkumbuka El Commandante Fidel Castro siku ya Jumamosi, tarehe 25/11/2017. Mahala itakuwa kwenye ukumbi wa Soma Book Cafe; na muda ni saa 7 mchana hadi saa 12 jioni.
WOTE MNAKABISHWA. HAKUNA KIINGILIO!
"Mwambie Comrade amwambie Comrade"

November 15, 2017

NAMKUMBUSHA MBUNGE WA JIMBO LA NYASA

NA MARKUS MPANGALA
NIMEANDIKA safu hii leo baada ya kusoma Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano iliyosomwa na waziri Profesa Makame Mbarawa mjini Dodoma. Kwa mujibu Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma inaeleza kuwa Wilaya ya Nyasa iliyopo mkoni humo, ilianzishwa rasmi mnamo Machi  2012 baada ya kumegwa kutoka wilaya ya Mbinga.

Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mheshimiwa Stella Manyanya
Aidha, eneo la wilaya hii liko kando ya Ziwa Nyasa. Makao makuu ya wilaya yako mjini Mbamba Bay. Wakati wa sensa ya mwaka 2012, wilaya ya Nyasa ilikuwa na wakazi 146,16. Vilevile wilaya hiyo ina jumla ya Kata 16 ambazo ni Chiwanda, Kihagara, Kilosa, Kingerikiti, Liparamba, Lipingo, Lituhi, Liuli, Liwundi, Luhangarasi, Mbaha,    Mbamba Bay,Mtipwili, Ngumbo, Nindai,na Tingi.

Kwanini ninamkumbusha Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mama Stella Manyanya? Nitaeleza sababu za msingi kwa madhumuni ya kumsaidia vipaumbele katika jimbo lake. 

November 02, 2017

KAMPUNI YA MKUKI NA NYOTA WAINGIA SOKO LA VITABU CHINA


NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Mkuki na Nyota ambayo hujishughulisha na uchapaji wa vitabu imetanua wigo wa soko lake la uchapishaji na utangazaji wa vitabu baada ya kusaini makubaliano na Shirika la World Affairs Press (WAP) la nchini China.
 
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi wa MNN, Mkuki Bgoya amesema kuwa wamesaini Makubaliano na Shirika la World Affairs Press (WAP) ya China kufanya kazi pamoja katika miradi mbalimbali ya kuchapisha na kuvitangaza vitabu ikiwa ni njia mojawapo ya kutanua soko la kampuni hiyo barani Asia.

Mkuki na Nyota ni kampuni mashuhuri kwa uchapaji wa vitabu ambayo ilianzishwa mwaka 1992 jijini Dar es salaam. Mwanzilishi wa kampuni hiyo ni Walter Bgoya ambaye alitumia uzoefu wake wa miaka 18 ya kuwa Meneja Mkuu wa Tanzania Publishing House. 

October 16, 2017

CHUO CHAANZISHA SHAHADA YA WADUDU

NAIROBI, KENYA

KITUO cha Elimu na Utafiti kinachofadhiliwa na Benki ya Dunia kimeasisiwa katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jaramogo Oginga Odinga na kinasubiri ruhusa ya kuanzishwa kwa programu za Uzamifu na Uzamili kuhusu wadudu wanaoweza kuliwa.

Taasisi hiyo inapania kubuni njia za kuzalisha wadudu hao kwa wingi bila ya kuharibu mazingira ili kukidhi utashi mara baada ya wazo hilo likifanywa kuwa biashara.Wadudu wanaoliwa sana maeneo ya Magharibi mwa Kenya, ambao wana wingi wa madini ya protini na Zinki watafanywa kuwa biashara ili kuimarisha uwepo wa chakula cha kutosha, na kuondoa dhana mbaya katika kula wadudu.