Showing posts with label Mbunge. Show all posts
Showing posts with label Mbunge. Show all posts

June 16, 2013

JK MGENI RASMI MECHI YA WAKUU WA WILAYA NA WABUNGE


 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mechi ya hisani itakayowakutanisha waheshimiwa wabunge na Wakuu wa wilaya, itakayopigwa Juni 29, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo itatanguliwa na ile ya Juni 22 mjini Dodoma, ambapo huko mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambapo lengo la mechi hizo ni kuchangisha fedha za ujenzi wa shule ya albino, huku kukipangwa kuwa na burudani za kila aina, sambamba na wasanii watakaoamua kuungana na serikali juu ya uchangiaji huo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa timu hiyo ya wakuu wa wilaya, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alisema kuwa huku mheshimiwa rais akiwa mgeni rasmi, ila wamejipanga imara kwa ajili ya kuwaonyesha kazi wabunge, ambao baadhi yao wameanza kujigamba dhidi ya mechi hiyo ya aina yake.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu
Alisema kuwa Watanzania wote watakaopata fursa ya kuhudhuria kwenye mechi hizo wataaburudika kwa kiasi kikubwa, huku wakiamini kuwa licha ya wakuu wa wilaya wengi kuwa mikoani, ila wana nguvu na ari ya kushinda mbele ya wabunge.

“Tupo imara na tutaanza mazoezi yetu kesho Jumatatu kwa kukutanisha wakuu wa wilaya wote waliokuwa kwenye timu hii, huku barua za kuwaombea mialiko kutoka kwa Wakuu wa Mikoa tayari zimeshafika kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili.

“Katika mechi hizi, mwamuzi wa kati atakuwa atakuwa Reginald Mengi, ambaye ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, huku waamuzi wa pembeni wakiwa ni IGP Said Mwema na Stephen Wassira, ambapo wote watashiriki katika mchezo huu,” alisema.

Aliwataja Wakuu wa wilaya waliotwa kwenye uundwaji wa kikosi hicho kuwa ni pamoja na Venas Mwamoto (Kibondo), Ramadhan Maneno (Kigoma), Norman Sigara (Mbeya), Krispin Meela (Rungwe), Benson Mpesya (Kahama), Deodatus Kinanilo (Chunya), Herman Kapufyi (Same), Francis Isaac ( Chemba), Wilson Mkambaku (Kishapu), Yahya Nawanda (Iramba), Elibariki Kingu (Igunga), Festo Kiswaga (Nanyumbu), Paza Mwamlima (Mpanda), Abdallah Ulega (Kilwa), Seleman Mzee (Kwimba), John Mongela (Arusha), Konstantin Kanyasu (Ngara), Paulo Mzindakaya (Busega), Mrisho Gambo (Korogwe), uhingo rweyemamu handeni, Cristofa Magala( Newala), Erasto Sima (Bariadi), Jordan Rugimbana (Kinondoni), Joseph Mkirikiti (Songea), Ngemela Rubinga (Mpanda) nay eye mwenyewe anayotokea wwilaya ya Handeni, ambaye pia ni msemaji wa timu hiyo.

Aidha, Muhingo alitaja kikosi cha wanawake kuwa kinaongozwa na Beth Mkwasa (Bahi), Sarah Dumba (Njombe), Josephine Mapiro (Makete), Hafsa Mtasiwa (Pangani), Mboni Mgaza (Mkinga), Halima Dendegu (Tanga), Queen Mlozi (Singida), Angelina Mabula (Butiama), Merry Tesha (Ukerewe), Christina Mndeme (Hanang), Anna Magoha (Urambo) Jacqueline Liana ( Magu).
mwisho

December 29, 2012

AZIMIO LA ZANZIBAR LILISAHAU B.E.E


Na Markus Mpangala 



Azimio la Zanzibar linafahamika kuwa nyenzo iliyotumika kuua lile la Arusha.
Ingawaje viongozi wetu hawasemi walichokubaliana kule Zanzibar, lakini hali haijifichi na inaonekana tunazidi kusonga mbele.
Kuna mtikisiko wa kijamii unaendelea kwa sasa, kutoka kwenye mitazamo na maisha ya ujamaa hadi kwenye kiwango cha chini cha ubepari. Bahati nzuri ni kwamba ujamaa upo mioyoni mwetu yaani ndio maisha ya watanzania.
Ni kwa sababu hii ndiyo maana Mwalimu Nyerere aliuita ujamaa wa kiafrika. Sasa basi, katika azimio la Zanzibar viongozi wetu bila shaka walikusudia kufanya mabadiliko katika uchumi. Bahati mbaya mabadiliko hayo yalikuwa yanafanyika kwa kudanganywa na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Dunia.
Walichodanganywa viongozi wetu ni sera za asasi hizo kuwa mwongozo wa uchumi wetu. Halafu hali ikiwa mbaya wanachofanya ni kulaumu kuwa nchi imeshindwa. Sera za IMF na WB hazijali mazingira ya mwanadamu wa kitanzania.
Maeneo mengi imetokea hali hiyo na hivyo kuongeza kiwango cha ufukara kwa wananchi katika nchi husika. Ufukara huo unachochewa zaidi na jinsi sera inavyopuuza hali halisi ya mazingira ya nchi na utamaduni wa watu.
Sera za IMF na WB zinatokana na uzoefu wa nchi za Ulaya na Amerika. Kule wataimba nyimbo kuwa ruzuku ni muhimu kwa mkulima na wanakwenda nchi zetu za Afrika na kusema kama, ‘utampatia ruzuku mkulima basi unampunguzia uwezo wa kuwa mbunifu.’
Lakini hatujiulizi kwanini wakulima wa Ulaya wanapewa ruzuku na kadhalika. Sera za IMF na WB ndizo zilisababisha azimio la Zanzibar kuonekana kituko mbele wa wajuzi wa mambo.
Azimio hilo lililo katika kibarua cha Azimio la Arusha halikuja na mbinu mbadala ya kuweka msingi wa kukuza uchumi. Badala yake likaja na mageuzi ya uchumi katika mkondo wa sera za IMF na WB.
Kimsingi hilo lilikuwa kosa na dosari kiuchumi. Serikali yetu haikumwandaa au haikuhodhi moja kwa moja uchumi. Bali ikadanganywa na IMF na WB kuwa jambo muhimu ni kufungua milango ya mageuzi ya uchumi.
Milango iliyofunguliwa sio ile ambayo ilifunguliwa na chama cha siasa cha ANC cha Afrika Kusini. Chama cha ANC kilifungua milango ya mageuzi ya uchumi kwa sera yake, misingi yake na baadaye kikawa kinapokea ushauri tu.
Sera kubwa ambayo iliing’arisha ANC ni B.E.E. ( Balack Economic Empowerment). ANC ilikuwa wazi kabisa, hata kama sera hiyo iliwalenga watu weusi wa Afrika Kusini, na kuwatenga wazungu ambao ni raia halali wa nchi hiyo, lakini kilichofanyika ni kuziba pamba masikioni.
ANC ikasema inatambua kuwa B.E.E inaonekana kama inabagua lakini ni wajibu wao kutimiza uwezeshaji wa watu weusi katika mitaji ya kiuchumi. Mazao ya ANC ndio Tokyo Saxwalle, au familia ya kina Khoza.
Mfanyabiashara Tokyo Saxwalle anafahamika kuwa miongoni mwa matajiri wakubwa na wawekezaji wa kiwango cha juu kutoka jamii za waafrika. Ni kutokana na sera hiyo iliwezesha kuibua wafanyabishara, wawekezaji na wajasiriamali wengine ambao walifanya kila jitihada kwa kutumia sera ya B.E.E kufanikiwa.
ANC ikasema lazima watu weusi wawezeshwe. Tafsiri sahihi hapa ni kuwawezesha wazawa. Hali hiyo ilitokana na miaka mingi ya utawala wa kaburu kuwanyonya na kuwakandamiza watu weusi. ANC ilipania, ikathubutu, ikatimiza dhamira yake.
Ni sababu hiyo tunaona baadhi  wawekezaji wakubwa waafrika kutoka Afrika Kusini, vinginevyo ubaguzi ulioanzishwa na makaburu ungeendelea kuwafanya waafrika wabaki hohehahe.
Mfano wa pili ni Chujusong, Korea Kaskazini. Tangu mwaka 1925 Korea Kaskazini chini ya chama cha kikomunisti ilifanya jitihada kubwa ya kujenga uchumi huku ikitanganza kuwa ni Jamhuri ya Kisoshalisti.
Chujusong ni mpango wa kujitegemea kiuchumi. Msingi mkuu ulikuwa kuhakikisha mitaji ya kiuchumi inakuwa huru ili kuondokana na utegemezi kutoka nje. Sera hiyo ilichukua ngumu na kuhodhi mwenendo wa nchi hiyo kujenga uchumi wake.
Polepole mabadiliko makubwa yakajitokeza hadi Korea Kaskazini tunayoiona leo. Hapa kwetu sera ya wazawa tu ilitushinda, na kwakuwa tulikuwa tumekosa uelewa wa kutosha tukadhani sera hiyo inabagua.
Laiti tungelikuwa na msimamo na uelewa wa kutosha kuwa huo siyo ubaguzi sababu hata wageni walioingia nchini mwetu waliwabagua wenyeji. Kwahiyo ili kukabaliana na pengo lililokuwepo zama za ukoloni, ilipaswa serikali ya awamu ya pili ilipofungua milango kuruhusu mageuzi ya kichumi, itunge sera za B.E.E.
Mpango wa kuwawezesha waafrika sio dhambi. Mpango wa kuwawezesha wazawa sio dhambi. Wazawa hao maana yake tuwe na wawekezaji sampuli ya Reginald Mengi.
Watu wa aina yake tuwe nao wengi ili kuimarisha mitaji ya serikali na uchumi wetu. Tusipokuwa na misingi inayoakisi ustawi wa taifa kiuchumi, itawezesha fedha nyingi za Tanzania kuishia mikononi mwa wadokozi. 
Na wadokozi wengine tulipowajua wakati wa miaka ya 1990 ntumejikuta sasa nchi inabomolewa benki yake. Sasa baada ya kuipoteza misingi hii tumejikuta tunahamasisha ujasiriamali.
Tunahangaika na ujasiriamali sababu wakati wa kufungua milango ya mageuzi ya uchumi hatukujua mageuzi hayo yanafanyikaje na uchumi utakuwaje.
Milango iliyofunguliwa ikawa ni kuruhusu wachuuzi ambao walidhaniwa wawekezaji, wakawa wanachuma mali za watanzania. Sasa, akili inapoibuka kipindi hiki tunajikuta kumbe wakati tunazika azimio la Arusha tulipaswa kutamka kwakuwa lazima tuwezeshe wazawa. Lazima watu weusi wawezeshwe kwenye mitaji. Na iwe sera sio huruma. Kwa sasa tumejikuta tunao wawekezaji wengi kutoka nje, halafu wawekezaji wa ndani bado uwezo wao  sio mkubwa sababu hawakuwa sehemu ya mageuzi ya uchumi yaliyofunguliwa wakati ule.
 Nionavyo, tunatakiwa kuwa na sera za kuondokana na uchuuzi wa kijasiriamali. Lazima tujenge uwezo kwa wazawa. Lazima tuwaige ANC kwa sera ya Black Economic Empowerment. Tujiulize, hivi kuna ofisi ngapi za Benki ya Dunia na IMF katika nchi za Kiarabu? Jibu hakuna ofisi hizo kwakuwa hazihitajiki. Tafakari. Nahitaji changamoto. 

December 20, 2012

MAKAA YA NGAKA KUIMARISHA UZALISHAJI VIWANDANI


Mitaa ya mbinga mjini.
picha kwa hisani ya Prof Joseph Mbele

Uzalishaji wa makaa ya mawe unatarajiwa kuongezeka baada ya mradi wa uchambiaji wa makaa ya mawe mjini NGAKA wilayani MBINGA katika mkoa wa Ruvuma kufanza kufanyiwa kazi na kampuni ya uchimbaji makaa hayo wilanai humo.
KWA TAARIFA ZAIDI BONYEZA HAPA KUSOMA HABARI NZIMA

November 09, 2012

WADAU WA MAENDELEO YA WILAYA YA NYASA WAJADILI MUSTAKABALI WA WILAYA YAO

 MICHAEL NCHIMBI akandika kwenye mtandao wa Facebook kuhusu Wilaya ya Nyasa. Kupitia mtandao wa NYASA akasema kuwa; .... "Jamani hivi Nyasa hakuna matatizo yoyote yale ya kijamii? Sababu ndugu Komba(John) mbunge wa jimbo la Nyasa hajawahi kusimama Bungeni tangu lianze tarehe 30 kueleza matatizo ya wananchi wa Nyasa"! 
 
 Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba akifungua Zahanati ya Tumbi, wa kwanza kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Mbinga Anastia Amasy 

 WADAU WAKACHANGIA YAFUATAYO;

1. JOSEPH NDOMONDO ... akasema, "Huyo mtu vijana wenye mtazamo tulimkataa, But(lakini) CCM, pesa ya wananchi na akina mama wakinyasa ndiyo waliyompa nafasi tena. Kwahiyo hata hajasimama bungeni hiyo imekula kwetu. Kwahiyo guys(vijana) tuwaelimishe wamama(wanawake) wapendwa wa Nyasa ili Nyasa iwe mfano 2015 tumbwage. But i'm not interested with political now. Pamoko kwa sana ila mje Nyasa siyo kwenye Facebook tuuu@Joe.

2. JAMES ZOTTO, akasema haya ........ " Kwani ni lazima aongee kila Bunge?"

3. MAURICE NCHIMBI ... akachangia pia, " Acha siasa bwana Zotto kwani Bunge lililopita aliongea nini..."

4. JAMES ZOTTO, 
 Akarejea tena kuchangia  ..."Aliongea mpaka wetu na Malawi na Huduma za Jamii lakini wanaomlaumu John Komba ni wanafiki sana maana wao ndio wa kwanza kumpigia debe na kumchagua. Kwani alichaguliwa na nani? Je, nani alijitolea kutoa elimu kwa wapiga kura na kuwafahamisha wanyasa kuwa tunataka mabadiliko? Si Komba tu, ni mfumo mzima umedorora! Labda hapa nitaeleweka, nitagombea 2015, Mtanisapoti?

5. MARKUS MPANGALA, ..... 
 Nami nikajongea na kusema haya ..."Kaka James Zotto, kabla hujagombea una kazi kubwa ya kufanya naomba hilo wazo sogeza hadi 2020. Nadhani sasa tushughulikie hili unalofanyia kazi sasa na mengineyo. Suala la John Komba kutoongea jamani inabidi tujiulize nani KERO ipi inatakiwa kuzungumziwa na hatua gani zilichukuliwa ama zinafanyiwa nini. Binafsi kuna juhudi zinanifurahisha sana ndio maana nazijaza kwenye blog hata kama ni kidogo lakini zinaleta matumaini. Mimi natamani ELIMU na AFYA ziwe kipaumbele. Je, mbunge wetu anaweza kufanya kila kitu kuhusu Nyasa? Na kila jambo linategemea Bunge? Kama tulivyo na desturi yetu ya kujitolea kwa maendeleo yetu Wanyasa, naomba tudumishe hilo. Kaka Hoops Kamanga ananipa mengi na kuelewa Nyasa inaelekea wapi. Nina miaka mitano mbele naamini Nyasa itakuwa na fursa nyingi mno na habari za Dar es salaam syndrome zitaanza kutoweka angalau kidogo. 

6. HOOPS KAMANGA, 

Naye akachangia haya, ..............." Markus lazima tukubali kuwa vijana na wasomi wa leo tuna tatizo la kulalamika pengine bila hata kujifikirisha nn kiini cha ttz kumlaumu komba kuwa haongei bungeni ni kutojua kinachoendelea nyasa jamaa ana influnce kubwa sana kwenye hii serikali nyasa hv leo kuna miradi mikubwa ya maendeleo ambayo hatukuwahi kuiona kwa serikali hii ya ccm sion mwakilishi atakaeisaidia nyasa zaidi ya huyu kuna haja gani kuongea bungeni wakat ukipeleka kimemo kwa waziri unatekelezewa hv mnajua nani ali push ishu ya wilaya mpya na mwez ujao halmashauri inaanza.....kwa nafasi zetu tuanze ss kurudisha fadhila nyasa napendekeza tuanzishe online harambee tukusanye fedha kila baada ya miezi 3 au 6 tuanze kuwanunulia wadogo zetu vitabu nawasilisha.