MWANDISHI: SAID AHMED MOHAMED
MCHAMBUZI: KIZITO MPANGALA
AMEZIDI ni tamthiliya iliyopgwa
chapa na East African Educational Publishers (Nairobi, Kampala, na Dar es
Salaam) ambapo chapa ya kwanza ilitolewa mwaka 1995. Kitabu
hiki kimesajiliwa kwa namba za usajili ISBN 9966-46-752-1.
Tamthiliya hii imegawanyika
katika maonyesho kumi ya jukwaani ambapo kila onyesho lina ujumbe ambao
unailenga jamii ya Afrika kwa ujumla hasa katika suala la maendeleo ya
liuchumi, kielimu kijamii na kadhalika. Wahusika wakuu wa tamthiliya hii ni Ame
na Zidi. Maonyesho haya yote na tamthilya yenyewe kwa ujumla ni cmhezo wa
mawazoni tu!
Ame na Zidi wanajikuta katika
umasikini mkubwa katika bahari iliyojaa mali. Katika hali hii ya uhitaji
wanatambua kuwa hawana lingine la kufanya ila kuomba misaada ili wayatosheleze
mahitaji yao. Msaada unapokuja unaleta madhara mengi zaidi.
Onyesho la kwanza linaonyesha
Zidi akiwa anamwamsha nduguye Ame aliyekuwa amelala kukiwa kumeshakuchwa. Zidi
anamwonyesha Ame mihogo miwili aliyotoka kuitafuta ili wapate kuila.
Onyesho la pili linaonyesha Ame
na Zidi wakiwa katika kasri lao wanalisifia kasri hilo lililojaa samani nyingi
kutoka Paris (Ufaransa) na vito mbalimbali pamoja na mazuria kutoka Iran.
Onyesho la tatu linaonyesha
Zidi akiwa na mpenzi wake Mariam ambaye alizoeleka kuitwa Mari. Wapo katika
kasri la akina Zidi huku mari akiwa amejiremba na kujiita msichana wa kileo! Zidi
na Mari wanazungumza kuhusu umasikini ambao unawatafuna Zidi na Ame huku mawazoni
mwao wakijinadi kwamba wana mali nyingi zenye thamani lakini si kweli.
Onyesho la nne linaonyesha Zidi akiwa mwalimu na
wanafunzi darasani katika kipindi cha somo la sayansi. Wanafunzi wanamuuliza
mwalimu maswali ili wapate kujua lakini mwalimu naye hajui kitu ila anajilinda
haiba yake kwa bakora!
Onyesho la tano, Ame mkuu wa
ofisi fulani akiwa na msaidizi wake Zidi wakiwa ofisini wakijadiliana mambo
mbalimbali na jambo kuu ni kughushi nyaraka ili kujipatia fedha kinyume na
utaratibu wa kasri lao. Onesho la sita ni mwndelezo wa omyesho la tano.
Onyesho la saba Mari amerejea
kutoka mbali kumtembelea mpenzi wake aliyemuacha siku nyingi. Zidi na Mari
wanashangaana na kisha kila mmoja anamuona mwenzake amebadilika lakini Mari
anamwambia Zidi kuwa hajabadilika kimawazo kwa kuwa bado yu masikini. Mari amekuwa
na mwonekano wa kizungu na ngozi amejichubua.
Onyesho la nane, Ame na Zidi
wanajadiliana masuala mbalimbali kuhusu kasri lao iliwaondokane na utegemezi wa
misaada kutoka mbalia. Kubwa hasa wanajadiliana kutokomeza ugonjwa wa maleria.
Onesho la tisa, Zidi anaugua
tumbo baada ya kula nyama ya ngombe iliyoletwa kwa msaada kutoka Jumuiya ya Umoja
wa nchi za Ulaya (EC). Nyama hiyo ilikuwa imevunda lakini waliiparamia tu na
kuila kutokana na njaa. Baadae Zidi anakufa.
Onyesho la kumi, Ame naye
anaugua tumbo baada ya kuharisha kwa muda mrefu, hivyo kipindupindu kimemshika
na yeye pia anakufa. Usingizi unamkosesha Ame morali
ya kufanya kazi kwa bidii hivyo anabaki kitandani akiwa mvivu kuamka. Usingizi aliouzungumza
mwandishi hapa huenda si ule wa kuliparamia godoro tu bali ni kuwa katika hali
isiyo na mabadiliko katika kitu licha ya kubadilika kwa nyakati. Mwandishi ananuia
kusema kuwa usingizi wa mawazo ni mzito ziadi kuliko usingizi wa kuparamia
godoro. Tuamke katika fikra ili kujiendeleza.
Suala la elimu ni suala ambalo
linajadiliwa kwa kiasi kikubwa katika nchi nyingi barani Afrika. Mwandishi aeonyesha
kwamba upo uwezekano mkubwa wa baadhi ya walimu kufundisha mabo wasiyokuwa na
ujuzi nayo, hivyo ni vema kila mwalimu angeshika somo moja tu kwa siku na
afundishe madarasa mawili tu. Somo hilo awe analimudu vizuri. Pia maarifa
wanayofundishwa wanafunzi yalenge jamii kwa ujumla, si vema mhitimu wa uhandisi
wa umeme ashindwe hata kurekebisha pasi ikiwa na hitilafu. Mhandisi wa majengo
kwenye makaratasi atafundishwa ubora wa kuchanganya zege lakini akiletewa theruji,
lipu, mchanga, kokoto na maji anshindwa kufanya vipimo. Elimu yetu ina hitaji
mabdiliko. Udadisi wa wanafunzi nao uheshimiwe!
Tunahitaji kuthamini bidhaa za
ndani. Tuna samani nyingi zimejaa maeneo mbalimbali zinasota kwa siku nyingi
tu. Tunaona vema kununua meza na viti vya vioo kutoka Uchina, Paris, Italia ili
kuviweka ndani mwetu lakini samani bora za mbao zinazodumu kwa muda mrefu
twaziona ni bure ka bisa. Mwandishi ananuia kusema kuwa tunapaswa kutahamini
vitu vyetu kama vile tunavyothamini vya ughaibuni.
Ulimbwende siyo lazima kukoboa
ngozi. Kwa wanawake, wanaweza kuwa warembo wazuri bila kukoboa ngozi zao na
kuwa na rangi ya bandia inayoleta matatizo mwilini. Mari ni mrembo bandia
aliyekoboa ngozi na kunyoa upala kisha kuvaa mawigi ya katani au ya nywele za
watu waliokufa na pia amenyoa kope zote na kubandika kope za plastiki
zilizotengenezwa Kanada. Tabia hii mwandishi ameisema kwa muda muafaka, na
wengi wanaofanya hivyo hupata matatizo mbalimbali katika miili yao.
Wanafunzi huko vyuoni wasome
kwa ujuzi wa mambo lakini si tu kupata GPA yenye alama za juu. Ikiwa ujuzi wa
mambo hautazingatiwa basi hata fundi wa kuziba pancha ataitwa kutoka Ujerumani.
Tunafurahi nini kutoa tenda kwa kandarasi nyingi za nje? Kama tunazo za kwetu
kwa nini hatuziimarishi kwa kuziamini na kuzipatia tenda hizo? Barabara nyingi
katika nchi za Afrika zimejengwa na kandarasi za ughaibuni. Basi kwa msaada wa
tamthiliya hii ya AMEZIDI tusizidi tu kutegemea mbali na nyumbani kwetu.
Hakuna haja ya kughushi nyaraka
ili kujipatia mali kinyemela. Tukijivika kanzu la kufanya mambo ipasavyo na kwa
kanuni maalumu basi kanuni ile itaiishi na itatusaidia tukiisimamia ipasavyo. Hivi
zisingekuwepo Marekani, Kanada, Ujerumani, Italia, Ujapani, Ubelgiji, Ufaransa,
na kadhalika tungenyosha wapi mikono yetu zaidi? Tunekubali kwenda Haiti au
Tahiti kuomba?
Afrika tuna changamoto nyingi,
kuzitatua kunahitaji umakini wa kufikiri. Semina, mikutano, makongamano,
maandamano, na mabango ni mitazamo tu kuhusu utatuzi lakini “mtazamo hauliwi hata tukitumbuliana macho
namna gani”. Tuimarishe sera, na elimu tuijali kwa kina.
© Kizito Mpangala (0692 555
874)
Nimependa mtiririko wa mawazo Haya.. Shukrani Kwako bwana Mpangala
ReplyDeleteKazi nzuri shukran
ReplyDeleteKazi nzuri mno imenisaidia kuielewa tamthilia Amezidi
ReplyDeleteKazi nzuri mno imenisaidia kuielewa tamthilia Amezidi
ReplyDeleteKazi nzuri sana bwana mpangala
ReplyDeleteKazi nzuri sana
ReplyDeleteKazi ya Safi saana, kwa ufupi umasikini Ni mbaya
ReplyDeleteKazi nzuri sana shukran
ReplyDeleteExcellent thanks đź‘Ťđź‘Ťđź‘Ťđź‘Ťđź‘Ť☺️
ReplyDeleteHeko Bw. Mpangala
ReplyDeleteDaaah bila ya kupitia hilo dodoso ,kwa kweli kitabuni nilikua naona kimendikwa kichina tuu baaada ya kiswahili
ReplyDeleteumejitahidi san kuchambua kitabu hiki hongera
ReplyDeleteShukraniii sanaa
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteKazi nzuri mno
DeleteShwari kabisa,,kazi njema
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteKazi nzuri nimevutiwa nayo
ReplyDeleteShukrani Bw. Mpangala
ReplyDeleteShukrani Bw Mpangala
ReplyDeleteHongera Bwana Mpangala kwa kazi nzuri uliyofanya
ReplyDeleteHongera kazi safi
ReplyDelete