Showing posts with label maoni. Show all posts
Showing posts with label maoni. Show all posts

March 21, 2018

JE, JAMII IMECHOKA KUISHI KWA MAFUNDISHO YANAYOTOLEWA KWA MIFANO?

Na KIZITO MPANGALA

Mafundisho ni moja kati ya elimu ambayo haina mpinzani katika maisha yetu ya kila siku. Mafundisho hayo yapo kwa namna mbalimbali, kuna mafundisho ya jumla, kuna mfundisho ya kipekee ambayo hugusia katika uga husika kama vile mafundisho ya dini, mafundisho ya stadi za kazi, mafundisho ya maadili, mafundisho ya rika na kadhalika. Hayo yote husaidia kujenga jamii na kuiweka katika mwenendo unaokunalika na wengi na ambao una manufaa mazuri kawa jamii hiyo na pengine hata kuakisi kwa jamii nyingine mahali popote duniani.
Mafundisho ya kijinsia yana umuhimu mkubwa sana katika maisha yetu. Jinsia fulani ifundwe yale yanayopaswa kufanyika nayo ili kuendeleza maadili au jeme lipatikanalo kutoka katika mafundisho hayo. Ikiwa mtu wa jinsia tofauti ataifunda jinsia nyingine fundisho fulani, kinachotakiwa ni kufikiri kilichosemwa ili kubaini kama kina manufaa ya kurekebisha kitu fulani kwa jinsia iliyofundwa au kama kina maudhui mabaya dhidi ya jinsia iliyofundwa kishapo hukumu itolewe, iwe hukumu chanya au hukumu hasi.
Kitendo cha kutoa mafundisho kinaweza kuwa cha namna mbili. Huenda mafundisho yakatolewa kinagaubaga au kwa kutumia mifano ambayo inalenga kurekebisha jambo fulani katika jamii. Ikiwa hilo linafanyika, si vema kulalamika ghafla bila kufikiri lengo au dhamira ya mafundisho hayo. Na kwa sasa jinsi ilivyo rahisi kusambaza taarifa katika mitandao basi ndani ya dakika kadhaa dunia yote huenda ikajua kinachojiri na kisha kila aliyepata taarifa anatoa maelezo yake kadiri ya taarifa ilivyomfikia. Watasifu, watalaani, watahamasisha watu kuwa watulivu, watamshutumu mnenaji, watamtetea mnenaji na kadhalika.
Katika suala hili la kuishi katika mafundisho yanayotolewa kwa mifano, inawezekana mfundaji anakuwa na nia ya kuonya au kurekebisha jambo fulani lakini huenda akaeleweka tofauti na lengo la fundisho lake. Hii inatokea mara nyingi na pengine husababisha maandamano ambayo yanaweza kuzua madhara kwa waandamanaji wakiwa wanakemea fundisho wasilolikubali au kama limefikirirwa kuwa ni la kejeli kawa kundi fulani katika jamii.

February 22, 2018

UTUKUFU.

Na Kizito Mpangala
Utukufu nikupe au nisikupe? Twasema utukufu kwake yeye aliye juu japo sijui yupo juu ya mti, juu ya paa, au juu ya kichwa cha mtu mwingine au juu ya mnazi, au pengine juu ya mbuyu basi kotekote utukufu uende tu kwa sababu ni juu. KumBe nami nikiwa juu nitapata utukufu, sawa! Lakini utukufu gani nitakaopewa unifanye niwe mtukutu badala ya mtukufu? Unaona sasa, kumbe nikiwa mtukufu sipaswi kuwa mtukutu lakini nikiwa mtukutu sipaswi kuwa mtukufu kwa kuwa watoaji wa utukufu wanapungua, nasema tu wanapungua ingawa siwajui wanaotaka kunipa utukufu kama nisipokuwa mtukutu.
Lakini mimi tu, kweli? Mimi nikipewa nitawapa na wengine utukufu huo ili tuone kama ni watukutu au ni watukufu katika utukufu huo uliotolewa na wenye utukufu wanaoonwa ya kwamba ni watukutu katika akili  na utashi lakini wanao utukufu ambao huwapa wengine na wengine hao wakipewa utukufu huo wanakuwa watukutu kwa kuwa wamepewa utukufu basi pengine ni watukufu kweli kadiri ya wagawaji wa utukufu wanaotazamwa kama watukutu. Jamani mimi nausema utukufu uliotolewa na wenye haki ya kukaa nao na wakawapa wa kuutumia ili wawarudishie mambo matukufu.

November 08, 2017

SASA NAMWELEWA HILARY CLINTON

NA  MARKUS MPANGALA
 
WAKATI wa kampeni za Uchaguzi nchini Marekani mwaka 2016, aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Democrat, Hilary Clinton alisema: “Kama mgombea (wanasiasa) anakasirishwa na sentensi moja iliyoandikwa kwenye mtandao wa kijamii basi huyo hafai kupewa mkoba wa nyuklia, maana vidole vyake vitabonyeza wakati wowote,”. 
 
Tafsiri ya Kiswahili ni yangu kwa sababu ninahitaji kurahisisha kueleweka hoja yenyewe. Maneno ya Hilary Clinton yalimlenga mgombea wa chama cha Republican, Donald Trump ambaye alishinda uchaguzi huo baadaye.

Clinton aliamini kuwa kitendo cha Trump kukasirishwa na sentensi zinazoandikwa kwenye mitandao ya kijamii ikiwamo yeye mwenyewe kujibu mapigo au kuwatisha watu, ilikuwa ni ishara ya mtu ambaye hawezi kustahimili ukosoaji au kukosolewa pale anapokuwa kiongozi.

Kwamba ili uwe kiongozi unatakiwa kustahimili au kama wasemavyo wahenga lazima uwe na ngozi ngumu hata kama utapigwa mishale ya kila namna. Hii ndiyo changamoto inayotukabili vijana, viongozi wa kila ngazi na watendaji mbalimbali kwenye vyombo vya uamuzi kwa maslahi ya Watanzania. 

Mara nyingi tumesikia wanasiasa au wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wakijiapiza kufanya jambo hili au lile. Wengine wanatajwa kuudhika kutokana na maneno kadhaa yanayozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii.

Tunafahamu kuwa ipo sheria ya mtandao na maudhui, ambapo inalenga kudhibiti nidhamu pamoja na kukabiliana na “hatari” yoyote inayoitwa kama udhalilishaji (Cyber Bullying), matusi na hulka mbaya dhidi ya viongozi au watu wa kada mbalimbali. 

Lakini katika kipindi hiki kuna jambo limenishangaza. Nashangaa kuona wanasiasa wetu nchini wanakasirishwa na ‘status’ zinazondikwa huko Facebook, Twitter, Instagram na kwingineko. 

UCHAMBUZI WA TAMTHILIYA YA BLACK MAMBA

KITABU: BLACK MAMBA
MWANDISHI: JOHN RUGANDA
MCHAMBUZI: KIZITO MPANGALA.

Black Mamba ni tamthiliya iliyoandikwa na John Ruganda kutoka nchini Uganda. Namba za usajili ni 978-9966-46-378-X na kuchapiswa na East African Educational Publishers. Kina jumla ya kurasa 70 tu. Wahusika wa tamthilya hii ni Profesa Coarx (kitivo cha sosholojia), Berewa mfanyakazi wa Profesa Coarx, Namudd mke wa Berewa, Odiambo mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya Sosholojia, Catherine Smith mkufunzi mpya kitivo cha Sosholojia, Ofisa wa Polisi na msaidizi wake. Na mhisika msaidizi ni Namatta ambaye ni kahaba.