Showing posts with label vicheko. Show all posts
Showing posts with label vicheko. Show all posts

October 21, 2017

TABASAMU NA KITABU


Ragin Mmbanga (kushoto) na Markus Mpangala (Kulia)
Huyu ni rafiki yangu. Anaitwa Ragin Mbaga, ila tuwapo farashani hupendelea kumwita "Mzee wa bustani ya usomaji". 

October 17, 2012

HARAKATI ZA MAENDELEO WILAYA YA NYASA, KARIBU KUWEKEZA


Wilaya ya Nyasa ni miongoni mwa Wilaya mpya zilizoanzishwa na serikali ya awamu ya nne. Habari za kuundwa wilaya ya Nyasa nilianza kuzisikia mwaka 1993 nikiwa shule ya msingi. Lakini mwaka huu Wilaya ya Nyasa imezinduliwa rasmi na shughuli za maendeleo zinaendelea ili kukidhi mahitaji ya wananchi. Katika harakati hizo ni pamoja na huduma ya Maji ambayo ni muhimu sana kwa wananchi wa Wilaya hiyo. Hapa ni picha mbalimbali ambazo zinaonyesha suala la upatikanaji wa maji katika vijiji mbalimbali wilayani humu.  Bila shaka wageni na wenyeji watavutiwa kuwekeza katika wilaya mpya ambayo fursa mbalimbali zinajitokeza. karibuni. Picha zote na Hoops Kamanga
 Chanzo cha Mradi wa maji kikifanyiwa ukaguzi.
 Tenki la Maji katika mradi wa maji katika kijiji cha Ng'ombo wilaya ya Nyasa
 Mradi wa Maji katika kijiji cha Kindimba Juu ambao umekamilika na wananchi wanategemea kutumia siku chache zijazo. Hapo fundi anamalizia marekebisho katika tenki.

November 13, 2008

kipindupindu kiingie ikulu


sikujua uchungu, sononeko la moyo
akili yagota kwangu, moyoni harijojo
ghadhabu yanisibu,adhuhuri si kikomo
dibaji ya nini,uchafu mitaani?

kila leo twaumwa,vichomi na kuhara
miili yatuuma,akili nayo yagoma
maji haba salama, twanywa ya visima
dibaji ya nini uchafu mitaani?

kipindupindu chapindua,kinyesi kuwa maji
mwili kukongoroka,acheni dhihaka jamani
kila leo twanya uharo, ikulu vipi?
dibaji ya nini,uchafu mitaani

kipindupindu ikulu,napenda kitinge
waharishe wakuu,nasi tupumzike
aghalabu isiwe vigumu, wanye uharo preeee
wakome na kuona mashudu,wanune au wacheke?
dibaji ya nini,uchafu mitaani

ngoja kipindupindu kiingie ikulu
ooooh alamsiki waungwana wema

April 30, 2008

Bado Hasira hazijaisha kwani nakumbuka sna Nyasas

Unajua kipi kinachonikasirisha hapa?aa samahani siyo hapa kwenye blogu yangu bali huku ninakoongeza kaelimua Mlimani chuo kikuu cha Dar es salaam.LKulikuwa na mgomo na vurugu za hapa na pale watu wanalilia haki halafu watawala wahuni na wasiojali utu wa wanafunzi wanakandamiza uhuru wa kufikiri.Ngoja nikomee hapa kwani ukisoma mengi utasema nimehama nyasa yangu na kuandika yasiyonihusu.Nyasa napakumbuka kwasababu ni nyumbani na napapenda kuliko chochote.Ngoja kuna habari nimezipata kwa wanyasa nitaandika

April 27, 2008

Mgomo wa Mlimani na Sherehe ya Muungano wa Tanzania

Ndugu zanguni mnyasa likuwa kimya tokana na songombingo kama siyo sekeseke na kasheshe la Mgomo wa hapa Chuo kikuu cha Dat es Salaam sehemu ya mlimani.Kwa jweli nimejikuta nikipata homa na huzuni kwani huwa sipendi haki kudhulumiwa na watawala washenzi kabisa wa aina hii.Iliniuma kutangaziwa sisi wanafunzi wa Mlimani ni wahalifu na wavutaji bangi.Lakini yote hayo yalikuwa yakifanyika ili kutimiza ngebe zao za kijinga na ushenzi wao mkubwa.Ninaandika kwa huzuni lakini wanamapinduzi kamwe hatuachi kuhoji ushenzi kama huu.Lakini kwa jina la Mwalimu Nyerere uhuru utadumu hata kama hawataki kuacha huru mapambano yanaendelea.......Naam muungano wa Tanzania,yaani natafuta picha ambazi zinaweaza kunifanya nimwone mwal;imu wangu wa kufikiri Julius Kambarage Nyerere,ngoja naendelea kuzisaka nitaiweka hapa

April 20, 2008

Ziwa Limechafuka,Wanyasa na Ngalawa Tu

Nilikaa juu ya jiwe nikiangaza huku na huko kuwatazama wanyasa wanavyohaha katika shughuli zao za maisha ya hapa na pale.Nikaona ngalawa zinaumiza vifua vya wanyasa kwani hali siyo nzuri katika ziwa kwa sasa.Hakika ziwa nyasa limechafuka namaanisha dhoruba kali sana wiki hili,kila myasa/mvuvi unayemuona kanuna,kafura kama chatu ghadhabu imejaza vibaba wala haimithiriki zaidi ya hapo,hawacheki.Ziwa linanguruma mawimbi makali makali,nyavu zinapotea nyakati hizi shauri maboya yanazama kwa kushindwa kuhimili nguvu ya mawimbi.Lakini pamoja na kuchafuka kwa ziwa hilo hakuna hata mvuvi anayethubutu kusema atabaki nyumbani kujipumzisha au kurejesha zana za uvuvi nyumbani ili kupisha dhoruba hiyo,wapi bwana sahau kabisa habari ya wanyasa kuogopa dhoruba nyakati hizi au kuacha ngalawa ili kukosa kitoweo,hakuna mnyasa anayefikiri kula nyama za kuku wasiokomaa,wanaotafunika hata mifupi,wanaokuzwa kwa kudungwa sindano,wanatia kinyaa kuwala,au chipsi za huko mijini.Wanyasa wanaelewa uzuri wa kuwa wajuzi wa ziwa hili ambalo wenyewe wanasadiki kuwa hakuna ziwa lenye dhoruba kali ulimwenguni zaidi ya hili.Hakuna aliyeka chini kuacha ngalawa au kuacha kupanda mitumbwi.Yaani uvuvi unaendelea kana kwamba ziwa lipo shwari wakati "limekasirika" utafikiri limedungwa sindano ya kukasirika.Yote hao ni kitoweo cha asili hiki utamu adimu huu.

September 05, 2007

Unakumbuka 'inshu' ya Dito au umesahau

Jamaa hapa ananidokeza ndogo ndogo za mjini Mbinga na maeneo mengine ya nchi hususani Darisalama eti kuna jamaa wandai haki katika kesi zao kama ilivyokuwa kwa mtuhumiwa wa m******** ya kijana wa daladala huko Darisalama,ndugu Dito mzuri.

Jamaa wanaona kesi yao haitendewi haki hivyo wanatumia jina la Dito angalu kudai kile wanchoita haki.Lakini hivi haki ni nini hasa?mbona watu wanalalamika sana suala hilo.
Inawezekana kuna namna ambayo kila raia anapaswa kumiliki haki hiyo hata hivyo imetoweka na kuchukuliwa na watu mithili ya dito,mimi sijui maana kazi yangu kuvua samaki kwetu nyasa lakini suala la sheria namwachia Ndesanjo anajua hizo kesi ni nini.

Hta kama atabeza kazi kwake maana ye' ni mwanasheria mahiri tu.kama humjui hebu zama hapa www.jikomboe.com

August 31, 2007

Da' Maria karibu

Kupiga gumzo mtandaoni ni raha sana,basi jana nikaanza kuandika ujumbe kwa dada Maria Mtawali..sijui yuko wapi siku hizi hasemi mahali alipo labda ananiogopa.Nikawa naandika ujumbe kadhaa kwa ajili yake...mara nikakuta ujumbe unaoniuliza 'nyasa' ni nini? halafu...'wewe ni mnyasa?' duuh! kufikia hapo nikaona sasa dadangu amenikuana sana anaponiuliza kuhusu nyasa.

Ndiyo..tunavua samaki aina tofauti,kwanza hata wengine hawajui hata nikisema samaki ndio nin..si hiyo misangara yenu ila mandongo,kambale,ngorokoro n.k au waulize wale wazungu kule Liuli wanafanya nini,kisha njoo makao makuu yangu hapa LUNDU niambie unataka samaki wa aina gani au unataka mihogo ya kutafuna ambayo huko ughaibuni wengine wanasikia tu hewani.

Lakini dada maria miye ni toto la kinyasa yaani usijaribu yaani nakupenda nyasa kwangu hapa,kwani nguvu za kukaa katika kompyuta wananipa wao.Jana nilikula sana samaki kutoka mtera halafu nikabeza hawana hata harara kwa mwenye njaa.
Da' maria mi ndio mwenyewe nipo nimetulia nakukaribisha.....njooooo...katika darasa la Ndesanjo hili tujidai mpaka basii