Showing posts with label Maendeleo. Show all posts
Showing posts with label Maendeleo. Show all posts
March 26, 2018
NGUZO ZA GATI LA BANDARI YA NDUMBI
March 01, 2018
USHAURI KWA RAIS: NAKUOMBA KUBALI TUENDELEE KUCHANGISHANA
NA.HONORIUS
MPANGALA
KWANZA kabisa nianze na kukusalimia shikamoo
mheshimiwa Rais wangu, Dk. John Pombe Magufuli. Najua hii kazi ni ngumu kama
usemavyo wewe mwenyewe lakini sina budi kukuombea uione nyepesi ili uweze
kupata nguvu ya kututumikia vyema kama yalivyokuwa malengo yako siku unaenda
kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.
Mheshimiwa nikiwa safarini kuelekea makao makuu
ya nchi yetu Dodoma, katika gari nilipata tafakuri ambayo ilinifanya
nitoe kitabu changu cha kuandika kumbukumbu na kuhifadhi mawazo yangu ambayo
nimeona nikuandikie.
Hoja yangu kubwa ambayo ilikuwa ikizunguka katika
kichwa changu ni ile niliyokumbuka kauli yako ya kupiga marufuku wananchi
kuchangishwa mchango wowote katika shule za serikali.
February 28, 2018
NAFASI ZA KAZI MAMLAKA YA BARABARA VIJIJINI "TARURA" MKOA WA RUVUMA
February 13, 2018
JE, WAKALA WA MAJENGO NCHINI (TBA) WANAO UWEZO WA KUKIDHI MAHITAJI YA SEKTA YA UJENZI?
Jengo hili linalotakiwa
kujengwa na TBA halijaisha hadi leo. Lipo Halmashauri ya Madaba, mkoani Ruvuma. Haifahamiki
litajengwa lini au wakati gani. Hali hiyo inachochea baadhi ya mafundi kuondoka. Chanzo cha habari kimesema, “Hata
kwetu Nyasa wapo tunatimua muda sio mrefu hao (TBA) sio wenyewe,”
DC SONGEA
Naye mkuu wa wilaya ya Songea
amekasirishwa na utendaji duni wa TBA. DC huyo amesema, “DC SONGEA HAIWEZEKANI
UJENZI WA GOROFA HATA KOKOTA HAKUNA TBA MNASUMBUA WATU,”
Mkuu huyo amewataka wakala wa uthibiti wa majengo TANZANIA
TBA kuharakisha ujenzi wa ofisi ya mkurugenzi wa Madaba kwa wakati ili kusogeza
huduma kwa wananchi. Katika wilaya ya Nyasa wanajenga ghorofa la ofisi ya Mkurugenzi,
Chuo cha Veta, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya (DC) na Nyumba ya Mkuu wa Wilaya (DC).
February 12, 2018
ANA KWA ANA NA MBUNGE WA VITI MAALUMU CHADEMA, NDUGU UPENDO PENEZA
Sisi katika blogu yetu tunakutana
na wanasiasa mbalimbali bila kujali itikadi zao. Au pia viongozi wa kila kada
tunazungumza nao bila kujali fani zao.
Madhali wengi wao ni marafiki
zetu maana ni watanzania wenzetu basi huwa tunazungumza nao mambo yahusuyo ustawi wa jamii yetu kwa ujumla wake. Tunazungumzia
maendeleo ya elimu, uchumi, siasa, utamaduni, afya na kadhalika.
Madhumuni yetu ni kuendelea
kuzungumzia maendeleo ya wananchi pamoja na furaha ya jamii. Tunajikita katika
maslahi ya taifa letu. Tanzania ni nchi yetu na hatuna kwingine. Tutailinda na
kuikosoa ikibidi.
Pichani; kutoka kushoto ni
Gabriel Mushi (mwandishi wa gazeti la RAI), mhariri wa Blogu hii Markus
Mpangala (katikati) na Mbunge wa Viti maalumu ndugu Upendo Peneza.
February 02, 2018
KAHAWA YA MBINGA, MABADILIKO NI HATUA
Nakumbuka zamani tulikuwa tunatumia pumba za kiwanda cha
kukoboa Kahawa Mbinga kufanya mazoezi ikiwemo kuruka sarakasi. Kiwanda hicho
kipo mtaa wa Kiwandani unaopakana na Msimbazi. Zamani Kiwanda cha Mbinga
kilikuwa kinajishughulisha na Kukoboa Kahawa peke yake. lakini sasa mabadiliko
ni makubwa hadi kutengeneza Kahawa yenyewe kuweka kwenye paketi na kuziuza.
Mabadiliko ni hatua.
Markus Mpangala,
Dar es salaam
January 19, 2018
HAPO NI ENEO LA LWIKA KATIKA KIJIJI CHA LUNDO
Madhumuni
kazi,
kumbukumbu,
lundo,
Maendeleo,
maisha
January 17, 2018
HALMASHAURI YA WILAYA YA NYASA INAO WAJIBU WA KUHUDUMIA BARABARA ZAKE
UJUMBE WANGU: Halmashauri ya
Nyasa inao wajibu wa kuhudumia barabara zake wakati wote si kujaza vifusi
kwakuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu anapotembelea au kiongozi yeyote, au shughuli
yoyote ya muda inapofanyika. Barabara ni nyenzo muhimu sana ya kukuza uchumi wa
eneo lolote. Kila la heri wahusika. Tutaendelea kukumbushana.
January 15, 2018
ELIMU BURE INAVYOTESA WATOTO WA WANANCHI WA HALI YA CHINI
NA HONORIUS MPANGALA
KITAALUMA na hisia zangu
zimenifanya niwe mtu tofauti kabisa kuhusiana na matumizi ya baadhi ya maneno
hapa nchini. Mengi hutumiwa na viongozi wa ngazi za juu kuwaona wale waliopo
chini au wasio na vyeo kama wao kuwa
wenye kiwango fulani cha dhiki kinachostahili kuitwa cha chini. Ni hapo
ndipo nakuwa na hisia tofauti sana juu ya kutumia maneno fulani dhidi ya kundi
jingine hasa lile ninaloongoza au viongozi wanaloliongoza.
Japokuwa nimekuwa mtu nisiyependezwa
na na hili neno “Wananchi wa hali ya chini”' lakini najiuliza hao wa hali ya
juu ni akina nani, wanafanya nini kutokuwa na hali ya chini na njia zao zikoje
ili tuwaambie wa hali ya chini wajifunze kwenda huko juu?
January 12, 2018
JIMBO LA NYASA: KWANINI WANANCHI WA TARAFA YA RUHUHU WAMEACHWA UKIWA?
NA MARKUS MPANGALA
Kwa
mujibu wa sensa ya mwaka wa 2012, Kata ya Mbaha ilikuwa na wakazi wapatao 6,972.
Ni Kata ambayo ndiyo mwenyeji wa Shule ya Sekondari ya Monica Mbega iliyoanzishwa
rasmi mwaka 2006. Jina la shule hiyo lilitokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma, Monica Mbega kabla ya kuondoka.
![]() |
| Ubovu wa Barabara katika kijiji cha Ndumbi. |
RUHUHU
ni miongoni mwa Tarafa zinazounda Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa. Wilaya hii ni
miongoni mwa zingine kama Songea Vijijini, Songea Mjini, Mbinga, Namtumbo, Tunduru
zilizopo mkoani Ruvuma. Wilaya ya Nyasa ilianzishwa rasmi mnamo Machi 2012 baada
ya kugawanywa wilaya ya Mbinga. Eneo la wilaya ya Nyasa liko kando la Ziwa
Nyasa.
Tarafa
ya Ruhuhu ipo kwenye mwambao huo, ikiwa ni miongoni mwa maeneo yaliyoachwa nyuma
kimaendeleo na kiuchumi. Tarafa hiyo inazo Kata za; Mbaha, Lituhi, Ngumbo na
Liwundi.
Kwa
mujibu wa sensa ya mwaka wa 2012, Kata ya Mbaha ilikuwa na wakazi wapatao 6,972.
Ni Kata ambayo ndiyo mwenyeji wa Shule ya Sekondari ya Monica Mbega iliyoanzishwa
rasmi mwaka 2006. Jina la shule hiyo lilitokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma, Monica Mbega kabla ya kuondoka.
Wananchi
wa Tarafa hii wanakabiliwa na changamoto nyingi mno hali ambayo inadhoofisha
ukuaji wa uchumi. Changamoto hizo zinatokea katika nyakati tofauti na kuziba
mianya ya kujipatia pato kutokana na huduma kadhaa wa kadhaa kuwa dhaifu.
BENKI YA DUNIA YATOA MSAADA WA KUBORESHA KITUO CHA AFYA MKILI
NA MWANDISHI WETU
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Benki ya Dunia wametoa
msaada wa shilingi milioni 400 kwa Kituo cha Afya cha Mkili kilichopo Kata ya
Ngumbo wilayani Nyasa mkoani Ruvuma kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma
bora za Afya kwa wananchi kwa ujumla.
January 10, 2018
UJUMBE WA CHINA NDANI YA NYASA
Ni Mwenyekiti wa chama cha
Wawekezaji kutoka China hapa nchini, Bwana Ding (Mwenye shati nyeupe), mbele ya
Naibu Waziri Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Injinia Stella Manyanya, ambaye pia
ni Mbunge wa Jimbo la Nyasa mkoani Ruvuma. Naibu waziri na mwenyekiti huyo
walikutana katika tamasha la utamaduni la Nyasa linalofanyika kila mwaka Disemba
31/2017 hadi Januari 6, 2018 mjini Mbamba Bay. Mwenyekiti huyo amethibitisha
kuhamasika kujenga Viwanda kwenye Wilaya ya Nyasa. Tuvute Subira.
PICHA NA GEORGE NDIMBO, DIWANI
WA KATA YA KIHAGARA.
January 05, 2018
AMBULANCE YA HOSPITAL YA WILAYA NYASA ILIVYONUSURIKA KUANGUKA.
NA
HONORIUS MPANGALA, LUNDU
AWALI
niombe radhi kwa kukosa picha kwasababu nilipofika eneo la tukio simu yangu
ilizima moto. Nakumbuka nilitumia simu yangu ndogo kumweleza kakangu Markus Mpangala kuwa narejea nyumbani
lakini tumesimama mahali kuna gari inasaidiwa kunasuliwa toka ilikoegema. Ni
mlima wa kwanza ukitoka kijiji cha Kihagara eneo la Camp, tulikuta hiyo Ambulance
ikiwa imeshindwa kupanda mlima kwa uterezi na kuburuzika hadi pembezoni mwa
barabara. Jambo la kuahukuru ni kwamba ilikuja kugota kwenye jiwe vinginevyo
ingelala kwa ubavu katika kuta za barabara.
![]() |
| Barabara ya Lituhi kwenda Mbamba Bay eneo la mtaa wa Likwambe katika Kijiji cha Lundu wilayani Nyasa. |
Subscribe to:
Posts (Atom)















