Showing posts with label kumbukumbu. Show all posts
Showing posts with label kumbukumbu. Show all posts

February 28, 2018

SIKU YA MASHUJAA SONGEA


Wanafunzi wa shule mbalimbali wa Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, wakiliangalia kaburi la Nduna Songea Mbano, aliyezikwa kiwiliwili tu na kichwa chake kupelekwa Ujerumani, kwa kuwasumbua wajerumani kukata kamba ya katani Mara tatu na baadaye kupigwa risasi. Mashujaa wengine 65 walizikwa katika kaburi moja halaiki. Leo ni kumbukizi za mashujaa wa vita vya majimaji walionyongwa miaka 112 iliyopita. (27.02.1906).

PICHA NA JUMA NYUMAYO

February 17, 2018

R.I.P AKWILINA, ETI MKOA WA DAR ES SALAAM UNA BARABARA ZA HEWANI ZA KUPITA DALADALA!!


 MIAKA mitano iliyopita nilipata kuandika kuwa, ‘utamaduni wa wananchi kupigwa risasi, kushambuliwa kwa riasi za moto, kushuhudia wapendwa wao wakifariki dunia mbele ya macho yao, kuna matokeo hasi yenye athari kubwa nchi yetu. 
 
Nilisema wananchi wanazoeshwa kupigwa risasi za moto. Wanazoeshwa kuuana. Watatamani kuuana. Watatamani kujiua. Wanazoeshwa kuchukia kwa vitendo vinavyoumiza mioyo yao.  

Mwishowe nilisema kuwa wananchi hawa wanapotenda jinai wakitumia mapanga, marungu au visu, jawabu ni kwamba wanatumia vitu hivyo kwasababu ‘hawana bastola wala bunduki’. 

January 24, 2018

KITOWEO KATIKATI YA MANDHARI MAZURI NA YA KUVUTIA KATIKA UFUKWE WA NYASA

Dagaa Nyasa wakiwa wameandaliwa tayari kwa kuchomwa na kuandaa kitoweo.
Mandhari ya Nyasa
Mandhari ya maeneo ya kupumzika ufukweni

January 19, 2018

HAPO NI ENEO LA LWIKA KATIKA KIJIJI CHA LUNDO

Leo hii hakuna Mawasiliano ya Barabara toka Mbamba Bay to Kilosa....Bus zilizotoka   Mbinga na Songea Zimeishia shell pale Tambachi Kuna Calvart Limekwenda na maji watu wanahangaika hawajui cha kufanya.Hali ya mawasiliano kwa njia barabara ilikuwa mbaya sana siku ya tarehe 18/1/2017.

TAITU BETUL: MALKIA JASIRI ALIYEASISI MJI MKUU WA ETHIOPIA, ADDIS ABABA.

Na Kizito Mpangala

Taitu Betul alizaliwa mwaka 1851 nchini Ethiopia ambayo wakati huo ilikuwa ni Milki ya Ethiopia kabla ya kuwa Jamhuri. Neno Taitu kwao lilimaanisha “mng’ao wa jua au jua”, hilo ndilo lilikuwa jina lake la asili.
Baada ya kubatizwa katika kanisa la dhehebu la Orthodox aliitwa Walatta Mikael, lakini baadae alilirudia jina lake la asili yaani Taitu Betul. Baba yake alikuwa aliitwa Betul Haile Maryam ambaye alikuwa na uhusiano na ukoo wa Mfalme Sulemani. Lakini baba yake huyo hakufahamika sana kama alivyofahamika mjomba wake  aliyeitwa Dejazmach Wube Haile Maryam, ambaye alikuwa mtawala wa Ethiopia Kaskazini miaka ya 1840.
Familia ya baba yake Taitu ilikuwa imeweka makazi yake katika mkoa wa Semien ambao ulikuwa ukitawaliwa na Mfalme Susenyos I. Baba yake alikuwa ni mjukuu wa Ras Gugsa ambaye alikuwa mshirika wa familia iliyotawala eneo la Yejju iliyokuwa na asili ya kabila la Oromo. Baba yake huyo alikuwa Muislamu na baadae akabadili dhehebu akajiunga na Ukristo.

Taitu Betul alikuwa na nafasi kubwa ya kuwepo katika ngazi za juu katika maeneo hayo kutokana na ndugu zake wengi kuwa katika nafasi za milki mbalimbali hasa katika ngazi za mikoa. 

Taitu Betul aliolewa mara nne na kuachwa kabla ya kukutana na Mfalme Menelik wa Shewa kama mke wa tatu. Muda mfupi baadae, baada ya kuolewa na Mfalme Menelik wa Shewa, Mfalme huyo akatawazwa kuwa Mfalme wa Milki ya Ethiopia (Ethiopian Empire). Taitu Betul akiwa kama Malkia pamoja na mumewe Mfalme Menelik II walikuwa wanamiliki watumwa elfu sabini (70,000).

January 11, 2018

AFYA, IMANI NA HUDUMA LUNDU

Hapa ndipo tunapopata busara za kiroho tuwapo kijijini kwetu Lundu (Nyasa). Lilijengwa mwaka 1946. Awali wamisionari walifanya makao yao katika mlima Chipyaghela (haupo pichani).
Eneo walilofanya makao mlimani hapo lilikuwa linakumbwa na upepo mkali sana nyakati za kiangazi, ndipo mwaka 1929 wamisionari hao wakiongozwa na Padre Adrian (Mjerumani) waliiomba serikali ya kijiji cha Lundu kuwashawishi wazee Machwembele na Lipondelu ambao walikuwa ni wa ukoo wa akina Mpangala.
Ni ukoo ulioshika maeneo mengi yanayoizunguka misheni kijiji cha Lundu. Basi baada ya serikali kuwashawishi wazee Machwembele na Lipondelu, waliamua kuwapa wamisionari eneo la kujenga kanisa la kuanzia na nyumba ya kuishi mapadre.

January 04, 2018

BENKI KUU YAFUTA LESENI ZA MABENKI MATANO

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imezifutia leseni, na kuzifungia kufanya shughuli zozote, benki 5 za kibiashara ambazo ni Covenant Bank, Efatha Bank, Njombe Community Bank, Meru Community Bank na Kagera Farmers Cooperative Bank. Sasa wateja wa benki hizo watalazimika kuwasiliana na BOT ili kujua hatma yao.

December 30, 2017

PUGU HADI PERAMIHO; Kijiji cha Dar, Utemi wa Wangoni na kumbukizi maridhawa.

Katika kitabu cha "PUGU HADI PERAMIHO" kuna masimulizi ya kutoka mwaka 1888-1988 na ujio wa Wamisionari wa kijerumani kupitia Shirika lao la Benedictine Fathers lenye makao yale mjini Peramiho kwa sasa.  
Kitabu hiki ni mkusanyiko wa barua na kumbukizi binafsi (Diaries) zilizoandikwa na Mapadre, Mabruda, Masista wakielezea masuala ya ukoloni wa Kijerumani, Injili, Umisionari, Wapagazi, Wangoni na kupenda vita na starehe pamoja na mahusiano ya kibadamu kati ya wazungu na waafrika.

PADRE ANDREAS AMRHREIN
Kitabu hiki kinaanza kwa maandiko ya Abate Lambert Doerr, OSB. Kwanza "Abate" ni wadhifa waliopewa wakuu wa mashirika ya Benedictine Fathers. Lambert anafungua pazia la masimulizi ya Wamisionari Wabenediktine kusini mwa Tanzania. 

December 28, 2017

UMENG’ATWA NA MANYIGU, LAKINI KIU BADO UNAYO.

NIKIWA njiani kurejea Dar es salaam, mdogo wangu Honorius Mpangala alinitumia ujumbe mfupi katika simu yangu, “Aisee tupo Tingitingi, lakini nimeng’atwa na manyigu. Vifaa tulibeba kama kawaida,”. 
  
Nikashangaa. Sikufikiria kama eneo lile laweza kuwa na manyigu au hatari zozote za wanyama wakali. Leo pichani anasema, “Nikiwa najikagua mkono na miguu baada ya kung'atwa na manyigu saba. Ilikuwa tarehe 25/12 saa saba mchana pori moja kando ya ziwa Nyasa.Pori lenye msitu unaogota katika maji ukiwa na mawe makubwa huko ndo maskani ya wanyama kama ngedere, nyoka, nungunungu, mijusi wa rangi rangi,ndege kama kanga pori na Kwale. Baada ya shambulizi nilijiziba uso na kuacha sehemu ya miguu kuwa wazi lakini ajabu niling'atwa hadi kwenye makalio,”.

December 27, 2017

...KUMBUKIZI ZA MZEE MPANGALA NA WAMISIONARI WABENEDIKTINE LUNDU



Mwaka 1931 Wamisionari waliomba eneo la kujenga himaya yao ya kitawa kwa serikali ya kijiji cha Lundu. Baada ya pendekezo lao serikali iliwaomba wazee wawili kutoka Ukoo wa Mpangala ili kuwapa Wamisionari hao eneo la kujenga makazi ya Kitawa.
Alikuwa Mzee Machwembeli Mpangala (Baba yake Mzee Hansgary Mpangala au Waziri) na Lipondelu Mpangala (Babu yake Mzee Hubungu au Robert Mpangala).Mzee Machwembeli alikuwa anamiliki eneo la kuanzia kilipo kituo cha afya kuelekea kaskazini( Kwa wale wanao ifahamu Lundu) na Mzee Lipondelu alitoa kuanzia Hapo kituo cha afya kuelekea Kusini iliko nyumba ya mapadre.
1959 Walijenga machine ya kupump maji toka forodha ya Chivanga hadi eneo la misheni.Mzee alishiriki ujenzi Huo akiwa na Bruda Lambert. Ananiambia gari ya kwanza kufika kijijini kwetu ilikuwa ni 1954.
Asubuhi ya Leo alinipiga na salamu ya kijerumani nikabaki natoa macho tu.Uishi miaka mingi zaidi Mzee wangu.

Honorius Mpangala,
#Mtoto_Wa_Misheni

November 12, 2017

NANA YAA ASANTEWAA: MALKIA WA MILKI YA ASHANTI ALIYEWAKINGIA KIFUA WAKOLONI WAINGEREZA.

Na Kizito Mpangala

Alizaliwa mwaka 1863 katika mji wa Besease katika jamii ya Ashanti yenye dhahabu nyingi, Ghana ya sasa, magharibi mwa Afrika. Kaka yake Nana Akwasi Afrane alikuwa ndiye Edweso (kiongozi, au chifu) wa milki ya Ashanti wakati huo. Nana Yaa Asantewaa akiwa bado binti alijishughulisha sana na kilimo. 

Kaka yake (chifu Akwasi) alipokuwa Edweso (kiongozi) alituma askari wake kwenda mapiganoni dhidi ya wakoloni. Baadae aliwekwa kizuizini na wakoloni katika visiwa vya Ushelisheli pamoja na mfalme Prempeh I. Akiwa kizuizini, Nana Akwasi Afrane alimteua dada yake NANA YAA ASANTEWAA kuwa malkia wa milki ya Asante. 

Mwaka 1899 gavana wa wakoloni Waingereza Frederick Hodgson aliitisha mkutano mjini Kumasi ili kulazimisha apewe kiti kilichotengenezwa kwa dhahabu tupu ambacho ni alama takatifu ya Ashanti ambapo askari wa kikoloni walishindwa kukipata kiti hicho, hii ni baada ya kufikiri kwamba ugumu wa kuwatawala Waashanti ungeisha baada ya kupata kiti hicho cha dhahabu. Nana Yaa Asantewaa alimteua mjukuu wake mkubwa kuwa mkuu wa miliki ya Ashanti mara baada ya kufariki kaka yake. 

October 27, 2017

FELA ANIKULAPO KUTI: MWANAMUZIKI ALIYEASISI MTINDO WA PIJINI KATIKA MUZIKI NCHINI NIGERIA NA KUOA WANAWAKE 27.

NA KIZITO MPANGALA

TUNASIKILIZA muziki wa Nigeria mara kwa mara na pengine huenda uliwahi kujihoji aina lugha wanayotumia kuimba na hata katika mazungumzo ya kwaida ya wananchi wa Nigeria. Mtindo huo umejaa pijini kwa kiasi kikubwa hali iliyopelekea kuitwa NIGERIAN ENGLISH.

Fela Anikulapo Kuti alizaliwa  mjini Abeokuta nchini Nigeria mwaka 1938. Alipewa majina OLUFELA OLUSEGUN OLUDOTUM RANSOME ANIKULAPO KUTI lakini alifupisha na kuwa FELA ANIKULAPO KUTI. Mama yake alikuwa ni mwanaharakati wa haki za wanawake katika utawala wa kikoloni wakati huo, na baba yake alikuwa ni mwalimu na vilevile alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kwanza mweusi wa chama cha walimu nchini Nigeria. Fela ni binamu ya Akimwande Oluwole Babatubde Soyinka maarufu kama Wole Soyinka.

Fela alisoma nchini Nigeria na baadae mwaka 1958 alikwenda nchini Uingereza kwa ajili ya kusoma Udakitari wa Dawa lakini alipofika huko alivutiwa na masomo ya muziki hivyo akasoma masomo hayo ya muziki katika chuo cha Trinity. Fela alikuwa mjuzi wa kupiga tarumbeta na Saxophone.

Alianzisha bendi yake iliyoitwa Koola Labitos ambayo ilipiga muziki aina ya jazz.  Huko alimuoa mwanamke aliyeitwa Remilekun Taylor na wakawa na watoto watatu. Mwaka 1963 alirudi nchini Nigeria na kuendelea na bendi yake aliyoianzisha na pia utangazaji katika shirika la utangazaji redioni la Nigeria.
Mwaka 1967 alihamia nchini Ghana na kuanzisha mtindo mpya wa muziki ambao uliitwa Afrobeat. Mwaka 1979 alisafiri kwenda Marekani na alikaa kwa muda wa miezi 10 jijini Los Angels, huko alibadili jina la bendi yake na kuitwa NIGERIA 70. Baadae alitimuliwa nchini humo pamoja na waimbaji wenzake kwa kutokuwa na kibali cha kufanya kazi nchini humo.

October 22, 2017

PHILIP EMEAGWALI: MWANASAYANSI YA KOMPYUTA ALIYEIPA KASI ZAIDI INTANETI TUNAYOTUMIA SASA.

NA KIZITO MPANGALA

SOTE tunafurahia kutumia mtanadao wa kimataifa “international network” ambapo kwa utaalamu zaidi wa lugha maneno hayo mawili yamefupishwa kwa kuchukua herufi tano za mwanzo za neno INTERnet na haerufi mbili za mwanzo za neno NETwork na kupata neno INTERNET yaani mtandao wa kimataifa, na katika Kiswahili tumetoho na kpata neno INTANETI.

Mtandao huo unatusaidia kwa kiasi kikubwa sana katika shughuli mbalimbali. Wapo waliotumia muda na maarifa yao kwa ajili ya manufaa ya ulimwengu wote. Mtandao huo ulipoanzishwa haukuwa na nguvu kubwa ya “kukata mitaa” ya dunuia yote hii, lakini leo mtandao huu una pilikapilika nyingi na sehemu nyingi duniani na una matumizi makubwa. Ada yako ya kutumia intaneti ni bando tu!

October 19, 2017

STEPHEN HAWKING: MWANAFIZIKIA MGONJWA WA MUDA MREFU.

NA KIZITO MPANGALA

STEPHEN HAWKING alizaliwa mwaka 1942 jijini Oxford nchini Uingereza kwa wazazi Frank Hawking na Isobel Hawking. Japokuwa familia yake ilikuwa na mtikisiko kifedha lakini wazazi wake walijitahidi kujiendeleza kielimu katika chuo kikuu cha Oxford. Baba yake alisoma udakitari wa dawa na mama yake alisoma Falsafa, Sayansi ya Siasa, na Uchumi katika chuo hicho.

Baba yake na mama yake walikutana kwa mara ya kwanza muda mfupi tu bada ya kuanza kwa vita ya pili ya dunia katika Taasisi ya Utafiti wa Dawa ambapo baba yake alikuwa mtafiti  na mama yake alikuwa katibu wa taasisi hiyo. Ndipo mapenzi yao yalipoanza na walibahatika kupata mtoto wa kiume ambaye ni Stephen Hawking.

October 14, 2017

HAKUNA WA KUFANANA NA MWALIMU NYERERE

NA MWANDISHI WETU

"Nchi yetu inaongozwa kwa sheria. Hatuwezi kuchagua kiongozi asiyeheshimu sheria akawa anaongoza nchi kwa kushauriwa na mkewe, maana hamjui kesho akiamka atamshauri nini" Mwl. J.K. Nyerere

"Hivyo basi Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira, kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache katika nchi yao wenyewe." Mwl. J.K. Nyerere.
"Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa mawazo, ni umaskini mbaya sana"- Mwl. J.K. Nyerere

"Tatizo la paka kwa panya lingeisha kama paka angefungiwa kengele shingoni: tabu ni kumpata panya wa kuifanya kazi hiyo."- Mwl. J.K. Nyerere
"Mtu aliyejiandikisha kupiga kura, halafu siku ya Uchaguzi haendi kupiga kura, Huyo ni Mpumbavu'' Mwl. J.K. Nyerere

"Dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana, sawa na kula nyama ya mtu,dhambi ya ubaguzi haiishi inaendelea tu, leo utabagua kwa kusema sisi ni Wazanzibari hawa ni Watanganyika ,kesho utasema sisi ni Wanzanzibari hawa ni Wazanzibara. Lazima utaendelea, utaona kuna mpemba na Muunguja. Utaendelea tu haiishi sawa na kula nyama ya mtu" Mwl. J.K. Nyerere

"Ukiona mtu anakwambia jambo la kipumbavu na yeye mwenyewe anajua kuwa unajua ni la kipumbavu..ukilikubali ujue amekudharau" Mwl. J.K. Nyerere

KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE



Pichani ni Nyumba ya Mwalimu Nyerere iliyopo eneo la Magomeni ambayo kwa sasa ni makumbusho ya Taifa. 

Mwaka 1957 Mwalimu akiwa anafundisha shule ya Sekondari Pugu alikusanya mafao yake ya ualimu na akamwomba rafiki yake Mustafa Songambele amtafutie kiwanja katika maeneo hayo, naye akamtafutia kiwanja hicho kilichopo Magomeni, Mtaa wa Ifunda.

Enzi hizo Magomeni ndiyo ilikuwa kama Masaki ya sasa na Mwalimu alitaka kukaa mahali penye mazingira salama na ulinzi ili kuendelea na harakati za kulikomboa Taifa kutoka kwa Mkoloni wa Kiingereza. 

Lakini baadae Mwalimu kwa Moyo wa ajabu akaitoa nyumba yake mwenyewe aliyoijenga kwa jasho lake na mafao yake na kuikabidhi kwa Serikali ya Tanzania ili iwe Makumbusho ya Taifa kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo vikumbuke ni wapi tulipotoka na wapi tunaelekea.


Mwalimu wakati wa Uhai wake katika Ngazi ya Familia alikuwa Baba na Babu pia, angeweza kujilimbikizia yeye na familia yake Mali zote za Taifa lakini kwake Tanzania na Afrika nzima ilikuwa Zaidi ya Maisha yake binafsi na Familia.

October 09, 2017

ZENZILE MIRIAM MAKEBA: MWANAMUZIKI ANAYEKUMBUKWA NA WENGI BARANI AFRIKA.

Na Kizito Mpangala

Zenzile Miriam Makeba alizaliwa mwaka 1932 jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini. Alizaliwa kwa wazazi wenye asili tofauti kikabila, baba yake ni Mxhosa, na mama yake ni Mswazi. Bibi yake alikuwa mkunga wa jadi na ndiye aliye fanikisha z0ezi la kumsaidia mama yake kujifungua salama. Bibi yake huyo alimuasa mama yake Miriam kwamba asione taabu na asijisikie upweka kumlea mtoto (Miriam) katika hali duni ya maisha kwani ndiye aliyemleta ulimwenguni. Alikuwa akimwambia “Uzenzile” kwa lugha ya Xhosa, likimaaniasha “Umemleta wewe mwenyewe”, hivyo akaamua kumpa mtoto huyo jina la ZENZILE MIRIAM MAKEBA.

ZENZILE MIRIAM MAKEBA
Licha ya baba yake kuwa mwalimu, lakini walikabiliwa na ukata ambapo alipotimiza siku 18 tu tangu azaliwe alilazimika kwenda kuishi gerezani na mama yake ili apate kunyonya. Aliishi gerezani na mama yake kwa muda wa miezi sita, hii ni kutokana na Makaburu walioshinikizwa na  falsafa ya Apartheid walimhukumu mama yake Miriam kifungo cha miezi sita gerezani licha ya kuwaeleza kuwa ana mtoto mchanga na hajamaliza hata mwezi tangu azaliwe. Lakini hakusikilizwa. Sababu ya kuhukumiwa kifungo hicho ni baada ya kukutwa (mama yake Miriam) akiuza pombe ya kienyeji maarufu sana nchini Afrika Kusini ambayo inaitwa umqombot. Ndugu, jamaa na marfikia walishindwa kumlipia faini kutokana na ukata wa uchumi, hivyo ilibidi akaishi gerezani.

KUMBUKUMBU YA ERNESTO CHE GUEVARA

LEO imetimu miaka 50 tangu mwanamapinduzi wa Argentina Enersto Che Guevara alipouliwa huko Bolivia. Che anafahamika kwa harakati zake za kupigania uhuru wa nchi kama DRC/Cuba na nyingine nyingi. Aliwahi fika Tanzania miaka ya 1960 Kupitia Ujiji-Kigoma na kukaa miezi saba kabla hajaondoka kuelekea Cuba. 
 
Che Guevara alikuwa ni Mwanaharakati/Mwanadiplomasia/Mjamaa na Mwanamapinduzi katika Karne ya ishirini. Mchango wake unakumbukwa na wengi Duniani, alikuwa ni swahiba Mkubwa wa Rais wa Cuba hayati Alejandro Fidel Castro #Socialism.