Showing posts with label mila na desturi. Show all posts
Showing posts with label mila na desturi. Show all posts

October 21, 2017

UCHAMBUZI WA KITABU CHA UHAMASISHAJI

KITABU: ISHINDE TABIA YA KUGHAIRISHA MAMBO
MWANDISHI: JOEL NANAUKA
MCHAMBUZI: MARKUS MPANGALA


JOEL NANAUKA ni miongoni mwa waandishi wazuri katika vitabu vya uhamasishaji na utambuzi. Kitabu chake cha “Ishinde Tabia ya Kughairisha Mambo” kimechapishwa na kampuni ya Benison Communication &Printing iliyopo Dar es salaam na kupewa nambari za usajili ISBN 978-9987-761-99-9.

October 17, 2017

MANDHARI YA KIGOMA

Kigoma Tanzania, Barabara ya kuelekea Makumbusho ya Dr. David Livingstone Ujiji.

October 16, 2017

“RAIS ANA MIAKA 31”


Sebastian Kurz
JUMAMOSI nilikuwa nasoma makala ya James Masters kwenye tovuti ya CNN. Sentesi yake ya kwanza ilinivutia sana, “Ulikuwa unafanya nini ulipokuwa na umri wa miaka 31? Ingawa aliendelea na mengine lakini staili pekee haikuwa kivutio bali mtu aliyekuwa akizungumzwa alivutia zaidi.
James Masters alikuwa anamzungumzia Sebastian Kurz ambaye amewahi kuwa waziri wa  Ushirikiano wa Kimataigfa tangu mwaka 2013 akiwa na miaka 27.  Sebastian  Kurz ambaye amekuwa Kansela wa Austria mwenye umri mdogo zaidi kwani sasa hivi ana miaka 31 tu. 

Ni mwenyekiti wa chama cha  OVP. Sebastian kuanzia jana jumapili aanaongoza serikali ya Austria ( kama vile Rais hapa kwetu) baada ya chama chake kushinda viti vingi vya bunge. 

September 21, 2017

KWANINI MAJAJI WANAVAA MAWIGI?



Kwa wenye taaluma mjadala huu unafaa. Kuna mengine pia yamesema, mfano majina ya Victoria Falls, Ziwa Victoria na kadhalika. Makala hayo yalichapwa kwenye gazeti la THE CITIZEN toleo la Jumatano, Septemba 20, 2017. 

Swali linabaki kwanini Majaji huvaa mawigi hadi sasa wakati ni ishara ya ukoloni? Kwa mujibu wa gazeti hilo Wigi moja hugharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 6,500.

December 21, 2012

NAFASI ZA KAZI DESEMBA HII MPAKA MWEZI JANUARI MWAKA 2013

WADAU: kwa wale wanaoendelea kutafuta kazi mbalimbali kwenye amshirika na taasisi za umma yaani serikalini, kuna nafasi za kazi zimetolewa ambazo nanyi wadau mnatakiwa kuzifuatilia.
Kwahiyo hapa naweka tanagzo hili ambali lionyesha nafasi za kazi katika sekta binafsi na umma.

BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI

November 02, 2012

AMBROCE NKWERA, KIZAZI KIPYA CHA WILAYA YA NYASA NDANI YA MAHAKAMA

Miaka mingi sana imepita wazee wetu wazaliwa wa wilaya za Mkoa wa Ruvuma wemekuwa wakifanya kazi katika sekta mbalimbali, lakini hawana muda wa kutosha kufikiria kurudi nyumbani Nyasa na kufanya kazi karibu na wakazi wao. Lakini wapo vijana wenye tofauti kiasi kikubwa na wazee kama Prof. Nkoma (TCRA), Prof Mpangala (UDSM), Jaji Samatta(Mahakama Kuu), Mataka(ATC) na wengine wengi sana ambao waliozaliwa na kukulia wilaya Nyasa. Aidha, inapendeza pia kuona mzaliwa wa wilaya ya Nyasa James Zotto, akifanya utafiti wake wa masomo ya juu(Masters) katika suala la Utatuzi wa mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa baina ya Malawi na Tanzania. Zotto ni mzaliwa wa mji wa Liuli katika wilaya ya Nyasa.
                                      
                                        AMBROCE NKWERA KAZINI MAHAKAMANI
Hata hivyo kijana AMBROCE NKWERA yeye alisukumwa na nia ya kuwatumikia watu wa wilaya ya Nyasa, lakini amejikuta akipangiwa wilaya ya Mbinga ambayo zamani ilikuwa pamoja na Nyasa. Kwa hakika sio hatua mbaya, bali lengo lake liliongozwa na kuwatumikia watu wa ukanda wa Mkoa wa Ruvuma hususani wilaya za Songea, Tunduru, Mbinga na Nyasa au Ludewa(Iringa).
Baada ya serikali kutangaza nafasi za kazi ya Uhakimu kwa wilaya kadhaa za Nyasa, ndipo kijana huyu akachukua uamuzi wa kuomba nafasi hiyo. Na hadi sasa anaitumikia jamii ya Tanzania hususani wilaya ya Mbinga hivyo kukamilisha ujenzi wa Taifa. Labda swali hapa ni kwanini aliamua 'KURUDI NYUMBANI' ambayo ni sera yetu nami nikiwa mfuasi wake?
Sababu kubwa ni kwamba kuna wafanyakazi waliowahi kuajiriwa na kupangiwa wilaya ya Mbinga ama maeneo ya Wilaya za mkoa Ruvuma halafu hawaendi kufanya kazi vituo vya kazi. Hii ilikuwa ikimkera na kuona kuna haja wazaliwa wa maeneo hayo wenye sifa kuomba kazi ili warejee na kuwatumikia watu wa nyumbani kwao. 

                                          
                                                     AKITOKA KAZINI
Lengo hilo lilifanikiwa baada ya Mahakama kuu kumwajiri AMBROCE NKWERA na kumwapisha huko wilayani Lushoto mkoa wa Tanga. Kwa sasa yeye anatumikia taifa kupitia wilaya ya Mbinga ambayo ni jirani na nyumbani kwao wilaya ya Nyasa.  Yeye ni miongoni mwa walioshauri kuanzishwa mahakama maalumu ya kuwahukumu watu wote wanaoshtakiwa kwa kosa la Ufisadi ambayo anasema sawa na wahujumu uchumi (tutachapisha mahojiano yake siku zijazo).
Kwa hakika anastahili sifa na kupongezwa sababu uamuzi wake licha ya shahada yake ya sheria, akaona kuna haja ya kwenda kufanya kazi maeneo ambayo wengi hawataki kufanya kazi, maana huwa wanaripoti na kuondoka moja kwa moja, hawarudi tena. 
AKIFURAHIA MANDHARI YA MBINGA
Sasa, roho yake imetulia atakuwa HAKIMU mzuri sana, mikono yake itatenda haki na sera yake ya kushawishi wasomi ambao ni wazaliwa wa Wilaya ya Nyasa au Mbinga na nyingine za mkoa wa Ruvuma kwamba ni vyema wakarudi nyumbani kuwatumikia wananchi wao kuliko kulalamikia wageni wanaotoka mikoa mingine kutopendelea kufanya kazi maeneo ya mkoa huo. Mabadiliko na maendeleo yatawafikia watu kwa watu kufanya jitihada za kufanya kazi kwa bidii. Hongera sana Mgosi wa Ndimba AMBROCE NKWERA.

November 01, 2012

AYUBU RIOBA ALIPOTOA NONDO ZA NGUVU CHUO KIKUU CHA TAMPERE, FINLAND

AYUBU RIOBA akiwa katika Chuo Kikuu cha Tampere, jijini Tampere nchini Finland, ambako anapata Shahada ya Udaktari wa Falsafa(Phd) katika Sayansi ya jamii.
Kabla ya kufanikiwa kutunikiwa shahada hiyo, alitumia muda wake zaidi saa mbili(masaa mawili) kutetea utafiti wake juu ya "Media Accountability in Tanzania's Multiparty Democracy: Does Self Regulation Work"?
Baada ya mjadala mzito wa kitaaluma na maswali mengi kutoka kwa Profesa Audrey Gadzekpo kutoka Chuo Kikuu cha Accra, Ghana, pamoja na jopo la Maprofesa walifikia hitimisho na kumtunukia Shahda ya Falsafa ya uDAKTARI(Phd) katika fani ya Sayansi ya Jamii. Bila shaka ni jambo la kujivunia kwa watanzania na kwake AYUBU RIOBA. Mwenyzi Mungu ampe afya njema na kumlinda.

October 27, 2012

NYUMBANI LUNDU

Picha hii inaonyesha maeneo ya kijiji cha Lundu. Maeneo hayo ni mtaa wa Maliwa au Missionari, na wka upande wa magharibi kushoto unaonekana mlima ambao unaitwa Chipyaghela. Kisha maji ya ziwa Nyasa yanaonekana. Huu ndio mji ulionikuza na kunilea, katika mitaa yangu ya Maliwa, au missionari.
Picha hii imepigwa na kaka Egbert Jeremy aliyeko wilaya ya Nyasa katika shughuli za ujenzi wa miundo mbinu. Lundu ni miongoni mwa vijiji ambavyo anaendelea kujenga miundombinu ya wilaya hiyo. Karibuni kuwekeza wilaya ya Nyasa ambayo imeanza kutoa fursa mbalimbali. KARIBUNI NYASA

October 22, 2012

UPIMAJI WA MRADI WA MAJI LUNDU

MTAALAM WA MAJI, EGBERT JEREMY AKIANGALIA RAMANI YA MITARO YA MAJI KATIKA KIJIJI CHA LUNDU KANDOKANDO YA ZIWA NYASA.

April 04, 2010

YALE MAISHA YETU

Nikitazama nyumba kama hizi zinanikumbusha wale wanaoishi katika mazingira haya. Na kwakuwa nayakumbuka mazingira yaliyonizunguka kijijini kwetu nyasa nathubutu kusema najivunia kuishi katika mazingira ya aina hii ambayo yananipa USONGO zaidi wa kuishi kadiri niwezavyo.

Maisha ya aina hii yanasema,hayagombi,hayadanganyi,hayajutii,hayaogopi,hayakatai,hayaingilii uhuru wa mtu,hayasemi zadi ya kile kilichopo. Najivunia hili, najivuni kuyajua na kuendelea kuyaona, yananipa USONGO.Ingawaje kuna tofauti kubwa kati ya WIVU na USONGO. Lakini naamini safari inaweza kuwa na kona.

Je unajua kuwa unajua namna maisha ya binadamu wenzetu wanajua kuwa unaishi katika mazingira gani? Nitazamapo na kukumbuka nyumbani kwetu, nikiyaona haya, napata USONGO. Ni hayo tu.

March 24, 2010

CHEMSHA BONGO, SHINDANO, ZAWADI NONO

KAMA KWELI UNA 'MIAKILI', nataka uanze kusumbua kichwa kwa neno hili.
Hivi karibuni kumezuka neno fulani hivi lenye kumaanisha jambo fulani. Neno lenyewe linaitwa 'MKUU WA POSTA'.

Limeene neno hili, linazidi kukua, lakini usifikirie lina maanisha kazi ya ofisi za Posta, bali ni jina la mtu mwenye tabia fulani hivi.

Mwenye tabia hiyo ndiyo huitwa 'MKUU WA POSTA' ili kumtaja hadharani kutokana na tabia yake hiyo.

JE UNAWEZA KUNG'AMUA NENO HILI LINA MAANISHA NINI KATIKA TABIA?

February 16, 2009

Kitendawili kimewashinda? Karibuni tule basi!

Nilikuwa nangojea waungwana mjitahidi kufunua bongo zenu, nilidhani kwa wanazuoni kama ninyi lazima jawabu lipatikane ..... lakini wapi bwana, maji yamezidi unga..... yaani tatu bila, tatu bila. Haya basi nimekuja na chakula hiki sijui tutashiba maana samaki mmoja, kwahiyo kula ni kula mbaya kukoimba mboga jamani. Karibuni mkekani, mlozowea mezani msahau kwa leo.

January 06, 2009

Vipi unatuonaje, angalia tena

kama napumzika na kazi ya uvuvi yaani unajipa maraha kama haya! taratiiiiiiiiibu kinyasa nyasa siyo mchezo mambo haya.

January 01, 2009

20009+ YASINTA+ Wanablogu


2009 Pamoja daima.Wanablogu wote Nawatakieni mafanikio mema zaidi.Na kudumisha maendeleo ya Blogu zetu.Nimefurahi zaidi kwani jana nilikuwa na mwanablogu dada Yasinta,na kupiga gumzo la hapa na pale.Anatuandalia kitu kingine;tanzaniaresan2009.blogspot.com
NAWATAKIA SAFARI NJEMA.
ZIDUMU BLOGU ZETU na WANABLOGU DAIMA

December 24, 2008

kazi+kumbukumbu

ninakumbuka enzi zile tukilima mpunga, ekari kibao na shangazi yangu pale Ngindo, yaani ilikuwa tka asubuhi saa moja hadi saa kumi na moja jioni. Duuh kwa mwendo wa kuchoka na kulegea kila kitu. nipumue siku hizi huuuuuuuuuuuuuuuuuu nalima kwa kompyuta

December 09, 2008

Najua unanogea+mate yanatoka=urudi nyumbani

najua kabisa unanogea, najua nakupatia HAMU. maana najua bila hamu huwezi kukumbuka kitu. Hawa siyo sawa na dagaa kigoma wanaochacha kama wa enzi zile za KIGONSERA a.k.a CAIGO BOYS, umenisoma kaka Mtanga ha ha ha ha Nina HAMU ndiyo ndiyo maana nakwambia haya. Watazame walivyoanikwa mchangani vizuri halafu unapata NG'ONDA upo hapo. RUDI NYUMBANI ha ha ha ha ha

December 08, 2008

aaaah!! nina HAMU !!!

Nina hamu sana unajua? Nina hamu ndiyo maana nakwambia nina hamu mpaka nashindwa kujizuia. Nina hamu mpaka nataka kulia. Si hamu nyingine bali ya kukusalimia MAMBO? aaaaaah umnielewa huna hamu ya DAGAA wewe?

kazi+juhudi+ubunifu+mapenzi=MAISHA

maisha tu haya kama utapenda nunua tu utakuwa umenisaidia sana maana mwanangu namsomesha kwa kutegemea hii kazi yangu. Nahiheshimu sana. Ni kama anasema hivyo

November 26, 2008

ndizi ndizi KAPOLOTA karibu sana

wale walaji wa ndizi KAPOLOTA karibuni. Dada Yasinta huko ughaibuni unazikumbuka hizi

November 17, 2008

kuvua dagaa usiku


dagaa wa ziwa nyasa ni watamu sana, wananoga mno, ukila unajiumauma tu hamu na kuzidi kunogea. SASA ukitazama picha hii utaona KARABAI zimefungwa mtumbwini, hapo ndipo kazi inafanyika kwani ukisha funga hivyo kazi inaanza kwenda kilindini na anyavu ya kuvulia kusaka kitoweo kunoga na utamu kuliko chochote..... ebu taja kitu kingine kitamu kuliko dagaa? najua utataja nanii....... nini ile ...... sijui ebu inaitwaje!!!! aahaa tuache, hayo. haya ndiyo mambo ya nyasa na zana zao