March 24, 2010

CHEMSHA BONGO, SHINDANO, ZAWADI NONO

KAMA KWELI UNA 'MIAKILI', nataka uanze kusumbua kichwa kwa neno hili.
Hivi karibuni kumezuka neno fulani hivi lenye kumaanisha jambo fulani. Neno lenyewe linaitwa 'MKUU WA POSTA'.

Limeene neno hili, linazidi kukua, lakini usifikirie lina maanisha kazi ya ofisi za Posta, bali ni jina la mtu mwenye tabia fulani hivi.

Mwenye tabia hiyo ndiyo huitwa 'MKUU WA POSTA' ili kumtaja hadharani kutokana na tabia yake hiyo.

JE UNAWEZA KUNG'AMUA NENO HILI LINA MAANISHA NINI KATIKA TABIA?

3 comments:

  1. Duh, kazi kweli, mimi nafikiri ni msafisha choo au vipi!
    Vinginevyo basi ndio bosi wa kazini.

    ReplyDelete
  2. Nabunia jibu ni KIRUKA NJIA.

    Tukupe mji nadhani mkuu!

    ReplyDelete

Maoni yako