February 26, 2018

RIWAYA: SAA 72

Ijumaa iliyopita ndugu Japhet Nyang’oro Sudi aliwasiliana nami kunijulisha kuwa nimetunukiwa zawadi ya kitabu chake. Yeye ni mwandishi wa riwaya ya SAA 72. Hima jumamosi nikawasili kwa bwana George (Muuza vitabu huyu; simu yake; 0713 454152). George huuza vitabu vyake pembeni ya sanamu la Askari  jijini Dar es salaam (Posta Mpya). ana vitabu vingi, waweza kulonga naye kujipatia nakala zaidi. Nilianza kusoma kitabu hicho Jumapili asubuhi yapata saa 4 hivi, hadi saa 2 usiku. Nikatamatisha. Kina kurasa 202.
Masimulizi ya kitabu hiki ni kuhusiana na mgogoro wa vita vya wenyewe kwa wenyewe unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo Joseph Katanga anaachiliwa huru na Makahama ya kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa madai ya kubadilika kitabia). Lakini Katanga hakubadilika chochote. Alitumia kila njia kuendesha maasi kwa wanavijiji, na kudhoofisha utawala waDRC. Machache tunayoweza kujifunza.

1.Zonu amechorwa kama mwanamuziki lakini anautumia kujificha kuwa mdunguaji anayewaunga mkono waasi wanaoongozwa na Joseph Katanga. Kazi yake kuua wanajeshi wa vyeto vya juu. Muziki wake unateka wengi lakini nyuma ya pazia ni muas sambamba na Joseph Katanga.

2. Ushirikiano wanaopata waasi kutoka jeshi la serikali ni chanzo cha kushindikana kutokemezwa kwa vita hivyo tangu enzi za Patrice Lumumba. Ingawaje ni simulizi pana ukweli juu ya ushirikiano huu. Jeneral Faustin Munene amekamatwa Januari 10 mwaka huu nchini Gabon kwa kosa la mwaka 2011 la kutaka kuipindua serikali ya rais Kabila. Naye Kanali John Tshibangu anye alikamatwa Februai 1 hapa hapa Dar es salaam na kupelekwa DRC. Wote wawili walikusudia kumpindua Kabila. Ushirikiano wa waasi na jeshi.

3. UBAKAJI. Mara nyingi wanaoendesha vitendo vya ubakaji ni wale wanaofahamika kwa wabakwaji. Kwamba mwanamke anaweza kubakwa na mtu ambaye hakutegemea kama atatenda hilo. Tuzichunge njia zetu.

4. Mwanadamu yupo radhi kumwaga damu ili atomize kiu yake. (Dr. Jean au KK).

5.Juliana Owima anawakilishi kundi la wanawake ambao hutajwa kuwa wanaweza kuwa mashushushu wazuri kuliko wanaume. Ni binti pandikizi, lakini hasara ya kuwa pandikizi wan chi fulani mahali ni ukosefu wa UHAKIKA wapi utaendesha maisha yako kati ya nchi uliyopandikizwa na nchi yako. (Hapa nakumbuka mkasa wa Josephine Baker mzaliwa wa Marekani aliyekwenda kuishi Ufaransa. Akatumia muziki kama kichaka cha kuficha ushushushu wake). Pandikizwa, ila akili kichwani.

“Hiyo ndiyo tofauti yetu majasusi na ninyi wapelelezi. Siye hutumia gharama kubwa na miaka mingi kuweza kuingia kwnye mfumo wa adui, lakini ninyi hufanya kazi kwa lengo moja maalumu.m(uk199).

7. ukweli ni gharama na kila ukweli muna gharama zake. Khajat alibakwa, lakini anapotaka kuanza kulipiza kisasi ndipo ukweli uko bayana kwamba kuna gharama zake kulipiza kisasi.

8. migogoro haimaliziwi kwa mtutu wa bunduki peke yake.

9. Nia ovu mara nyingi hushindwa mbele ya wema. Waovu hawaoni kingine zaidi ya uovu wao. Wenye nia njema huona vyote viwili; uovu na wema.

10;katika maisha kinachoshinda ni dhamira. Ukiwa na dhamira daima utafanikisha mengi, hutoogopa kikwazo, bali ukabiliana navyo. 

11. MBINU. Katika mbio za maisha tunahitaji mbinu za kufanikisha mambo. kanuni mojawapo maishani ni hii “Kama jasusi mambo mawili ni kipaumbele. Kuwa mbali na wapelelezi wa adui ama kuwa sehemu ya wapelelezi wa adui”(197). Katika maisha ni ama utekeleze ndoto zao au uziache zipotelee kondeni. Ni uchaguzi wako.

Mwisho bwana Jabir Omar Makame tafuta demu wa kibongo bhana, usituwakilishe ugenini… Lol 

--MARKUS MPANGALA

No comments:

Post a Comment

Maoni yako