Showing posts with label bagamoyo. Show all posts
Showing posts with label bagamoyo. Show all posts

February 10, 2018

‘LOCATION’ YA WANAMUZIKI WA BONGOFLEVA ASLAY NA NANDY


Unaupata wimbo unaobamba sana katika vituo vya redio, kwenye magari ya abiria, bodaboda na Bajaj wa “SUBAKHERI MPENZI” ulioimbwa na wanamuziki wawili; ASLAY na NANDY?

Sasa hii pikipiki niliyokaa ambayo inamuundo wa aina yake imetumika katika video ya huo wimbo, maana ina usukani kama gari na makorombwezo ya mfumo Wa gari. Cratch inakanyagwa kama ya gari. Subiri kile ambacho wenye maeno yao wanavyosema pale inapotokea msanii anafanya video ya wimbo au kazi nyingine ya Sanaa kama filamu wao wanavyojisikia na namna gani wananufaika kupitia Location za hizo video zinazochukuliwa.

 Honorius Mpangala,

Matimbwa, Bagamoyo

September 26, 2010

USIPITWE; MAONYESHO YA KIMATAIFA BAGAMOYO SEPTEMBA 27-KESHO

Nimetua kwenye mji huu. na sitanii hali naona pilikapilika zinaongezeaka sana. Lakini ni za kwaida tu. Kwahiyo wewe unapenda sanaa? Unangoja nini sasa mambo yanakujia kesho kuna watu wengi hapa ambao wanazo dalili za kuwa wamekuja kama mzee wa lundunyasa kushadadia utmaduni wa mtu mweusi na kujua tamaduni za wale jamaa zangu wenye ngozi inayobadilika badilika kila wanavyozidi kuzeeka wenyewe wanajiita wazungu..... mimi huwaita wasungu. Ni maonyesho ya 29 ya kimataifa kuhusu sanaa. yanafantika mji huu kwa mara nyingine.
Usipitwe karibuni jamani au vipi? Nimeingia nipo hapa kwa raha zangu. Kazi kwako