August 18, 2017

ZIWA NYASA LA NANE KWA UKUBWA DUNIANI

ZIWA Nyasa linapita katika mikoa ya Ruvuma,Njombe na Mbeya,likishika nafasi nane kwa ukubwa duniani ni ziwa la tatu kwa ukubwa katika Bara la Afrika,likiongoza kwa kuwa na fukwe bora na maji maangavu.Ziwa Nyasa limezungukwa na nchi tatu ambazo ni Tanzania,Malawi na MsumbIji.

Ziwa hilo lipo kwenye usawa wa meta 500 toka usawa wa bahari ambapo kina cha ziwa hilo ni karibu meta 750,urefu wake ni karibu kilometa 1000 , upana mkubwa ni kilometa 80 na upana mdogo ni kilometa 15.Kulingana na utafiti ambao ulifanywa katika ziwa hilo na Jumuiya ya nchi zilizo Kusini mwa Afrika(SADC) kwa kushirikiana na nchi ya Uingereza kati ya mwaka 1991 hadi 1994 na mwaka 1996 hadi 2000,ziwa hilo lina kiasi cha tani 165,000 za samaki.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako