February 23, 2018

KAMBALE SAMAKI WA AJABU KULIKO SAMAKI WOTE DUNIANI

NA JACOB MALIHOJA
 
NIMEFUATILIA kwa kina samaki wa aina tofauti wa ajabu kama vile Electrical El (Mwenye uwezo wa kuzalisha umeme hadi Volts 900 yaani mara nne ya umeme tunaoutumia majumbani), 

Ngisi mwenye uwezo wa kujibadili rangi kama kinyonga kulingana na mazingira anayokuwepo na mwenye nguvu kubwa za kung'ata kuliko nguvu za kung'ta za simba, au Nyangumi kwa ukubwa wake .. binafsi nampa namba moja Kambale baada ya kugundua ni samaki pengine yaweza kuwa kiumbe wa kwanza kuishi mahali kwa miezi au miaka bila kupata chakula.

Kambale ana uwezo wa kuishi kwenye udongo mkavu kwa miezi au miaka akisubiri maji. Katika moja ya tafiti kambale aliwekwa katikati ya tofaali la Udongo na kujengewa na baada ya miezi kadhaa mvua ziliponyesha na tofali kulowa kambale huyo alitoka na kuanza safari ya kutafuta maji yalipo.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako