Nikupe mchapo? Wanawake nao WAMO sijui ndiyo wanaume tumewajuza au la. Wenyewe wanasema hakuna wanaume waoaji siku hizi. Lakini ukiwauliza wanasema wanaume ni kama mbwa eti tunawinda sana akina dada duh!
Duh! huku wenyewe wakishikiria nadharia yao kuwa siku hizi lazima uwe na wanaume (wapenzi) wawili (nazungumzia wale wasio na ndoa). Mmoja wanampenda sana na wapili wanamgeuza machimbo ya Mwadui-Shinyanga. Wanamchimba dhahabu halafu yule wa kwanza ananufaika shauri mwanamke anampatia mavuno ya mwadui.
Eti! weee! Markus utanipeleka wapi wakati unafikiria maisha? Unajua wazee hawana noma yaani ukitaka mkwanja wanakata tu, si unamuona yule nanii alikuwa anataka kununua gari?.....nikajibu namfahamu.... ' sasa sikiliza kile kibabu pale kilikuwa kikimtaka... akamweleza mbona mwenzangu una gari nami nataka lakini nina hela kidogo niongezee basi?
Duuh! kile kibabu kikasema nitakupa milioni tano na hizo 15 tafuta mwenyewe.
Aisee! basi yule dada alikuwa na mpenzi wake akampa habari ya kununua gari, jamaa anazo bwana akamwongezea milioni 5. Unaona? lakini nakwambia kile kibabu kimesotea 'kupata' tena 'kikapewa' siku moja tu, si unajua anaye mtu wake? kwahiyo inabidi kuwa na wawili ili mambo yakae sawa!
Wee mngoni, mmm tena mnyasa utanipeleka wapi wewe? acha bwana tafuta maisha Markus usihangaike nasi, wazia maisha kakangu eeeehee! Siku hizi wanawake tunao wapenzi wawili wawili ili kuweka 'mambo sawa', maana maisha yenyewe haya mmmm, utawehuka achana na soga zetu nenda ukasoma magazeti na vitabu vyako sivipendi kabisa halafu wewe mwanaume muda wote vitabu, ungekuwa 'wangu' nakwambia 'utapata' hivyo vitabu na magazeti nyooo lionee ha ha ha ha ha ha ha ha.
Mnyasa nikasema! Eee wala waungwana kumbe wanawake wamo! hamuogopi ukimwi ninyi? eeeeh kwaheri waungwana
sijui niseme nini. naamua kuufyata kwani wahenga wanadai eti listening is better than talking vinginevyo mungu asingetupatia masikio mawili na ka-mdommo kamoja tu tena kanakopaswa kunuka kwa ukimwa. let me stay kwayati.
ReplyDeleteunaogopa nini wewe mkuu
ReplyDeletenaogopa woga wenyewe. nisije kataliwa, si unajua namimi napenda kupendwa ili nipende!
ReplyDeletekaka Mpangala wanawake tupo hata kwenye kublog, tunawakilisha.
ReplyDelete