October 15, 2008

malaya/umalaya+uzinzi/mzinzi+uasherati/msherati/chupi mkononi/kahaba/ukahaba=UKIMWI?

Jamani hii ni kampeni ya ONE LOVE, huku ndiko unaambiwa subiri/tosheka naye/acha ngono/umalaya/uzinzi/uasherati. yaani weka neno lolote lenye maana ya jamaa anapenda ngono. kampeni ya kuwaweka sawa vijana kwamba UKIMWI unaua au kuwa waaminifu(?) sijui nini na mengine kibao, lakini mnajua kwamba kondomu zipo? mnafanyaje pale mnapokula raha zenu nyie watu? mimi sijui sababu sijui lakini najua kuna watu akina chupi mkononi n.k aiseh mambo juu ya mambo.unapomwambia binti wa miaka 16 kwamba awe mwaminifu.atosheke naye/awe na subira hivi mna maana gani? semeni huo ukimwi ni kuonjana/kutakana/kubanjuka/kubanjuana/utamu/kunoga/asali/uroda? eeeeh kama hujui kufa angalia kaburi. Simama uhesabiwe vinginevyo kaa chini usahauliwe.ONE LOVE

7 comments:

 1. ilikuwa viwanja vya mnazi mmoja pale kongamano la kuhimiza vijana kupiga vita ukimwi ONE LOVE

  ReplyDelete
 2. Ni kweli jamani tujitahidi mambo kwa soksi bila hivyo tunayatazama makaburi. Au pia dawa ni kumpokea YESU.

  ReplyDelete
 3. hapana dawa yake siyo yesu, unatakiwa kuijua akili yako kabla hujafanya hivyo.

  ReplyDelete
 4. KONDOMU KONDOMU NI NINI? unaweza kula pipi ikiwa ndani ya ganda? mm inakufikirisha kidogo? unadhani kwanini nasema kuhusu pipi? unaijali afya yako? lakini mahaba ni raha eti.......

  ReplyDelete
 5. pipi: ukisha onja pipi ni sawa kabisa na kufanya mapenzi ukishaonja bila kuvaa soksi basi tena

  ReplyDelete
 6. utamu unapatikana vipi kama unakula na ganda? mwenga utamu utajuaje kama unakula halau umefunika ganda

  ReplyDelete
 7. basi kama kwako suala ni utamu,tafuta wako mmoja mpime na uhakikishe mnaaminiana ili uu enjoy huo utamu unaopigania vinginezo ushauri wa bure jikinge.vijana mnahitajika sana katika jamii

  ReplyDelete

Maoni yako