October 08, 2008

maswali magumu

Mwanablogu Yasinta Ngonyani aliandika kuhusu yeye katika blogu yake. Ilikuwa Agosti 23, 2008 kwamba udadisi kwake ni sehemu ya maisha, akaongeza kwamba katika hali hiyo amejikuta amepoteza baadhi ya marafiki hasa wale wasiopenda maswali yake yaani walikuwa wakikerwa na maswali yake. Mimi sijui walikerwa kwasababu gani, wao wanajua. Sasa mimi namfahamu kiasi dadangu Yasinta, jamani hapo ni kiboko ya maswali yaani jamaa anauliza maswali mpaka unaona hee huyu vipi? Ukweli mmoja ya waathirika ya maswali yake ni Mnyasa hapa lakini kawaida ya Mnyasa ni uvumilivu na utulivu ndiyo uliobaini kwamba uulizwaji kwake maswali ni njia yake ya uwasilishwaji wa urafiki tofauti na wengine walivyokuwa wakidhani. Jamani dadangu anamaswali mpaka unaweza kuungua utadhaniumeunguzwa na moto. Sasa huwa najiuliza vipi mjomba wangu Erik na Camilla watakuwaje? nikajikuta nimegota,nimeishiwa maneno ya kuwatabilia. Lakini maswali yake yanakufanya muda wote uwe unafanya kazi ya kujibu na usipojibu heee umemkimbia au la. Jamani mimi nilivumilia na nimekubali kwamba kama alivyoandika ni kawaida yake kwahiyo naona poa tu. Habari ndiyo hiyo, kublogu/kuandika unachopenda

16 comments:

  1. Maswali kitu kizuri ingawa siku nyingine unaweza kujikuta hutaki kujua jibu.

    ReplyDelete
  2. nakubali mimi ni mimi hivyo ndivyo nilivyo na nimezaliwa hivyo. Nategemea kupunguza kidogo ili marafiki wasinikimbie kwani napenda sana vyote kwa hiyo hapa iko kazi kweli udadisi au marafiki.

    ReplyDelete
  3. naona safi tu. Lakini kaka Simon Dada Yasinta ni kiboko kama Sacrotes yule mwanafalsafa wa ugiriki aliyewasha kurunzi/tochi mchana huku jua likiwaka tena likuwa sokono halafu watu wakamwambia mzee kulikoni? wakadhani mjinga kumbe jamaa alikuwa katika utafiti kwamba wapo watu waliopo gizani. unajua niliamua kuandika baada ya kusoma tena kisa chake na kwavile nawaliana naye kila siku nikaona nimchokoze tena. Maswli ni mazuri na naamini ndivyo alivyo na mimi napenda hivyo lakini kuna watu ukiwadadisi tu wanasema udaku yaani bongo sijui tupoje jamani sikutkani ila nasema kweli. Bravo Yasinta Ngonyani endeleza fani bila hivyo hatuwezi kujua mambo/jambo

    ReplyDelete
  4. Huyu Yasinta Ngonyani ni dadako kweli au vipi na ni maswali gani hayo anayokuuliza mpaka usipojibu inakuwa taabu. Na kuhusu haw wajomba zako si unawaona kwa hiyo lazima utajua kama wapo kama mamayao.

    ReplyDelete
  5. Markus huyu Yasinta Ngonyani mbona unamwandika sana ktk blog yako? mara umwombe msamaha, sasa unasema ni mdadisi sana inaonekana unamfahamu sana.

    ReplyDelete
  6. sawa bwana asiyejulikana lakini nikwambie nashkuru kwa maoni yako. Nitakujibu hivi JE UNAWEZA KULIZIBA JUA KWA BAKULI? naona umenisoma sasa. kwamba jawabu ni la kifalsafa.

    ReplyDelete
  7. sijakuelewa

    ReplyDelete
  8. hujaelewa nini wewe wakati jibu umekwisha kupewa na mhusika? soma tena na tena na tena

    ReplyDelete
  9. Oh samahani sana naona umekasiika kama hivyo sitatoa tena maoni.

    ReplyDelete
  10. kwanini unahukumu hivyo kwa kipimo usichokijua? nami nikuhukumu kwa hilo?

    ReplyDelete
  11. ooh kumbe ulikuwa wewe wenye blog sasa nimekukamata

    ReplyDelete
  12. hola hiyo kwani vipi hujaona mamantile wa kizungu? nyoka kupaka wanja je? bado? we bado mudogo mudogo sana

    ReplyDelete
  13. nilidhani huyo alikuwa dada yako? kumbe ni mama yako sasa jamani ha ha hahaaaaaa

    ReplyDelete
  14. ebo! JAMANI NIITEJE SASA. kumbe mnapenda vyeo hata ambavyo hawezi kuvikwa navyo? mtakufa mnajitazama na hao wafadhili wenu wa ughaibuni

    ReplyDelete

Maoni yako