October 08, 2008
Labda leteni huku nyasa
sijaomba picha hii, lakini poa tu. Kuna jamaa walevi wanapenda sana hivi vitu. wengine wakunywa eti kupoteza mawazo. ebo nani kakwambieni mawazo yanapotezwa? mnajidanganya,mkipoteza mtapata wapi mengine. ndiyo nimechukua hapo bloguni Ruhuwiko kwa wanywa ulanzi na chimpunu(natania). jamani ukitaka kuwa na urafiki bora nami ni vema ukatofautisha haya makopo na nami. kama unasema unataka kupiga gumzo nami hakikisha pembeni hakuna makopo kama hayo. hata kama iwe mnasema 'mtoko' au 'matembezini' nakwambia nakuachia mtoko wako ukiniletea hayo makopo kama vipi kunywa kwa muda wako kisha harufu yako usilete kwangu au vipi waungwana. Unajua nini hapa nyasa hakuna, kwahiyo washamba tumekuwa wengi nasikia ukinywa tu unakufa. Kuna daktari mmoja alipogundua kwamba nina damu nyingi aliniuliza eti kama nakunywa pombe nusura nimzabe kibao, nikamwambia akome na akomae au vipi. karibuni nyasa lakini ONYO usije na hayo makopo ni haramu
Madhumuni
kumbukumbu,
Nyasa,
soga,
ughaibuni,
urafiki
WASIFU: Mwandishi wa Habari,Tawasifu,Mhariri na Mchambuzi wa Vitabu,Siasa, Utamaduni, Michezo,Afrika, Kimataifa,Mshauri wa Habari na Mikakati. TUWASILIANE: mawazoni15@gmail.com, lundunyasa@yahoo.com. WHATSAPP; +255 719226293/SMS; +255 764 936655
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Wala usinidanganye kabisa rafiki yangu nimezaliwa nyasa.
ReplyDeleteSi unajua na wangoni kwa ugimbi ndo wenyewe.
nilijua lazima utatetea sisi wangoni na ugimbi poa lakini naomba usilewe ukilewa uanjiju
ReplyDeletesijui maana ya kulewa nini na usiwe na wasiwasi ninywa he. ha ha ha
ReplyDeletesitaki habari za hulewi wala nini yaani hiyo harufu zako za ulanzi hukohuko hata hayao makopo siyapendi lakini napenda kodi wanayolipa au vipi
ReplyDelete