NA MARKUS MPANGALA
MAELFU ya vijana waliotokea
Wilaya ya Nyasa mkoa wa Ruvuma wamesoma elimu ya Sekondari katika shule ya Lundo iliyopo Kata ya Lipingo
wilayani humo. Hata hivyo sio vijana wote wamepata elimu ya sekondari ndani ya
Wilaya ya Nyasa au shule hiyo pekee, lakini idadi kubwa wamesoma hapo. Katika
kipindi cha miaka 2000 kumekuwa na ongezeko la shule za sekondari, ambapo
nyingi sasa hivi ni za Kata tofauti na awali.
Miongoni mwao ni ALPHONCE
KWENDE ambaye ni mwanazuoni wa masuala ya Kilimo hapa nchini. Yeye ni mzaliwa wa kijiji cha Chinula, tukiwa
tumehitimu pamoja shuleni. Amejikita katika fani ya Kilimo na anaitazama wilaya Nyasa ikiwa na uwezo wa kujenga Kiwanda
pamoja na watu kubadilika kuwa na mawazo ya kibiashara kupitia kilimo.
SOMA
MAHOJIANO KAMILI…..
SWALI: Habari za mchana mtumishi. Hebu tueleze baada
ya elimu ya Sekondari Lundo ulichaguwa kwenda shule gani?
ALPHONCE KWENDE: Yes,
nilijiunga na Kibiti High School, iliyopo mkoani Pwani kusoma masomo ya kidato
cha tano na sita.
![]() |
Mwanazuoni KWENDE akiwa kwenye shughuli za Kilimo. |
SWALI: Umewahi kujiunga na Chuo
chochote baada ya kuhitimua ‘High School’?
KWENDE: Sikujiunga na Chuo
Kikuu kingine zaidi ya SUA. Hiki ni Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, kipo
mkoani Morogoro. Hapo ndipo nilihitimu Shahada yangu ya Kilimo kwa ujumla wake.
SWALI: Aaah! Ndiyo maana kilimo
kimekushika sana? Nadhani ni msingi wa Lundo katika somo hilo. Nililipenda sana
ila likafutwa.
KWENDE: Ni kweli kabisa. Kabisa,
Lundo walitengeneza msingi mzuri sana kwenye somo la Kilimo, ndiyo matunda yake
niliyonayo sasa. Nilimalizana na elimua ye sekondari ya juu High School, mwaka 2004. Kisha mwaka 2009
nilifanikiwa kuhitimu shahada yangu ya Kilimo pale SUA.
SWALI: Tutajie mambo muhimu
ambayo unadhani yanaweza kuipaisha Wilaya ya Nyasa kiuchumi, Afya na Mengine.
KWENDE: Kujibu hilo inatakiwa
akili iwe imetulia kidogo. Mimi ningependa sana kuzungumzia sekta yangu ya
Kilimo na Ufugaji. Ujio wa Wilaya ya Nyasa unaibua hitaji kubwa sana la kuanza
kufanya kilimo chenye tija na cha kibiashara maana mpaka sasa bado wilaya ya
Nyasa inategemea Muhogo kama zao kwa chakula na biashara. Ingawaje jitihada
zinaendelea kufanyika kuendeleza uzalishaji wa zao hilo ili lilete kipato cha kutosha
kwa wakulima hao. Ujio wa Wilaya mpya unakuja na ujenzi wa Mahoteli ambako
hakuna uzalishaji wa kutosha mpaka sasa wa mazao ya bustani ya uhakika kukidhi
hitaji hilo hivyo kutakuwa na uhitaji wa mboga hizo na matunda kama Mananasi,Parachichi,Matango,Matikiti
maji na kadhalika.
Mojawapo ya Hoteli iliyopo wilaya ya Nyasa. |
SWALI: Bwana Kwende hapa
unatudhihirishia kuwa fursa hii inawahitaji waliosomea fani ya Horticulture
(kilimo cha mboga mboga na matunda), kwamba wanahitajika sana Nyasa?