Showing posts with label Mtwara. Show all posts
Showing posts with label Mtwara. Show all posts
February 23, 2018
AFYA: WATANI ZETU WANA NACHINGWEA, SHIRIKINI KATIKA ZOEZI LA MATIBABU YA WATOTO WENYE VICHWA VIKUBWA
January 01, 2018
SALAM ZA MWAKA MPYA 2018; KOROSHO MTWARA
NA
GABRIEL MWANG’ONDA
KAMA
ilivyo kwenye korosho kule Mtwara, basi kwa wale wahenga wenzangu wa mji wa Tukuyu
mtakuwa mnajua zile karanga za mitini kwa watu wa mjini na sehemu zinginezo
wanaweza kudhani nadanganya, lakini la hasha ni kweli kuna karanga humea mitini
na ni miti mikubwa kabisa, kwa kinyakyusa zinaitwa (Macadamia). Hizi zina vinasaba
vya korosho kwa mbali, ni very delicious and healthy vilevile.
Wakati
bei ya korosho ikipanda mpaka kufikia elfu nne kwa kilo kule Nangwanda Sijaona kunako Mtwara, watani wetu wa jadi hapo Kenya
wameamua kuachana na mashamba ya Chai na kukazania kilimo cha Karanga za mtini
ambazo zimefikia kilo moja Tshs 21,000.00 nakuendelea.
January 23, 2013
SAKATA LA GESI LIMEZUA JIPYA MKOANI MTWARA-Mgodi Unaotembea
![]() |
| Kambi Mbwana |
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
HALI ya mkoani Mtwara ni dhahiri inatishia amani, hivyo kuna
kila sababu ya serikali na wadau wote kukaa na kuliangalia suala hilo kwa
marefu. Nikiwa kama Mtanzania, nimekuwa nikifuatilia kwa karibu mno
sakata hilo la gesi inayopingwa na wadau kuletwa jijini Dar es Salaam, badala
yake wanataka ibaki mkoani Mtwara, ingawa wenye akili ndogo wanapinga au
kutukashifu kadri ya uwezo wao, wakijidanganya kuwa sipaswi kufuatilia mambo ya
Mtwara na Lindi.
Huu ni udhaifu na hauwezi kuchekewa, maana ni dhahiri
Mtwara, Lindi ni sehemu ya Tanzania kama ilivyokuwa Tanga, Arusha, Kilimanjaro
na kwingineko. Wananchi hao waliojikusanya kwa ajili ya kupigania sakata
hilo, wamefikia kubadilisha kabisa hisia zao, bila woga wowote katika kulizungumzia
suala la gesi.
Kama nilivyowahi kuhoji hapo nyuma, kuwa tatizo ni gesi,
choyo, siasa au ubaguzi? Makala haya yalitoka katika blog hii ya Handeni Kwetu
na kupokea maoni mbalimbali. Na haya ndio maoni ya Watanzania hao wanaoishi mkoani Lindi
na Mtwara. Mwanzo wa ugaidi Tanzania ni mwisho wa amani. Kusini
hawaogopi jeshi. Kauli ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete ipo kwenye mioyo yao. Leo
nasema, ila wana Mtwara watasema kwa sauti zao, maana vitisho kwao ni kama
kuitukana maiti.
Chochote kitatokea iwe ni vita vyovyote vile 2015 hatutaki
uchaguzi na hatutaki pia tuletewe kiongozi na ole wenu, +255712897794
![]() |
| Maandamano Mtwara |
Kaka nimefurahishwa na makala yako isemayo Tatizo ni ni
gesi, siasa, choyo au ubaguzi? Inaonekana na wewe pia umeandika makala hii kwa
lengo lako binafsi. Umeshindwa kutoa uhalisia wa jambo lenyewe, badala yake
umeandika kwa lengo la kutaka kumfurahisha ama kuwafurahisha watu fulani. Rudi nyuma angalia wanachofanyiwa wakulima wa korosho wa
Mtwara je ni sahihi? Lile zao halisaidii kuinua pato la Taifa? Angalia hali ya
maisha ya wakazi wa Mtwara. Nadhani umekurupuka na si mawazo yako kuna mkono wa
mtu nyuma yako.
Nenda kazunguuke na kufanya utafiti wa kina utapata majibu
sahihi kwa wenyeji. +255657614354.
Tatizo la mikoa
ya Kusini sio gesi bali ni kusahauliwa kwa miaka 51 ya Uhuru. Korosho, reli,
Bandari, miundo mbinu, tatizo la elimu na kuwa waanga wa ukombozi wa nchi
zilizopo kusini mwa Afrika.
Wanasiasa kujiingiza katika hoja si ajabu kwasababu duniani
kote wanasiasa ndio huibua matatizo ya wananchi , maana wasomi wetu wengi
hawana meno ya na ndio wanaopitisha
mikataba mibovu .
Sio choyo, lakini tunafikia wakati tunajuta kwa nini sisi
Mtwara Lindi tumekuwa sehemu ya Tanzania. Tuna rasilimali tosha za kuweza
kuitwa, kama vile Bandari, Bahari, Ardhi yenye rutuba, watu, mito, madini,
korosho, ufuta, mhogo na nyinginezo. Kusini tuna haki ya kumdai mume wetu Tanzania haki zetu za
msingi, maana tumevumilia mno hadi kilio cha kwi kwi. Ni mimi
mwanaharakati, Amoni, wa Kata
Msangamkuu, Mtwara Vijijini. +255652221100.
Ninaomba uelewe lengo la wananchi wa Mtwara na Lindi sio
kwamba hawataki gesi isitumiwe na wengine hapana, wao wanataka kiwanda
kitengenezwe Mtwara. Kule itoke gesi safi, maana wanakataa mambo yasijekuwa kama
ya madini ya Geita ambayo mwekezaji anachimba anaenda kuhakiki Mwanza na kulipa
kodi ya uwongo na kuiibia nchi na kuwa masikini, huku wakifaidi watu kutoka
nje.
Nimesoma makala yako, inayosema tatizo ni gesi, siasa, choyo
au ubaguzi? Mimi nimeisoma na kwa utafiti wangu, nimegundua kwamba wewe ni CCM
na ndio maana ukaona eti ni siasa. Hapana, ni kwasababu vyama vya upinzani
vinapenda maendeleo ya Watanzania.
Mbona hawakuhamisha miwa kutoka Kagera na kuileta Dar es
Salaam ili itengenezwe hapa? Pili, hebu fikiria gharama za kuweka bomba ni
kiasi gani? Tatu, kumbuka msongamano mkubwa wa watu, ina maana
wakiongeza viwanda wanazidisha msongamano. Nne, kwanini wasiwaachie watu wa
Mtwara na Lindi na wao wapate ajira? Tano, kila kilichokuwapo Dar es Salaam, Mtwara kipo kama
vile Bandari na mengineyo. +255713221244.
Ingawa hujaonyesha wazi ujumbe unaopeleka kwa wana Mtwara,
lakini ninachofahamu, Taifa halina rasilimali. Mikoa, wilaya, vijiji, ndivyo
vyenye rasilimali, kama vile mbuga za wanyama, madini, mazao na mengineyo
ambayo mapato yake hukusanywa na kuwa pato la Taifa. Gesi ni kama rasilimali nyingine tu. Ikiwa Mtwara, Lindi,
Kigoma, Mbeya au popote nchini, tueleze ni vipi italinyima Taifa letu pato? Au
italigawa vipi Taifa? +255717757797.
Hongera bwana Kambi Mbwana kwa makala yako. Endelea kuwapa
elimu Watanzania wenzetu wasioelewa. Naitwa Moi, +255757295249.
Unajua sisi tunaotoka Mtwara tunafananishwa na nyani katika
Taifa hili. Hatuna thamani mbele ya makabila mengine toka Uhuru. Barabara haijaisha, mazao yetu hayana usimamizi na hatuna
huduma za jamii zilizo bora. Tukipata wakarimu, sio bora pamoja na watumishi
wote. Sisi ni jamii ya mwisho katika Taifa hili, hujiulizi gesi na
mafuta aliyotupatia Mwenyezimungu ingekuwa sehemu nyingine ingehamishwa? Kwakuwa sisi nyani, hatuna thamani, gesi itaondoka na mafuta
pia yataondoka, maana hawa hawatatuthamini milele. +255712848839.
Asante kwa makala yako, lakini usiwe mwandishi mwoga
anayeogopa watawala walioshindwa kuwaondolea wananchi umasikini na kuligawa
Taifa, kati ya wenye nacho na wasiokuwa nacho. Jitahidi kuwa mkweli ili upate
mafanikio maishani mwako. +255755045295. Kijana mbona unakuwa kama popo asiyejulikana kama ni mnyama
au ndege. Ya Handeni Kwenu yamekushinda sasa umehamia kwenye gesi.
Nasikitika ujumbe huu uliotumwa kwa namba +255757602075. nimeufipisha
kwa sababu za kimaadili, maana ulijaa matusi na kashfa kutoka kwa mtumaji,
ambaye pia hakujitambulisha jina lake. Kaka nimesoma makala zako nyingi, nimegundua wewe ni kada wa
CCM na usiyejua nini wanachokitaka Watanzania. Hata hujui huko
vijijini watu wanaishi vipi. Unaogopa ya Daudi Mwangosi na Amina Chifupa na huo
sio uzalendo, hivyo hupaswi kuwa mwandishi.
Hivi unajua CCM wanaiendashaje nchi hii? Umeshahoji wananchi
wangapi kuhusu maisha yao badala yake unamfuata Nape Nnauye, unataka CCM ndio waiongoze
nchi milele na milele kwakuwa wewe si mzalendo. Ujumbe huu ulitoka kwa namba
+255652273836. Nashukuru brother kwa kuweza kupata fursa ya kuweza kusoma
makala yako.
Ni kweli hoja zako ulizozisema zinaweza kushabihiana na
ukweli, ila kutokana na vile hali
ilivyo naweza (kudetermine ya words) nazo yanatokana na siasa pia. Hebu nambie kaka angu, umaskini uliopo katika mikoa ya
kusini, moja kwa moja tumekuwa maskini na hii ilikua nafasi pekee ya kuweza
kupata ahueni.
Hebu jamani isifike wakati tukawa tunaangalia swala hili
kijuu juu, hali ni mbya kusini hatuna pa kushikia, serikali ilibidi iangalie
gesi hii pia katika kutafuta namna ya kuikomboa miji hii ya kusini.
Ni wazi kuwa serikali imekua ikifurahia tu kupata neema hiyo
kuendesha mambo yao na si kusaidia kuondosha umaskini.
Nyinyi waandishi tunawategemea kutoa hoja za kusaidia
kuondokana na majanga ya kimaskini. Ujumbe huu ulitumwa kwa njia ya barua pepe
kutoka kwa Raya Juma, Nashkuru Haya ni baadhi ya maoni yaliyoingia mara baada ya kuandika
makala ile, huku watu wakiingia moia kwa moja katika hoja yangu ya siasa,
ubaguzi na choyo nilizokemea. Kwanini nasema siasa? Ukiangalia hapo, wapo waliotuma ujumbe
huo wakiwa na chukia serikali ya CCM. Hata hivyo, kuyaanika maoni yao si
kuwaletea matatizo, bali kusoma mawazo ya watu wa Mtwara.
Wao ndio wahusika. Ndio wenye kupigania suala la gesi, hivyo
inaweza kuwa njia muafaka ya kuepusha shari inayozidi kujengeka mioyoni mwa
Watanzania, hususan wale wanaoishi mkoani Lindi na Mtwara. Watu wamekuwa na mawazo tofauti juu ya sakata hilo. Wapo
wale wanaofikia kutamani Mtwara iwe na utawala wake, jambo ambalo hakika si la
kuchekea.
Rasilimali za Tanzania zinaanza kutugawa kadri siku
zinavyozidi kwenda mbele, ndio maana nikaamua kuyaanika mawazo ya ndugu zetu
hao. Kwa kumalizia tu, sakata la gesi linaweza kujadiliwa upya
kwa kuwashirikisha wadau na wananchi wa Mtwara, hasa kwa kupewa mikakati ya
namna ya serikali kuwapelekea maendeleo maana ni wajibu wao.
Masuala ya chokochoko ya gesi yasiachwe tu kwa wanasiasa
ambao wamekuwa wabunifu kuingia kwenye hoja zinazoshirikisha watu kwa ajili ya
kujijenga kisiasa, jambo ambalo si zuri.
Na sisi tunaofikia kujadili suala la gesi, wakiwamo wana
harakati, wasitumie maneno makali, maana siku zote jazba inaondosha maana
husika. Maoni mengi ya Watanzania nimeshindwa kuyaandika kwa
kwasababu hayajatolewa kiungwana, huku niliyoaandika nikiyafanyia marekebisho
mengi mno.
Katika hili, serikali kwa kupitia Waziri wake wa Nishati na
Madini, Professa Sospeter Muhongo, anapaswa kukaa na kulijadili jambo hili kwa
mapana yake.
kambimbwana@yahoo.com
www.handenikwetu.blogspot.com
+255712053949
+255753806087
Madhumuni
Lindi,
Mgodi Unaotembea,
Mtwara,
siasa
January 15, 2013
MIKOA YA MTWARA,LINDI NA RUVUMA TAFUTENI SULUHU KUFELI MITIHANI
Na Hamisi Magendela , Dar es Salaam
SIKU chache zilizopita wananchi wa mikoa ya kusini waliandamana kupinga uchimbaji wa bomba la gesi kutoka huko kwenda Dar es Salaam ambacho ingetumika kwa ajili ya kuzalisha umeme.
wanafunzi wakiwa darasani katika moja ya shule za msingi wilayani Nyasa
Umeme huo ambao ungezalishwa jijini Dar es Salaam ungetumika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania hali ambayo inaaminika kuwa itasaidia kupungua ghalama za umeme na kufanya ukali wa maisha kupungua.
Sipingi mawazo yao kwani kila mmoja anafikilia kwa utashi wake japo ni vema wakaangalia faida kuliko na mafanikio yatakayopatika siku za usoni ikiwa gesi hiyo itasafilishwa kwa njia ya bomba kwenda Dar es Salaam.
Kikumbwa ambacho naweza kusema ni kwa wananchi wa mikoa ya kusini wanatatizo makubwa zaidi ya kuandamana kutaka manufaiko ya gesi wakati suala zima la elimu likiwa limewatupa mkono kiasi kwamba inatia simanzi kuona inashika nafasi 10 za mwisho katika ufauru wa matokeo ya kidato cha pili yalitangazwa juzi na Wizara ya Elimu na Mafunzo jijini Dar es Salaam jana.
Kikumbwa ambacho naweza kusema ni kwa wananchi wa mikoa ya kusini wanatatizo makubwa zaidi ya kuandamana kutaka manufaiko ya gesi wakati suala zima la elimu likiwa limewatupa mkono kiasi kwamba inatia simanzi kuona inashika nafasi 10 za mwisho katika ufauru wa matokeo ya kidato cha pili yalitangazwa juzi na Wizara ya Elimu na Mafunzo jijini Dar es Salaam jana.
Licha ya kuwa ni aibu kwa wananchi pamoja na viongozi wa mkoa huo lakini naweza kusema kuwa ni kashfa ambayo katika miaka 50 ya Uhuru ijayo inatakiwa kufanyiwa kazi ili kuhakikisha wanapata elimu ya kutosha na kuondoka na ujinga wa kukosa elimu.
Ingekuwa vema zaidi badala ya kulalamikia kuhusu gesi wangepiga kelele kwa kukosa elimu bora kwa wanachi wengi wa mikoa hiyo hali inawafanya kukosa nafasi nzuri katika viwanda vinavyojengwa katika mikoa.
Kwa maana nafasi nzuri ya ajira itakuwa ikishirikiliwa na wageni ambao wana elimu ya kutosha ya kukidhi mahitaji ya kazi inayohitajika kwa wakati huo na kufanya wenyeji kufanya kazi za hali ya chini kila siku.
Pia wananchi wa mikoa ya kusini umefikia wakati wa kusimama kidete kuhakikisha fursa iliyotangazwa na Serikali kuwa kuanzia sasa hakutakuwa na mwalimu atakaepangiwa kazi mijini kwa wanaotoka vyuoni.
Kwa maana hiyo ikiwa viongozi wa mikoa hiyo wakitumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi wa kuzingatia elimu badala ya kung'ang'ani masuala ambayo kwa sasa hayasaidii sana katika miaka 50 ijayo.
Kusudio hilo la Serikali kupeleka walimu vijini linatokana na malalamiko kutoka sehemu hizo kuwa zimesahaurika kielimu kutokana na kukosa walimu wa kutosha hali inayofanya mikoa hiyo kushikia mikia katika matokeo ya mwisho kama ilivyo sasa kwa mikoa ya kusini.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu ilisema lengo la kufanya hivyo ni kupata uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 10 hali itakayosaidia kunyanyua kiwango cha elimu katika mikoa iliyo pembezoni mwaka nchi.
Hivyo naamini fursa hiyo ikiwa itatumiwa vema na wananchi wa huko itafanya viwanda vinavyojengwa sasa katika mikoa hiyo wenyeji kunufaika kazi zaidi kuliko wageni ndio madhumuni makubwa ya baadhi ya wawekezaji.
Kwa maana wapo wanaotoa ahadi kuwa ikiwa viwanda vyao vitamalizika waajili wenyeji kwa asilimia zaidi ya 60, lakini ikiwa hali ya elimu itaendelea kuwa hivyo ni dhairi wageni watakuwa na nafasi kubwa kuliko wazawa.
Viongozi wa mikoa ya pembezoni mwa Tanzania ikiwemo ya kusini kazi kwenu kuhakikisha mnahamasisha wananchi wenu wanatumia fursa inayotolewa na Serikali kupeleka walimu vijijini inatumiwa vizuri na matunda yaonekana.
Pia kwa Serikali ni vema ikatambu kuwa si walimu pekee wanahitajika katika mikoa hiyo iliyo pembezoni mwa Tanzania bali vyenzo za kufundishi nazo ni muhimu, itakuwa haina maana kupeleka walimu bila ya vitendea kazi na kuwajengea miondo mbinu mingine ikiwemi malazi bora.
Kwani upo uhushuhuda kuwa walimu wengi wanakacha kwenda kufundisha vijini kutokana na kutopatiwa mahitaji muhimu ya kibinadamu ikiwemo usafiri, nyumba nzuri za kuishi na kuishi katika maboma.
Maoni: 0782839898
December 29, 2012
UTAJIRI WA GESI ASILIA: TUWASIKILIZE WATANZANIA WA MTWARA NA LINDI. TUSIWAPUUZE
Na Zitto Kabwe, Dar es Salaam
Maandamano ya amani yaliyofanyika mjini Mtwara siku ya
alhamis wiki hii yameibua hoja mbali mbali kutoka kwa viongozi, wananchi,
vyombo vya habari na mjadala wa siku nzima kwenye mitandao ya kijamii hasa
facebook, twitter na JamiiForums. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ameita waandamanaji
wapuuzi na Waziri wa Nishati na Madini amewaita watu hatari na wahaini. CHADEMA
tumetoa kauli kupitia kwa Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba udhaifu wa
utendaji serikalini ndio chanzo cha maandamano haya.
Lakini kuna tatizo kubwa zaidi ambalo linaonekana siyo
katika sekta hii tu bali pia katika sekta nyingine ambapo tunaona matokeo yake
katika maisha ya watu wetu na naweza kusema ni dalili za kushindikana kwa sera
za CCM. Sera hizi ndizo ambazo zimelifikisha taifa hili hadi hapa. Kama hadi
wananchi wa Mtwara ambako kwa muda mrefu imekuwa ni ngombe ya CCM wanaanza
kuhoji matokeo ya sera za chama tawala basi ni dalili kuwa Watanzania
wamefungua macho yao na wanaona.
Wanaona katika nishati, wanaona katika utawala bora, wanaona
katia elimu (kuanzia ya msingi hadi ya juu kabisa!), wanaona katika afya,
wanaona katika utendaji wa jeshi la polisi wanaona katika madini. Sera za CCM
zimeshindwa. Zimeshindwa kuinua maisha yao na zinaonekana kuendelea kushindwa.
Mtwara na Lindi wanataka nini?
Watu wa Mtwara wanataka gesi isiondoke Mtwara na badala yake
viwanda na mitambo ijengwe Mtwara kisha kama ni umeme au mbolea isafirishwe
kupelekwa sehemu nyingine ya nchi. Watu wa Mtwara hawasemi kwamba Gesi yote na
mazao yake vibaki Mtwara na Lindi. Wanasema umeme uzalishwe Mtwara usambazwe
nchi nzima. Mbolea izalishwe Mtwara na kusambazwa nchi nzima. Wanataka Bandari
ya Mtwara iboreshwe na kuhudumia mikoa ya Kusini. Watu wa Mtwara hawasemi
kwamba mapato yote ya Gesi yatumike Mtwara tu la hasha.
Sio dhambi hata kidogo kwa watu wa Mtwara kudai masuala
haya. Watu wa Mtwara wamefanya maandamano kwa amani kabisa bila kuharibu mali
na kutoa maoni yao. Kwanini tuwasute na kuwasusubika kwa madai yao haya? Kwa
nini tusiwasikilize? Kosa lao nini kudai viwanda ili wapate ajira? Tumesahau
kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara ni mikoa masikini kabisa nchini? Tumesahau kuwa
mikoa ya Lindi na Mtwara ilitumika kwa ukombozi wa kusini mwa Afrika kiasi cha
kuwa katika hatari kabisa?
Tumesahau ‘sacrifice’ ya watu wa Mtwara na Lindi
dhidi ya usalama wa nchi yetu? Tumesahau kuwa Korosho imekuwa zao kubwa la
biashara na linaloingiza mapato mengi sana ya Fedha za kigeni? Waziri Muhongo
anasema Mtwara warudishe Fedha za Mkonge na Kahawa. Mbona hataji fedha za
Korosho? Mwaka 2011 Korosho ilikuwa zao la pili kwa kuingiza fedha nyingi za
kigeni baada ya Tumbaku.
Lakini tujiulize, watu wa Mtwara na Lindi walifadi fedha za
Mkonge? Walifaidi fedha za Kahawa? Wamefaidi fedha zao za Korosho? Tumesahau
hata Reli iliyoachwa na Mkoloni ya Nachingwea – Mtwara iling’olewa na Serikali
huru ya Tanzania? Tujiulize zaidi, hivi watu wa Nzega wamefaidika vipi na
Mgodi wa Resolute pale Lusu? Mgodi umefungwa ukiwa umezalisha na kuuaza dhahabu
ya thamani ya dola za marekani 3.3 bilioni. Hivi katika uhai wa mgodi huu
Serikali Kuu imekusanya kodi kiasi gani? Halmashauri ya Wilaya ya Nzega imepata
ushuru kiasi gani? Watu wa Mtwara wanayaona haya yaliyotokea Nzega na
yanayotokea Tarime, Biharamulo, Kahama na Geita. Watu wa Mtwara wana Haki
kuandamana kuzuia haya yaliyotokea wenzao yasiwatokee wao kwenye Gesi asilia.

Mtwara na Lindi
wanakosea wapi?
Madai yao halali na mimi binafsi na chama changu tunayaunga
mkono. Lakini kuna mahala lazima waelimishwe. Watu wa Mtwara pia wanapaswa kuelewa kuwa juhudi zao
zisiwatenganishe na Watanzania wengine kwani bado utajiri wa Taifa unafadisha
kikundi cha Watanzania wachache sana. Watu wa Mtwara wanahitaji kuungana na
watu wa Mara, watu wa Mwanza, watu wa Shinyanga na watu wa Kagera kudai utajiri
wa nchi utumike kwa maendeleo ya watu badala ya kunufaisha kundi dogo la watu.
Watu wa Mtwara wanapaswa kuunganisha nguvu na Watanzania wengine kuzuia uporaji
wa rasilimali ya nchi dhidi ya kizazi kijacho. Watu wa Mtwara wasijitenge
wakawa peke yao na Gesi yao. Nguvu ya mnyonge ni umoja.
Serikali isiyosikia
Serikali ina hoja kuhusu kujenga Bomba la Gesi kwa ajili ya
kuzalisha umeme kwa gharama nafuu. Umeme unaotumiwa na asilimia 14 tu ya
Watanzania. Kwa kuwa hii asilimia 14 ndio wenye sauti basi watu wa Mtwara
wataonekana hawana hoja kabisa. Lakini Serikali imejiuliza mara mbilimbili
kuhusu mradi huu wa Bomba? Tunaambiwa na Wataalamu kwamba kuna uwezekano mkubwa
mwakani gesi asilia ya kiasi cha futi za ujazo trillioni 20 itakuwa
imegunduliwa katika Kitalu namba 7( block 7) ambacho kipo mkoani Dar es Salaam
katika Wilaya ya Temeke. Iwapo gesi nyingi hivi itakuwa hapa Dar karibu kabisa
na mitambo ya kuzalisha umeme, mradi huu wa Bomba unaojengwa kwa trillioni za
shilingi utakuwa na maana tena? Huu mkopo utakuwa na tija?
Serikali imewaambia watu wa Mtwara gharama za kuleta bomba
Dar dhidi ya gharama za kujenga mtambo wa kuzalisha umeme Mtwara na
kuusafirisha umeme kwenda maeneo mengine ya Tanzania? Serikali imeangalia faida
ya kujenga gridi nyingine badala ya kuwa na gridi moja tu yenye kushikwa na
bwawa la Mtera? Leo bwawa la Mtera lisipozalisha hata megawati moja hata Dar es
Salaam izalishe megawati alfu kumi umeme hautakuwapo maana uti wa mgongo wa
gridi ni Mtera! Kwa nini tusiwe na gridi nyingine yenye uti wa mgongo Lindi au
Mtwara?
Picha zote kwa hisani ya Said Msonga
Tuwasikilize watu wa
Mtwara
Watanzania sio mabwege tena. Kuwaita watu wa Mtwara ni
wahaini, wapuuzi au watu hatari haisaidii kujenga Taifa moja lenye watu huru.
Serikali na wadau wote wa sekta ya Gesi likiwemo Bunge washirikiane na watu wa
Mtwara kuhusu miradi ya gesi asilia. Tuwe na Azimio la Mtwara, tamko la
kuelekeza namna bora ya kutumia utajiri wetu wa Gesi bila kuathiri umoja wa
Taifa letu.
Ujio wa Sera, Maono
na Uongozi Mbadala
Sasa hivi wananchi wa Mtwara kama wananchi wa sehemu
nyingine wanahitaji maono mbadala, uongozi mbadala, sera mbadala na mwelekeo
mbadala wa kitaifa ambao utaangalia mahitaji yao, utazingatia raslimali
zilizopo na utaunganisha utendaji wa sekta mbalimbali katika kutengeneza mfumo
wa kiutawala na kiuchumi ambao utaliinua taifa zima.
Ni kwa sababu hiyo naamini chama changu ni jibu sahihi kwa
matamanio na kiu ya wananchi wa Mtwara na sehemu nyingine nchini. Ikumbukwe
kuwa katika Ilani yetu ya Uchaguzi ya 2010 tulielewa haja ya kuangalia mikoa
hii ya Kusini kwa namna ya pekee na kuipa mwelekeo wa kipekee katika sera. Bado tuna makusudio hayo tunapoelekea
2015 na tukishika Dola wananchi wa Mtwara na sehemu nyingine zote zilizoachwa
pembezoni mwa mafanikio wajue kuwa wamepata rafiki na mshirika wa karibu wa
kushirikiana nao kuleta maendeleo.
Siyo katika suala la gesi tu bali katika nishati, maji,
elimu, miundombinu, kilimo, ufugaji, uvuvi, utalii. Mtwara kama ilivyo mikoa
mingine ina raslimali za kutosha kuweza kuwainua wananchi wake kimaisha, na
zaidi ya yote kutoa mchango mkubwa wa kiuchumi. Hili ambalo ni kweli kwa Mtwara
ni kweli kwa mikoa mingine kama Kigoma, Manyara, Katavi, Lindi n.k.
NB: ZITTO KABWE ni mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chadema.
NB: ZITTO KABWE ni mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chadema.
Subscribe to:
Posts (Atom)








