NA
GABRIEL MWANG’ONDA
KAMA
ilivyo kwenye korosho kule Mtwara, basi kwa wale wahenga wenzangu wa mji wa Tukuyu
mtakuwa mnajua zile karanga za mitini kwa watu wa mjini na sehemu zinginezo
wanaweza kudhani nadanganya, lakini la hasha ni kweli kuna karanga humea mitini
na ni miti mikubwa kabisa, kwa kinyakyusa zinaitwa (Macadamia). Hizi zina vinasaba
vya korosho kwa mbali, ni very delicious and healthy vilevile.
Wakati
bei ya korosho ikipanda mpaka kufikia elfu nne kwa kilo kule Nangwanda Sijaona kunako Mtwara, watani wetu wa jadi hapo Kenya
wameamua kuachana na mashamba ya Chai na kukazania kilimo cha Karanga za mtini
ambazo zimefikia kilo moja Tshs 21,000.00 nakuendelea.
Hapa
nchini sijui kama kuna sehemu nyingine zaidi ya Tukuyu ambako macadamia
zinalimwa na baadhi ya sehemu mkoa wa Mbeya, nimewahi kuziona Mbozi pia. Hizi
karanga kama ukiweza kuzi process unaweza kuziuza kilo moja kwa $40 yes ndio
hivyo, utajiri unachezewa.
Our
research institutes zinaweza kulifanyia kazi hili zao ili tuweza kujua kama
tunaweza kuli scale na kulifanya la kibiashara zaidi, hapo zamani sie wakulima
tulikuwa tunalitumia kucheza michezo yetu ya kitoto, nakumbuka tukiwa watoto
tulikuwa tukizinunua na kuzichezea then tunakula baadae sana, wazee wetu
wanahangaika sana na chai labda hili zao linaweza kuwa mwarobaini wa ugumu wa
zao la chai.
2018
mwaka wa mabadiliko, karanga za mtini zaweza kuwa mbadala muafaka kabisa wa
chanzo cha mapato yetu. Rais wa benki ya maendeleo ya Africa kaamua kulivalia
njuga swala kilimo ni muhimu kwenda hii vision ya Afrika pamoja, alinukuliwa
akisema asilimia 80% ya mabilionea hapo baadae watakaokuwa wakitokea Afrika
watakuwa wanajishughulisha na kilimo, Yes inawezakana Inaanza na wewe na mimi.
Happy
new year ndugu zanguni, muwe na mwaka wenye baraka tele.
@GM
No comments:
Post a Comment
Maoni yako