Showing posts with label uhai. Show all posts
Showing posts with label uhai. Show all posts

March 22, 2018

MRADI WA MITI KIJIJI CHA LUNDU


Mradi wa shamba la Miti la kijiji cha Lundu linalomilikiwa na Kanisa Katoliki Parokia ya Lundu na kufadhiliwa na Mfuko wa Misitu Tanzania.

March 05, 2018

MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU BUSTANI YA MUNGU- HIFADHI YA KITULO.

1.Hifadhi ya Taifa Kitulo ndiyo eneo pekee Tanzania lenye ndege aina ya tandawala machaka (Denhams Bustard) wenye uwezo wa kuruka kutoka bara moja hadi jingine.
2.Hifadhi hiyo inayopita katika mikoa ya Mbeya na Njombe ilitangazwa rasmi kuwa hifadhi ya Taifa mwaka 2005 ikijumuisha sehemu ya eneo la shamba la mifugo, msitu wa Livingstone na bonde la Numbi.
3.Kitulo ina ukubwa wa kilometa za mraba 442. Awali ilijulikana kama Elton Plateau baada ya Mvumbuzi Fredirick Elton kupita eneo hilo mwaka 1870. Mwaka 1960 Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) lilichukua eneo hilo kwa ajili ya ukulima wa ngano na ufugaji wa kondoo.
4. Ndege aina ya tandawili machaka hawapatikani sehemu nyingine yoyote hapa Tanzania zaidi ya Kitulo.
5.hifadhi hiyo ndiyo eneo pekee ambalo ndege hao hutaga mayai na kuzaliana kwa wingi kabla ya kusafiri kwenda mabara mengine.

October 16, 2017

CHUO CHAANZISHA SHAHADA YA WADUDU

NAIROBI, KENYA

KITUO cha Elimu na Utafiti kinachofadhiliwa na Benki ya Dunia kimeasisiwa katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jaramogo Oginga Odinga na kinasubiri ruhusa ya kuanzishwa kwa programu za Uzamifu na Uzamili kuhusu wadudu wanaoweza kuliwa.

Taasisi hiyo inapania kubuni njia za kuzalisha wadudu hao kwa wingi bila ya kuharibu mazingira ili kukidhi utashi mara baada ya wazo hilo likifanywa kuwa biashara.Wadudu wanaoliwa sana maeneo ya Magharibi mwa Kenya, ambao wana wingi wa madini ya protini na Zinki watafanywa kuwa biashara ili kuimarisha uwepo wa chakula cha kutosha, na kuondoa dhana mbaya katika kula wadudu. 

December 20, 2013

UTENGENEZAJI WA POMBE YA WANZUKI "VIPOROMBA" NYASA


Kwasasa pombe ya Wanzuki inazalishwa kwa wingi na akina mama pamoja na mabint wengi huku Nyasa. Vijana wanalewa asubuh asubuh kwa bei Rahisi sana. Pombe hii hutengenezwa kama Chai isipokuwa ongezeko la hamira.
ILA NAPATA MASHAKA NA NAMNA POMBE hiyo inavyotengenezwa kwani mazingira yake. Vitambaa vya kuchujia havifai na makopo yake hayaoshwi. SAWA NI AJIRA, ila sijui wewe Mnyasa mwenzangu una maoni gani?
Utengenezaji wa pombe aina ya Wanzuki

Pombe aina ya Wanzuki ikiwa imekamilika na kuwekwa ndani ya chupa

Pombe aina ya Wanzuki ikiwa tayari kuuzwa kwa wateja.