NAIROBI, KENYA
KITUO cha Elimu na Utafiti kinachofadhiliwa na Benki ya Dunia kimeasisiwa katika Chuo Kikuu cha
Sayansi na Teknolojia cha Jaramogo Oginga Odinga na kinasubiri ruhusa ya
kuanzishwa kwa programu za Uzamifu na Uzamili kuhusu wadudu wanaoweza kuliwa.
Taasisi hiyo inapania kubuni njia za kuzalisha wadudu hao
kwa wingi bila ya kuharibu mazingira ili kukidhi utashi mara baada ya wazo hilo
likifanywa kuwa biashara.Wadudu wanaoliwa sana maeneo ya Magharibi mwa Kenya, ambao
wana wingi wa madini ya protini na Zinki watafanywa kuwa biashara ili
kuimarisha uwepo wa chakula cha kutosha, na kuondoa dhana mbaya katika kula
wadudu.
“Kwa muda mrefu, Senene, kumbikumbi na panzi wamekuwa
wakiliwa sana Magharibi mwa Kenya na wana madini mengi ya protini na zinc.
Lakini imani potofu kuwahusu umuhimu wao, imefanya ulaji wa wadudu hawa
kupungua na ndio maana kituo hiki ni muhimu sana,” alisema Naibu Mkuu wa Chuo
Hicho Stephen Agong. Wadudu watakaoshughulikiwa mno ni pamoja na Senene,
kumbikumbi na panzi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa chakula kutoka kwa wadudu,
mpango huo unatazamiwa kuanza kufanyiwa kazi katika kipindi cha miezi michache
ijayo na taasisi hiyo itakuwa na uwezo wa kuwapa mafunzo wanafunzi 20 wa
Uzamivu (PHD) na 60 wa Uzamili ambao 35% watatoka Kenya.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako