October 16, 2017

“RAIS ANA MIAKA 31”


Sebastian Kurz
JUMAMOSI nilikuwa nasoma makala ya James Masters kwenye tovuti ya CNN. Sentesi yake ya kwanza ilinivutia sana, “Ulikuwa unafanya nini ulipokuwa na umri wa miaka 31? Ingawa aliendelea na mengine lakini staili pekee haikuwa kivutio bali mtu aliyekuwa akizungumzwa alivutia zaidi.
James Masters alikuwa anamzungumzia Sebastian Kurz ambaye amewahi kuwa waziri wa  Ushirikiano wa Kimataigfa tangu mwaka 2013 akiwa na miaka 27.  Sebastian  Kurz ambaye amekuwa Kansela wa Austria mwenye umri mdogo zaidi kwani sasa hivi ana miaka 31 tu. 

Ni mwenyekiti wa chama cha  OVP. Sebastian kuanzia jana jumapili aanaongoza serikali ya Austria ( kama vile Rais hapa kwetu) baada ya chama chake kushinda viti vingi vya bunge. 


Hitimisho la James Masters lilipa somo, anasema kwa Austria wanamwona Sebastian kama kujibu mapigo ya Ufaransa wanaoongozwa na kijana Emmanuel Macron  mwenye miaka 39. Pia ni kujibu mapigo ya Canada wanaoongozwa na Justin Trudeau, mwenye umri wa miaka 45. 

Nami nionavyo, katika ulimwengu wetu huu mabadiliko ya uongozi yanazidi kuchukua nafasi kubwa zaidi. Kwahiyo suala la msingi ni uwezo wa uongozi si umri wa akina 'Sebastian Kurz". Afrika tuko dunia hii, hatutokwepa hayo. 

©Andunje wa Fikra

No comments:

Post a Comment

Maoni yako