NA
MARKUS MPANGALA
SWALI: Naam, shikamoo Mzee Macha?
SWALI: Naam, shikamoo Mzee Macha?
FREDDY
MACHA; Marahaba. Habari zako bwana! uko wapi wewe siku hizi? Maana tangu
tuliposalimiana pale Soma Café,Mikocheni na baadaye Nyumba ya Sanaa, Dar es
Salaam wakati wa warsha nilizoendesha huko.
SWALI;
Nipo hapa Bongo naendelea vema tu. Ni kweli, kitambo hatujawasiliana, pia
nilifaidika sana na warsha zako hata hivyo si neno, tutaongea kidogo leo.
![]() |
Freddy Macha |
FREDDY
MACHA; Asante. Nadhani leo unalo la kuongea zaidi. Karibu.
SWALI;
Ni kweli, nahitaji mengi kutoka kwako mzee wangu. Kiu yangu ni huu mradi wa
Kiswahili Society, kwani umeeleza mahala fulani nikasoma nami nimevutiwa ili
niwaarifu wasomaji. Je mradi huu ulianza lini na wapi?
FREDDY
MACHA; Umeanzishwa na wanafunzi na Wahadhiri wa Kiswahili pale chuo cha lugha
cha SOAS (School of Oriental and African Studies) hapa London,Uingereza.
SWALI:
Nini dhumuni la kuanzishwa kwa Kiswahili Society?
FREDDY
MACHA; Kuunganisha Wazungumzaji wa Kiswahili duniani lakini hasa hapa
Uingereza.
SWALI:
Nashukuru sana. Ndugu Macha, wewe ni Mwanamuziki,Mwanafasihi,na Mwandishi
mkongwe. Katika fani hizi kuna mambo mengi umejifunza kutoka bara letu la
Afrika,Latin Amerika,Marekani na sasa Ulaya. Unadhani jamii za watu wa Ulaya
hususani Uingereza zinaweza kuhamasika kukiendeleza Kiswahili?