Showing posts with label malezi. Show all posts
Showing posts with label malezi. Show all posts

November 20, 2017

KONGAMANO LA KUMBUKIZI YA FIDEL CASTRO


Jukwaa la Wajamaa Tanzania, Taasisi ya Usomaji na Maendeleo "Soma" na Rastafarai United Front wanashirikiana kuandaa kongamano la kumkumbuka El Commandante Fidel Castro siku ya Jumamosi, tarehe 25/11/2017. Mahala itakuwa kwenye ukumbi wa Soma Book Cafe; na muda ni saa 7 mchana hadi saa 12 jioni.
WOTE MNAKABISHWA. HAKUNA KIINGILIO!
"Mwambie Comrade amwambie Comrade"

October 21, 2017

TABASAMU NA KITABU


Ragin Mmbanga (kushoto) na Markus Mpangala (Kulia)
Huyu ni rafiki yangu. Anaitwa Ragin Mbaga, ila tuwapo farashani hupendelea kumwita "Mzee wa bustani ya usomaji". 

FUAMBAI SIA AHMADU: MWANAMKE ANAYETETEA UKEKETAJI AFRIKA.

Na KIZITO MPANGALA

FUNAMBAI SIA AHMADU alizaliwa mwaka 1969 nchini Sierra Leone katika jamii ya kabila la Kono kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Alifanya kazi na UNICEF nchini Gambia. Fuambai Sia Ahmadu alipata shahada ya uzamili katika chuo cha masuala ya Uchumi jijini London Uingereza akiwa kama mataalamu wa Anthropojia. Baadae aliendelea na masomo zaidi katika chuo kikuu cha Chicago na kupata shahada ya uazmivu.

Anafahamika zaidi kwa utetezi wake wa ukeketaji hasa akifikiria zaidi kutoka katika jamii ya kabila la Kono ambapo yeye mwenyewe amekeketwa na anafurahia jambo hilo. Anasema masuala mengi kuhusu ukeketaji hayajaeleweka kwa ufasaha miongoni mwa watu wengi duniani.   

October 17, 2017

MAONI YA MHARIRI: KWA WILAYA YA NYASA DUNIA HAIJABADILIKA?

Majuzi nimeona picha ya mwanadada mashuhuri katika mtandao wa Instagram, Mange Kimambi akionyesha majengo ya hospitali ya Lumeme wilayani Nyasa ikiwa na mazingira mabaya ya kufanyia kazi na ukosefu wa huduma muhumu. Pamoja na jengo lenyewe kutokamilika, lakini limekuwa likitumika hivyo hivyo.

Kwangu mimi ile ilikuwa habari kubwa sana kwa wilaya yetu ya Nyasa. Kama mwanahabari naamini kuripotiwa matukio au masuala yasiyofaa  ndani ya jamii ambayo haitoi habari za kutosha ni njia mojawapo kubwa ya kubadili mwenendo.

HAPA CHINI kuna Blogu ya JIMBO LA NYASA. Lakini habari za Jimbo husika ziliwekwa mara ya mwisho Januari mwaka huu. Nimejiuliza wasaidizi wa Mbunge wanafanya nini kama hawawezi kutoa taarifa za ofisi ya mbunge? Najiuliza hivi hatuoni umuhimu wa habari zetu zikiwa hadharani bila kujali mbaya au nzuri?

Je waanzilishi wa blogu ya JIMBO walikusudia tamasha au nini? BONYEZA HAPA KUTAZAMA.  Kimsingi habari za Jimbo la Nyasa ni lazima zitolewe wala kwa wananchi. Pili inadhihirisha "kuamini" kuwa NYASA ni ileile ambayo inaishi pasipo kuwa na habari zozote. Mtazamo huo si sahihi ndio maana wahusika wanaona "bora liende tu" huku wakisahau na kushindwa "KUMUUZA" mbunge. 

Nimejiuliza hadi leo hata kutengeneza ukurasa wa habari za mbunge kwenye mitandao hatuwezi kweli?  Hivi mahusiano ya mbunge na wapigakura wake yana maana gani? Naandika hapa kwasababu naamini wapo wahusika wanaofikisha ujumbe. Ningependa kuwakumbusheni kuwa "kutomuuza mbunge" katika ulimwengu wa kidigitali ni uzembe. Labda tunaweza kutembelea wananchi kila kona ya jimbo, lakini tunapawa kuelewa kuwa taarifa za huko ziwekwe sehemu maalumu kutunza kumbukumbu sio mambo ya "MASJALA" tena (hizo ni zama za kale mawe).

Kwa heshima nawakumbusha wasaidizi wa mbunge, kutoitendea haki blogu, kutozungumzia hata utalii ambao ni chachu ya kukuza mzunguko wa fedha wilayani kwetu ni UDHAIFU unaopaswa kurekebishwa.
Ninawatakieni majukumu mema. 
HABARI NI BIASHARA. HABARI NI UCHUMI.

MARKUS MPANGALA,
Oktoba 17/ 2017
Dar es salaam

September 30, 2017

MTOTO UMLEAVYO

Mtoto umleavyo, hivyo ndivyo akuavyo,
Akilelewa hovyo, naye atakuwa hovyo,
Ukimdekeza hovyo, na atalemaa ovyo,
Mtoto umleavyo, hivyo ndivyo akuavyo.

Mtoto mlee vema, aje kukusaidia,
Umzoeshe mapema, kufua na kufagia,
Tamsaidia mama, baba atafurahia,
Mtoto umleavyo, hivyo ndivyo akuavyo.

Ukimletea ukali, atakuwa mwoga sana,
Atajiweka mbali, si jambo lenye maana,
Hapo huzuka kitali, sio vema kuchapana,
Mtoto umleavyo, hivyo ndivyo akuavyo.