Na KIZITO MPANGALA
FUNAMBAI SIA AHMADU alizaliwa mwaka 1969 nchini Sierra Leone katika jamii ya kabila la Kono kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Alifanya kazi na UNICEF nchini Gambia.
Katika kitabu cha “AFRICAN STUDIES” chenye masuala mbalimbali kuhusu jamii mbalimbali za Afrika lipo swali linalouliza hivi ‘je, ukeketaji ukubaliwe na kuendelezwa kama jambo bora la kimila? Watu kadhaa walitoa majibu kuhusu swali hilo kulingana na mtazamo wao wanavyoona. Fuambai Ahmadu alikubali katika insha yake maarufu ya “Rites And Wrongs” kwa mujibu wa kitabu cha “FEMALE CIRCUMCISION AFRICA: CULTURE, CONTROVERSY AND CHANGE” kilichoandikwa na Lynne Rainer, 2001.
Kabla ya jibu la Fuambai Ahmadu, mwanadada Liz Creel Et Al alipinga suala la ukeketaji. Jibu la mwanadada huyu ni kwa mujibu wa ripoti ya “ABANDONING FEMALE GENITAL CUTTING: PREVALENCE, ATTITUDES AND EFFORTS TO END THE PRACITCE” iliyoandikwa na taasisi ya Population Reference Bureau, Agosti 2001 Marekani ambapo Liz anasema serikali za Afrika zipitishe sheria kali inayobana wakeketaji.
Bi Fuambai Ahmadu anatetea
ukeketaji na kukosoa baadhi ya waandishi hasa wasio wa Afrika na wa Afrika pia
wanaohimiza ukeketaji ukomeshwe na kuwataka wanawake na wasichana wa Afrika
wawe na muonekano wa Kimagharibi.
Bi Fuanmbai Ahmadu anasema na
anaamini kwamba ukeketaji haupaswi kuzuiliwa kwa kuwa unaambatana na mila zingine kulingana na jamii husika inayotekeleza
zoezi la ukeketaji ambazo zinampa mkeketwaji kuwa mwanamke anayekubalika zaidi
na jamii yake katika mapokeo ya kihistoria ya jamii hiyo. Yeye ni mmojawapo kati ya waliokeketwa katika jamii
ya kabila la Kono nchini Sierra Leone.
Bi Fuambai Ahmadu anasema anachukizwa na wale wanaohubiri ubaya wa ukeketaji kwamba hawajaona na hawajui jema lililomo kwenye shughuli hiyo na hivyo hulinganisha na maeneo wanayoishi wao ambayo ukeketaji haufanyiki.
Bi Fuambai Ahmadu anasema anachukizwa na wale wanaohubiri ubaya wa ukeketaji kwamba hawajaona na hawajui jema lililomo kwenye shughuli hiyo na hivyo hulinganisha na maeneo wanayoishi wao ambayo ukeketaji haufanyiki.
Katika makala yake ndefu ya “RITES AND WRONGS: EXCSION AND POWER AMONG KONO WOMEN OF SIERRA LEONE” amezungumza mengi kuhusu ukeketaji. Katika makala hayo, anazishauri serikali za Afrika siruhusu ukeketaji ufanyike na ziborshe mazingira ya kufanyia ukeketaji yawe ya kitabibu zaidi yaani ukeketaji ufanyike hospitalini badala ya kienyeji. Ansema “the issue of female initiation and circumcision is of significant intellectual and personal interest to me” yaani “suala la uhamasishaji na ukeketaji kwa wanawake ni jambo la muhimu la kiakili na matakwa binafsi kwangu”
Bi Fuambai Ahmadu anasema yeye
kama mtaalamu wa Anthropolojia kama walivyo Wanaanthroplojia wengine anavutiwa
sana na masuala ya kijamii, kidini, kiitikadi, na kimila katika jamii nyingi na
zaidi ni katika maeneo anayoyajua zaidi. Andai zaidi kwamba suala ukeketaji liboreshwe mazingira yake na hivyo liwe la kitabibu zaidi ili
kuondokana na athari ndogondogo.
Ni Fuambai anasema utafiti
mwingi kuhusu ukeketaji unafanywa na wale wasioishi Afrika na pengine hawana
asili ya Afrika au wale wanaoishi Afrika na wenye asili ya Afrika lakini
hawaishi katika jamii ambazo zinafanya ukeketaji. Ansema wanawake wengi
wanaoandika habari kuhusu madhara ua ukeketaji hwajaishi katika jamii
zinazoheshimu ukeketaji. Anaongeza kusema kwamba ukeketaji hauna madhara,
kinachotakiwa sasa ni kuboresha mazingira ya kufanyia shughuli hiyo.
Bi Fuambai ansema kuwa
wanaopinga ukeketaji wameathiriwa na hoja za kizungu na hisia hasi dhidi ya
ukeketaji. Anasema wengi wanaokosoa ukeketaji wanajitetea kwa hoja za
kimagharibi dhidi ya miili ya wanawake kwa kigezo cha hoja kwamba sehemu
inayoondolewa katika shughuli ya ukeketaji ndiyo msingi mkuu msisimko wa hisia
za mwanamke katika tendo la ndoa. Yeye anapinga
vigezo hivyo vyote na kusema kwamba hata
sehemu hiyo ikiondolewa mwanamke atabaki na msisimko wake kama kawaida. Na vile vile inasaidia kumfanya mwanamke awe mwaminifu zaidi katika
ndoa yake na kuepukana na tama ya kunuia kufuata wanaume wengine.
Bi Fuambai Sia Ahmadu kwa sasa
ana uraia wa Marekani. Anatoa msisitizo kwamba kutokana na madhara ya muda
mfupi baada ya kukeketwa ni vema jambo hilo lifanyike hospitalini ili kuepuka
madhara hayo kuwa makubwa.
Msomaji wa makala haya, umepata
nyongeza ya maarifa kuhusu ukeketaji na jinsi Bi Fuambai anavyotetea suala hilo
kwa nguvu. Huo ndio masimamo wake. Maoni yako ni muhimu sana kuhusiana na suala
hili la ukeketaji hasa katika dunia ya leo ya sayansi na teknolojia kama ilivyoasisiwa
rasmi mwezi Januari mwka 2000.
0692 555 874, 0743 369 108
0692 555 874, 0743 369 108
No comments:
Post a Comment
Maoni yako