Na Albert Nyaluke Sanga, Iringa |
Tangu siku Mungu anamuumba Adam, alimuumba kijasiriamali na
alimwagiza akawe mjasiriamali. Unashangaa? Soma Biblia yako kitabu cha Mwanzo.
Twende polepole utaelewa tu. Unajua neno Ujasiriamali/biashara linamaanisha
nini? Ngoja nikujulishe. Biashara/Ujasiriamali inamaanisha, ubunifu wa
uzalishaji (production), uongezaji wa ulichobuni ama kuzalisha
(multiplication), usambazaji (distribution) na kutawala soko (dominion over
market and ideas/innovation). Umeelewa enhee? Sasa turudi kwa Adamu.
Mungu
alipowaumba Adamu & Eva aliwambia hivi, "Enendeni mkazaliane,
mkaongezeke, mkaijaze nchi na kutawala vitu vyote". Wengi wanaposoma
Biblia huwa wanadhani kuzaana ni "kupata watoto pekee"; lakini
ukisoma English Bible (KJV) ina-highlight vizuri neno hili kuzaana;
"Fruitful". Kuwa "Fruitful" inamaana "kutumia materials/rasilimali/akili
ulizonazo ili kupata ama kutengeneza kitu chenye thamani zaidi", kwa lugha
nyepesi ni 'uzalishaji (production). Tunaenda pamoja?
Hebu turudi kwenye yale
maagizo ya kijasiriamali ambayo Mungu aliwapa akina Adam na mkewe, "Enendeni
mkawe wazalishaji (fruitful/production), mnachozalisha kikaongezeke
(multiplication), mnachokiongeza mhakikishe kinajaa dunia yote (distribution),
hivyo mnavyovijaza dunia yote hakikisheni mnaweza kuvitawala (dominion over
market and ideas)"
Haaa! haaa! Nimekupoteza? Usijali! Rudia kusoma pole
pole, afu ujitahidi kuwa unasoma Biblia kwa tafakari; utaelewa! Sasa yoooote
haya namaanisha nini? Ni hivi: Mungu alimuumba kila mwanadamu kufikiria na
kuishi kijasiriamali. Si lazima kufanya ujasiriamali wa kupata fedha, lakini
mtazamo wa kiujasiriamali utakupa ushindi wa maisha ya Kimungu wakati wote.
~SmartMind~
Kama upo kwenye ajira "isiyolipa" ama hujapata "japo pa
kujishikiza"; basi ujue mtazamo wako kuhusu ajira na maisha "umejaa
matope"!
KWA WALE TU! WANAOTAKA KUFANIKIWA 2013!
Nimekuwa nikieleza mara nyingi kuwa; mafanikio katika maisha
hayaji kwa lelemama! Iwe unataka uchumi mzuri, ajira nzuri, mke ama mume mzuri;
ni lazima jasho likutoke. Hata hivyo sote tunatambua kuwa mafanikio yanaanza
katika ufahamu wako. Namna unavyowaza inaamua namna unavyotenda, namna
unavyotenda inadhihirika katika maisha uliyonayo hata sasa. Huwezi kudanganya!
Tukiyatazama maisha yako, "automatically" tunajua mfumo wa mawazo na
fikra zako.
JE WAJUA? Kuwa mfumo wa mawazo yako ni matokeo ya mambo
unayoyaingiza katika ubongo wako kupitia kusikia, kutazama na kusoma? Kama
umenasa kwenye uhaba wa kifedha basi utambue kuwa ubongo wako umejaza "matango
mwitu" kuhusu fedha, kama mapenzi yanakutesa, uwe na uhakika kuwa fikra
zako zimejaa "upupu" kuhusu unavyotakiwa kubehave kwenye mapenzi.
Soko kuu la Songea mjini |
UNAJIKWAMUAJE KUTOKA HAPO? Jibu ni rahisi! BADILISHA MTAZAMO NA
NAMNA UNAVYOFIKIRI! Utabadilishaje? Jifunze kutoka kwa waliofanikiwa kufika
unapotaka kwenda, Soma vitabu vinavyojenga fikra na mitazamo chanya, ama fanya
yote mawili. Mimi ngoja nikusaidie moja: NITAKUPA VITABU VYA AINA HIYO! Kwa
mwaka mzima nitakuwa nikituma vitabu viwili (2) kila mwezi kupitia
baruabebe(email) vilivyopo katika mfumo wa pdf; kwenda kwa marafiki wote
waliopanga kufanikiwa 2013. Kwa kuanza na mwezi huu Januari nitatuma vitabu
vifuatavyo: 1) THE SCIENCE OF GETTING RICHER 2) COACH YOURSELF TO MAXIMUM
EMOTIONAL INTELLIGENCE. Kwa rafiki unayehitaji ninapenda unijulishe email yako
hapa (ama inbox) kisha utapokea vitabu hivi. KAMA UNATAKA KUFANIKIWA, KUJIFUNZA
HAKUKWEPEKI. ~SmartMind~
very powerful
ReplyDelete