March 25, 2011

TANZIA: ASIFIWE HATUNAYE DUNIANI

Nimeshangaa lakini hofu haikubaki nyuma. Awali taarifa zako zilikuwa njema kwangu kwani baada ya matatibabu yako pale Kinondoni niliamini utakuwa salama mdogo wangu. Niliarifiwa na dada Yasinta uko salama na hakika utapona. Lakini siku ya jana nipo katika safari ngumu ambayo sijawahi kuifanya, lakini kazi imenifanya niwe mtumwa mdogo wangu.

Naomba dunia ikuombee mdogo wangu mpenzi kwa hakika tuna mengi ya kujifunza kutokana na uhai wako. nipo mbali na watu wengi lakini nitakuwa nawe kwa kila namna yoyote ya kufanya. Asifiwe dadangu mpenzi najua hatukuwa pamoja kwa muda sasa lakini matarajio ya kukutana punde yalikuwa makubwa. Ewe mlimbwende,mwali na binti usiye na makuu. Ulivumilia kila hali hapa duniani na ulijua dada yangu anakupenda na kila alipenda awe nawe kwa kila namna. alihangaika huku na huko kuhakikisha uko salama lakini mungu amekupenda zaidi.

Nakuandikia maneno machache kuwa TAMBUA NAKUPNDE NA UMEKWENDA MBELE ZA HAKI. POLENI FAMILIA YA MZEE GERVAS NGONYANI, NDUGU NA MARAFIKI WOTE.
AMEN.

2 comments:

  1. ni pigo kubwa....lakini sisi wanadamu tuna nini hata tukuzuie wewe usiende? Hukusema neno la kutuaga...lakini ukasema utatuombea daima huko ulikokwenda....hupo nasi kimwili....lakini kiroho ungali nasi siku zote....
    Tunamwomba Mungu akuangazie mwanga wa milele.
    Amina!

    ReplyDelete
  2. USENGWILI, Yaani hili pigo ni kubwa mno hata kusimulia siwezi . Basi niseme tu ahsante kwa kila mlotutendea kwa kutufariji..Pumzika kwa Amani mdogo wangu Mpendwa Asifiwe.

    ReplyDelete

Maoni yako