Showing posts with label Ruvuma. Show all posts
Showing posts with label Ruvuma. Show all posts

February 13, 2018

JE, WAKALA WA MAJENGO NCHINI (TBA) WANAO UWEZO WA KUKIDHI MAHITAJI YA SEKTA YA UJENZI?


Jengo hili linalotakiwa kujengwa na TBA halijaisha hadi leo. Lipo Halmashauri ya Madaba, mkoani Ruvuma. Haifahamiki litajengwa lini au wakati gani. Hali hiyo inachochea baadhi ya mafundi kuondoka. Chanzo cha habari kimesema, “Hata kwetu Nyasa wapo tunatimua muda sio mrefu hao (TBA) sio wenyewe,”

DC SONGEA
Naye mkuu wa wilaya ya Songea amekasirishwa na utendaji duni wa TBA. DC huyo amesema, “DC SONGEA HAIWEZEKANI UJENZI WA GOROFA HATA KOKOTA HAKUNA TBA MNASUMBUA WATU,”

Mkuu huyo amewataka wakala wa uthibiti wa majengo TANZANIA TBA kuharakisha ujenzi wa ofisi ya mkurugenzi wa Madaba kwa wakati ili kusogeza huduma kwa wananchi. Katika wilaya ya Nyasa wanajenga ghorofa la ofisi ya Mkurugenzi, Chuo cha Veta, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya (DC) na Nyumba ya Mkuu wa Wilaya (DC).

February 03, 2018

MUHUKURU: MGODI WA PILI WA MAKAA YA MAWE MKOANI RUVUMA

NA MWANDISHI WETU
 
KAMPUNI ya KAMBAS GROUP yenye makao yake Makuu jijini Mwanza imeanza kazi ya uchimbaji makaa ya mawe katika Mgodi Mpya wa Muhukuru wilayani Songea mkoani Ruvuma.

Kwa mujibu wa Afisa Mahusiano wa Kampuni hiyo, Issa Litunu amesema tayari kampuni hiyo imefungua tawi mjini Songea ambapo hatua za awali za uchimbaji na usafirishaji zimeanza.

Litunu amesema katika kipindi cha wiki moja Kampuni hiyo imechimba zaidi ya tani 1000 za makaa ya mawe ambayo yanasafirishwa kutoka mgodini umbali wa zaidi ya kilometa 100 toka mjini Songea, yanawekwa eneo la Likuyufusi lililopo Kata ya Lilambo Manispaa ya Songea kabla ya kusafirishwa kwa wateja jijini Dares Salaam.

Hata hivyo Afisa huyo amesema kazi rasmi ya uchimbaji inatarajia kufanyika baada ya kupungua mvua za masika ambazo hivi sasa zinaleta Changamoto ya barabara.Amesema taratibu zote zimefuatwa kabla ya kuanza kazi ya uchimbaji.Huu ni mgodi wa pili wa makaa ya mawe katika mkoa wa Ruvuma. Mgodi wa kwanza wa makaa ya mawe ni wa Ngaka uliopo wilayani Mbinga.

January 20, 2018

NDANI YA KISIWA CHA FALKLAND

NA ALBANO MIDELO, LITUHI
HIKI ni kisiwa kidogo cha Falkland ambacho kipo kwenye maingilio ya Mto Ruhuhu katika Ziwa Nyasa.Kisiwa hiki kinamilikiwa na wavuvi toka Ludewa mkoani Njombe na Nyasa mkoani Ruvuma.
Asili ya kisiwa hiki kuitwa Falkland ni mgogoro wa kugombania kisiwa hicho uliotokea mwaka 1982 kati ya wavuvi wa Ngelenge wilayani Ludewa wakati huo mkoa wa Iringa hivi sasa Mkoa wa Njombe na wavuvi wa Lituhi wakati huo wilaya ya Mbinga ambapo sasa ni wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

January 15, 2018

KARIBUNI RUVUMA. KARIBUNI KUTALII TUNDURU

Hili ni Jiwe kubwa sana ambalo linavutia watalii. Hili ni mojawapo tu, maana yapo zaidi ya haya. Mawe haya yanapatikana kilometa chache tu kutoka Tunduru Mjini mkoani Ruvuma.

November 24, 2017

TANZIA: MBUNGE WA SONGEA MJINI AFARIKI DUNIA



NA MWANDISHI WETU, SONGEA
MBUNGE wa Jimbo la Songea Mjini kupitia chama cha CCM ndugu Leonidas Tutubert Gama amefariki dunia usiku wa kuamkia leo hii katika Hospitali ya Peramiho ambapo alilazwa kwa saa chache kabla ya kifo chake.

November 13, 2017

MILIMA NA MABONDE YA MATOGORO KIVUTO CHA UTALII


Katika eneo hilo lililopo kusini mwa mji wa Songea, kuna bonde kubwa kabla ya kuufikia mlima huo. Ni eneo ambalo linavutia watalii. Mtu yeyote akipanda mlima wa Matogoro anaweza kutazama mji wa Songea ukiwa chini yake. 

November 03, 2017

KAULI YA MKUU WA MKOA WA RUVUMA

"Mimi ni Mnyamwezi original nipo tayari kutwishwa mizigo yote,mnitwishe wanaruvuma mizigo yote kwa lengo la kuleta maendeleo ndani ya mkoa',”
 
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ni Christina Mndeme

October 27, 2017

KWANINI WILAYA YA NYASA IMESHIKA MKIA KATIKA MATOKEO YA DARASA LA SABA?



RAYMOND NDOMBA, SONGEA
WILAYA ya Nyasa iliyopo mkoa wa Ruvuma imekuwa ya mwisho katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu 2017 kimkoa. Swali la kujiuliza ni kwanini hali hiyo imetokea. 


Mawazo yangu ni haya; Pamoja na sababu nyingi zilizosababisha matokeo hayo ya aibu kubwa. Wazazi wanapaswa kubeba lawama kubwa. Wengi wao hawafuatilii maendeleo ya watoto wao, pia makuzi na malezi mabaya.

Miaka ya hivi karibuni (kuanzia mwaka 2000), Wazazi wengi katika wilaya ya Nyasa hawajali elimu, hawajigusi katika ufuatiliaji wa watoto wao kielimu na hata kitabia (Angalia matokeo ya mitihani ya Taifa ya shule za msingi na sekondari kunzia miaka hiyo ya 2000 kwa shule kongwe ndani ya wilaya). 

January 15, 2013

MIKOA YA MTWARA,LINDI NA RUVUMA TAFUTENI SULUHU KUFELI MITIHANI

Na Hamisi Magendela , Dar es Salaam
SIKU chache zilizopita wananchi wa mikoa ya kusini waliandamana kupinga uchimbaji wa bomba la gesi kutoka huko kwenda Dar es Salaam ambacho ingetumika kwa ajili ya kuzalisha umeme.
wanafunzi wakiwa darasani katika moja ya shule za msingi wilayani Nyasa
Umeme huo ambao ungezalishwa jijini Dar es Salaam ungetumika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania hali ambayo inaaminika kuwa itasaidia kupungua ghalama za umeme na kufanya ukali wa maisha kupungua.
Sipingi mawazo yao kwani kila mmoja anafikilia kwa utashi wake japo ni vema wakaangalia faida kuliko na mafanikio yatakayopatika siku za usoni ikiwa gesi hiyo itasafilishwa kwa njia ya bomba kwenda Dar es Salaam.
Kikumbwa ambacho naweza kusema ni kwa wananchi wa mikoa ya kusini wanatatizo makubwa zaidi ya kuandamana kutaka manufaiko ya gesi wakati suala zima la elimu likiwa limewatupa mkono kiasi kwamba inatia simanzi kuona inashika nafasi 10 za mwisho katika ufauru wa matokeo ya kidato cha pili yalitangazwa juzi na Wizara ya Elimu na Mafunzo jijini Dar  es Salaam jana.
Licha ya kuwa ni aibu kwa wananchi pamoja na viongozi wa mkoa huo lakini naweza kusema kuwa ni kashfa ambayo katika miaka 50 ya Uhuru ijayo inatakiwa kufanyiwa kazi ili kuhakikisha wanapata elimu ya kutosha na kuondoka na ujinga wa kukosa elimu.
Ingekuwa vema zaidi badala ya kulalamikia kuhusu gesi wangepiga kelele kwa kukosa elimu bora kwa wanachi wengi wa mikoa hiyo hali inawafanya kukosa nafasi nzuri katika viwanda vinavyojengwa katika mikoa.
Kwa maana nafasi nzuri ya ajira itakuwa ikishirikiliwa na wageni ambao wana elimu ya kutosha ya kukidhi mahitaji ya kazi inayohitajika kwa wakati huo na kufanya wenyeji kufanya kazi za hali ya chini kila siku.
Pia wananchi wa mikoa ya kusini umefikia wakati wa kusimama kidete kuhakikisha fursa iliyotangazwa na Serikali kuwa kuanzia sasa hakutakuwa na mwalimu atakaepangiwa kazi mijini kwa wanaotoka vyuoni.
Kwa maana hiyo ikiwa viongozi wa mikoa hiyo wakitumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi wa kuzingatia elimu badala ya kung'ang'ani masuala ambayo kwa sasa hayasaidii sana katika miaka 50 ijayo.
Kusudio hilo la Serikali kupeleka walimu vijini linatokana na malalamiko kutoka sehemu hizo kuwa zimesahaurika kielimu kutokana na kukosa walimu wa kutosha hali inayofanya mikoa hiyo kushikia mikia katika matokeo ya mwisho kama ilivyo sasa kwa mikoa ya kusini.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu ilisema lengo la kufanya hivyo ni kupata uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 10 hali itakayosaidia kunyanyua kiwango cha elimu katika mikoa iliyo pembezoni mwaka nchi.
Hivyo naamini fursa hiyo ikiwa itatumiwa vema na wananchi wa huko itafanya viwanda vinavyojengwa sasa katika mikoa hiyo wenyeji kunufaika kazi zaidi kuliko wageni ndio madhumuni makubwa ya baadhi ya wawekezaji.
Kwa maana wapo wanaotoa ahadi kuwa ikiwa viwanda vyao vitamalizika waajili wenyeji kwa asilimia zaidi ya 60, lakini ikiwa hali ya elimu itaendelea kuwa hivyo ni dhairi wageni watakuwa na nafasi kubwa kuliko wazawa.
Viongozi wa mikoa ya pembezoni mwa Tanzania ikiwemo ya kusini kazi kwenu kuhakikisha mnahamasisha wananchi wenu wanatumia fursa inayotolewa na Serikali kupeleka walimu vijijini inatumiwa vizuri na matunda yaonekana.
Pia kwa Serikali ni vema ikatambu kuwa si walimu pekee wanahitajika katika mikoa hiyo iliyo pembezoni mwa Tanzania bali vyenzo za kufundishi nazo ni muhimu, itakuwa haina maana kupeleka walimu bila ya vitendea kazi na kuwajengea miondo mbinu mingine ikiwemi malazi bora.
Kwani upo uhushuhuda kuwa walimu wengi wanakacha kwenda kufundisha vijini kutokana na kutopatiwa mahitaji muhimu ya kibinadamu ikiwemo usafiri, nyumba nzuri za kuishi na kuishi katika maboma.
 Maoni: 0782839898