November 24, 2017

TANZIA: MBUNGE WA SONGEA MJINI AFARIKI DUNIA



NA MWANDISHI WETU, SONGEA
MBUNGE wa Jimbo la Songea Mjini kupitia chama cha CCM ndugu Leonidas Tutubert Gama amefariki dunia usiku wa kuamkia leo hii katika Hospitali ya Peramiho ambapo alilazwa kwa saa chache kabla ya kifo chake.


Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na Ofisa Habari wa Manispaa ya Songea, Albano Midelo na kubainisha kuwa Mbunge Gama alikimbizwa hospitalini Peramiho baada ya kujisikia homa. 

Aidha, taarifa zinasema kuwa Mbunge Gama alikuwa kwenye matibabu nchini India wiki kadhaa zilizopita, ingawaje haikufahamika mara moja ni ugonjwa gani ulisababisha afuate matibabu nchini humo.

Leonidas Gama ameshawahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Kilimanjaro, pamoja na kuwa Mkuu wa Wilaya za Ilala, Newala, Nachingwea, Muheza na Mbeya Mjini.

Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako