May 05, 2018

TAARIFA MUHIMU: TUMESITISHA KUWEKA TAARIFA MPYA ZA NYASA

MARKUS MPANGALA
SALAAM nyi wasomaji wetu wapendwa! 
Ni matumaini yetu nyote mna afya njema na Mwenyezi Mungu amewajalia hilo bila hiyana. Tumshukuru zaidi.
Kwa muda mrefu  nimekuwa nikitoa huduma ya habari za mwambao wa Ziwa Nyasa na yatokanayo na wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma. Nimekuwa nikifanya hivi kama mapenzi yangu tu (bila kutafuta faida yoyote ya fedha). Sikulipwa chochote kwa kutoa huduma hiyo ya kutangaza vivutio vya utalii, utamaduni, changamoto na mambo mseto ya wakazi wa maeneo hayo. 
KIZITO MPANGALA
Nilianzisha blogu hii mwaka 2007 nikiwa mwanafunzi kwa mapenzi yangu baada ya kupata somo kubwa kutoka kwa mwanablogu mashuhuri Ndesanjo Macha na msaada wa karibu wa mchoraji katuni maarufu Simon Regis. Wakati huo Macha alikuwa akielezea umuhimu wa nyenzo nyingine za upashanaji wa habari kama njia nyingine ya kuifikia jamii na kukuza uchumi pamoja na kuhifadhi taarifa za ukanda wa ziwa Nyasa. Leo hii ukiingia mtandao wa kama wa Google kutafuta taarifa za mwambao wa ziwa Nyasa utakutana na mengi yaliyoandikwa kwenye blogu hii kuliko Kamusi Elezo Huru ya mtandao wowote.

HIVYO basi… Napenda kuchukua nafasi hii kuwajulisha, tangu Machi 26, 2018, nilisitisha kutoa huduma ya taarifa za ukanda wa Nyasa iwe kwa njia ya picha au maneno. Tunawashukuru wasomaji wetu 664,299 mlioshirikiana nasi, ndani na nje ya nchi kwa ushauri au kuliza mengi kuhusu maeneo hayo na kuomba maelekezo mbalimbali pamoja na wale walioamua kuchukulia Blogu hii kama nyenzo ya kupata taarifa za utalii mwambao wa Nyasa na maingizo mapya yaliyoanza mwaka 2018, Tawasifu, uchambuzi kuhusu Nyasa, utafiti zaidi wa maeneo ya vivutio, Mitazamo na kadhalika. 

HONORIUS MPANGALA
Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu, nimeamua kusitisha  kutoa huduma katika blogu hii kwa MUDA USIOJULIKANA. Wakati ninawashukuru wasomaji, pia napenda kutoa shukrani zangu kwa wadogo zangu wapendwa, Honorius Mpangala na Kizito Mpangala kwa kuandika bila kuchoka pamoja na kuendeleza mapenzi yao kuhusu nyasa, historia na kadhalika. 

Namshukuru pia rafiki zangu Fadhy Mtanga, Yasinta Ngonyani, Profesa Joseph Mbele kwa ushauri kuhusu Nyasa na mipango ya maendeleo. Tunamshukuru kila mmoja aliyeshirikiana nasi kuhifadhi taarifa ambazo hazipo kwenye makabati yetu, na hazikuandikwa awali. 

MUHIMU: Kwa sasa unaweza kutembelea ukurasa wa ‘Lundu-Nyasa”@KijijiChaLundu katika mtandao wa Facebook. Karibuni huko.

Markus Mpangala,
Mwanzilishi na Mmiliki
Mei 5/2018
Dar es salaam, Tanzania
KWAHERINI

1 comment:

  1. Mume wangu amerudi!!! Baada ya miaka 1 ya ndoa iliyovunjika, mume wangu aliniacha na watoto wawili na maisha yangu yalivunjika. Nilitaka kuyamaliza, nusura nijiue maana alituacha bila chochote. Nimekuwa nimevunjika kihisia wakati huu wote na maisha yanaonekana kutokuwa na maana. Siku moja mwaminifu, nilipokuwa nikivinjari mtandao, nilikutana na baadhi ya shuhuda kuhusu Dk DAWN. Baadhi ya watu walishuhudia kwamba alimrudisha mpenzi wao wa zamani, wengine walishuhudia kwamba anarejesha tumbo na kuponya magonjwa kwa mimea. Nilipendezwa zaidi na upatanisho na mume wangu, ambao Dk. DAWN aliwezesha kumrudisha mume wangu ndani ya siku 3. Sasa mume wangu amerudi na tumekuwa tukiishi kwa furaha tangu wakati huo. Shukrani zote kwa Dk DAWN. Hapa, ninaacha mawasiliano yake kwa kila mtu. Maana kuna changamoto za aina yoyote,
    Barua pepe ( dawnacuna314@gmail.com )
    Whatsapp: +2349046229159

    ReplyDelete

Maoni yako