NA KIZITO MPANGALA,0692 555 874
Ndoa ni kitu johari, thamani yake nyumbani,
Ndoa ni kitu johari, thamani yake nyumbani,
Ndoa
usiikahiri, utakuwa matatani,
Ndoa
yahitaji siri, zihifadhiwe chumbani,
Pambo
la ndoa mapenzi, yenye afya na nidhamu.
Kuvumiliana
nako, ni muhimu kwenye ndoa,
Usiupende
unoko, utakutia madoa,
Nawirisha
ndoa yako, isinuke fondogoa,
Pambo
la ndoa mapenzi, yenye afya na nidhamu.
Pambo
la ndoa si pesa, ni mapenzi nakwambia,
Hata
pesa ukikosa, mapenzi yatafidia,
Ninakuambia
sasa, kwa masikio sikia,
Pambo
la ndoa mapenzi, yenye afya na nidhamu.
Penzi
halina mwalimu, wanandoa mfahamu,
Mlidumishe
lidumu, sizungumzi fonimu,
Nisikilize
ghulamu, lisikufikie ghamu,
Pambo
la ndoa mapenzi, yenye afya na nidhamu.
Mapenzi
pambo la ndoa, wanandoa nawambia,
Yaepukeni
madoa, ndoa kuwaharibia,
Hamwezi
kukokotoa, kwa hisabati na bia,
Pambo
la ndoa mapenzi, yenye afya na nidhamu.
Msikilizane
vema, jeuri ya fedha noma,
Zungumzeni
daima, kwa wema nayo hekima,
Mapenzi
yape heshima, mnapoishi daima,
Pambo
la ndoa mapenzi, yenye afya na nidhamu.
Migogoro
itupeni, mbali isionekane,
Yadumisheni
mapenzi, tena mvumiliane,
Msifanye
unajisi, na wala msizozane,
Pambo
la ndoa mapenzi, yenye afya na nidhamu.
Wasalamu
kutamka, sio kauli kukata,
Sasa
muda wa uraka, na ulimi unanata,
Ndoa
kuwa na viraka, inaongeza utata,
Pambo
la ndoa mapenzi, yenye afya na nidhamu.
Na Kizito Mpangala
No comments:
Post a Comment
Maoni yako