Ndugu
zangu sikieni, mimi hapa naondoka,
Ninahitaji
amani, mirindimo nimechoka,
Ninakwenda
kwa jirani, hata kama akifoka,
Ninaondoka
jamani, amani naitafuta.
Mitaani
kuna mambo, twakimbizana daima,
Yapo
mengi machafuko, yananitisha daima,
Yatokea
milipuko, inanipatia homa,
Ninaondoka
jamani, amani naitafuta.
Risasi
zinasambaa, mirindimo inazidi,
Naishia
kutambaa, ninapigwa na baridi,
Ninawasha
mishumaa, kufukuza ukaidi,
Ninaondoka
jamani, amani naitafuta.
Waasi
nao watisha, siwezi kuvumilia,
Mikutano
waitisha, mapigano kutulia,
Wakirudi
wanawasha, bomu kutufyatulia,
Ninaondoka
jamani, amani naitafuta.
Jirani
niwie radhi, hali yangu waiona,
Unigawie
ardhi, na wanangu nitapona,
Yaone
yangu maradhi, nisaidie kupona,
Ninaondoka
jamani, amani naitafuta.
Siwezi
kuishi hapa, na milio ya risasi,
Mabomu
yanalipuka, jirani kabisa nasi,
Wanangu
hawana raha, wanalala kwenye nyasi,
Ninaondoka
jamani, amani naitafuta.
Ndoto
yangu kuwa hai, kila siku nilalapo,
Ninahitaji
uhai, na wanangu waliopo,
Hatupuganii
chai, amani hapa tulipo,
Ninaondoka
jamani, amani naitafuta.
Ninataka
hewa safi, siyo kama iliyopo,
Inanuka
tu baruti, inakuwa na uvundo,
Vumbi
limetamalaki, mchakato wa mapigano,
Ninaondoka
jamani, amani naitafuta.
Ninataka
maji safi, si haya niliyonayo,
Yamechafuliwa
maji, ninaumia kwa moyo,
Maji
kweli ni uhai, hapa kwetu ni uchoyo,
Ninaondoka
jamani, amani naitafuta.
Nitakuwa
mkimbizi, niipate tu amani,
Sihitaji
kuwa mwizi, kuna nini duniani,
Hatuna
pia mavazi, ni haya tu ya mwilini,
Ninaondoka
jamani, amani naitafuta.
Ninakwenda
kwa jirani, nikaipate hifadhi,
Kuitafuta
amani, na kipande cha ardhi,
Nipokeeni
jamani, niyaondoe maradhi,
Ninaondoka
jamani, amani naitafuta.
Mashamba
yangu hakika, yana hali mbaya sana,
Yamegeuzwa
uwanja, wa vita kupigana,
Na mimi
sina hatia, moyoni ninaumia,
Ninaondoka
jamani, amani naitafuta.
Siasa
za kupigana, hazitazaa matunda,
Waasi
wanazaliwa, watazidisha ununda,
Mimi
sitaishi hapa, moyo wangu unadunda,
Ninaondoka
jamani, amani naitafuta.
Vikao
vingi vyafanywa, kukomesha mapigano,
Haionekani
dawa, kuponyesha mirindimo,
Nabaki
nimeduwaa, naumia kwenye moyo,
Ninaondoka
jamani, amani naitafuta.
Bunduki
zinarindima, zimekuwa kama bao,
Siwezi
kuishi hapa, penye sauti za ndumo,
Uhai
ninautaka, sipendi kuwa na ndweo,
Nianondoka
jamani, amani naitafuta.
Kwa
herini waungwana, mimi sasa mkimbizi,
Tutakuja
kuonana, hadi iachwe bunduki,
Ninahitaji
kupona, makovu haya kichwani,
Ninaondoka
jamani, amani naitafuta.
Wasalamu
natamka, ninakwenda kwa jirani,
Hapa
mimi nimechoka, nianatafuta amani,
Nalazimika
kutoka, nikaishi ugenini,
Ninaondoka
jamani, amani naitafuta.
Na Kizito Mpanagala
No comments:
Post a Comment
Maoni yako