October 05, 2017

MAISHA

Maisha ni furaha na huzuni,
Yakupasa kuyafikiri akilini,
Ongeza na maarifa ubongoni,
Usisahau na akiba kibindoni.

Ni huzuni na furaha maishani,
Ni furaha zaidi kupata amani,
Ya maisha kuitunza duniani,
Aliye mjini hata kijijini.

Maisha ni huzuni na furaha,
Wengine raha waona karaha,
Wapo wanaoupenda mzaha,
Wenigne wajigamba kwa madaha.


Ingawa ni furaha na huzuni,
Nyumbani kwetu nako mamtoni,
Jitahidi kuweka akiba kibindoni,
Ikufae uishipo hapa duniani.

Kweli ipo huzuni na furaha,
Tuichapeni kazi tuache mzaha,
Raha yetu isije kuwa karaha,
Unisikilize kwa makini Twaha.

Hakuna atafutaye huzuni,
Kwani yapiku furaha maishani,
Ikiingia  kukuvamia akilini,
Tadhani huna thamani duniani.

Furaha na amani sote tunataka,
Kuishi vema bila mashaka,
Tuchape kazi tusiogope viraka,
Tuongeze juhudi kakakaka.

Kalamu wino umejiishia,
Nami hapa basi nakomea,
Nakutaka uwe na furaha,
Usisahau akiba kujiwekea.


Na Kizito Mpangala

No comments:

Post a Comment

Maoni yako