Showing posts with label tehama. Show all posts
Showing posts with label tehama. Show all posts

March 19, 2018

UMUHIMU NA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZA NYWILA (PASSWORD)

Na KIZITO MPANGALA

Kila mmoja anatamani kuendeleza siri kubwa ya taarifa zake katika simu yake au tarakilishi (kompyuta) yake ili zisijulikane na wengine. Ulizni wa taarifa hizo husaidiwa na nywila (password). Nywila (password) inaweza kuwa ya haerufu tupu, namba tupu au mchanganyiko wa herufi pamoja na namba na baadhi ya alama za uandishi kama vile mkwaju (/) na kadhalika. Nywila ina umuhimu mkubwa katika ulimwengu huu wa Sayansi na Teknolojia ingawa ilianza kutumika zamani ila siyo kwa kiwango kikubwa kama ilivyo sasa.

Kabla ya kuboreshwa kwa teknolojia ya mawasiliano, zamani password ilijulikana kama “passphrases.” Kwa hiyo nywila ni ufunguo unaolinda lango la kuingilia katika kuzijua taarifa zako ili zisivamiwe na wengine (hackers). Hii ni kwa ajili ya usalama wa mawasiliano yako. Kila mmoja duniani ambaye anatumia tovuti au kurasa mbalimbali hukutana na kipengele cha kuingiza password ili apate anachokihitaji. Malengo ya nywila (password) ni:

1.      Kukupa ruhusa ya kuingia kwenye akaunti husika unayaotembelea,iwe ya kwako au ya mtu mwingine au kikundi au kampuni.

2.    Kuipa ruhusa barua pepe ifunguke ili kuona taarifa zilizomo. Baruapepe inaweza kuwa ya kwako au ya mtu mwingine kadiri ya maelewano kati yenu.

3.    Kulinda vifaa vya kielektroniki ili visitumiwe na wengine ikiwa mmiliki hapendi vitumiwe na wengine. Vifaa hivyo ni kama vile simu, tarakilishi (kompyuta), tarakilishi mpakato (laptop), ubamba (tablets) na kadhalika.

4.    Kupata mtandao (network) ikiwa itahitajika kutumia password.

5.     Kulinda tovuti ili isiingiliwe na wengine (hackers)

6.    Ulinzi wa data binafsi, za kikundi au za kampuni fulani.