February 11, 2009

Shindano! KITENDAWILI........

KITENDAWILI........................................., "Ni CHEUPE kama barafu na ni CHEUSI kama giza, KULIWA ni HARAMU na kunywa ni HALALI, kina herufi 5 na kinaanza na herfi M.
Kinatumiwa na WANAWAKE mara moja katika UMRI wao, na kinatumiwa na WANAUME mara tatu kwa siku.
Je, ni kitu gani hicho? Ukipata jawabu lake.

NB: ZAWADI NONO kwa mshindi

15 comments:

 1. Dah!! Kweli hiki ni kitendawili. Nawasubiri wenye kutegua ama tutakupa mji wa hukohuko Nyasa ukubali na kutuambia.
  Blessings

  ReplyDelete
 2. Mzee wa Changamoto msitake mji, ninyi nipeni jawabu tu halafu TUZO itatangazwa na hakika itatekelezwa tu.
  nawasubiri wengine. Koero yuko wapi wala simuoni humu, au kalala????

  ReplyDelete
 3. Nipo ngoja nitafakari........

  ReplyDelete
 4. Markus nimeshindwa,
  Ngoja nikupe mji, nendaaaaaaa,
  Nendaaaaaa, kijiji kimoja kinaitwa MFARANYAKI

  ReplyDelete
 5. JIBU LAKE NI MANII

  ReplyDelete
 6. MIMI NI SARA, JIBU LAKE NI MANII, NDIYE NILIYEANDIKA HAPO JUU

  ReplyDelete
 7. Koero kumbe upooOOO?
  Umetafakari lakini umeshindwa DUH!

  Sawa, unanipa mji,unataja kijiji cha Mfaranyaki. LAKINI Mfaranyaki ni mtaa tu uliopo hatua chache toka stendi kuu ya mabasi Songea.
  PIA niligoma sitaki mnipe mji, NATAKA JIBU

  SARA: Unasema MANII? nikuulize swali kwanza, je wanawake wanatumia MANII mara moja katika umri wao na wakati gani??? MANII wanaume wanatumia mara tatu kwa siku????????
  ha ha ha ha ha ha nacheka sana, ipo kazi hapa

  SARA asante kwa jawabu lakini tafakari maswali hapo juu halafu jiulize kama jawabu lako ni sahihi au la>
  Nawangojea wengine, ila msinipe mji!!!!!!

  ReplyDelete
 8. He! Markus, yaani bado umekomaa tu unataka jibu?

  Niliposema nakupa mji wa mfaranyaki, nilijua tu kwamba utafananisha na mtaa uliopa Songea,
  basi umechemsha, Kwa taarifa yako kuna mji unaitwa mfaranyaki kule Msumbiji.
  Kaka soma Jiografia......

  bado natafuta jibu, nikipata nitakujibu.
  Naona umempa changamoto dada Sarah.

  Sarah: mwaya hongera kwa kujaribu.

  ReplyDelete
 9. This comment has been removed by the author.

  ReplyDelete
 10. Kitendawili hicho ni kigumu kwani najaribu kufikiria ni kitu gani kinaweza kuwa cheupe na pia kikawa cheusi?, au jamaa katunga ili aweze kuwachemsha wana nzengo?, Akubali kupewa mji atupe jibu.

  ReplyDelete
 11. jibu ni maiti

  ReplyDelete
 12. JIBU NI MAUTI

  ReplyDelete
 13. mbona mauti haijaanza na herufi x

  ReplyDelete

Maoni yako