Jamani, sasa hivi ndiyo nataka kufunga haka kaofisi kangu niende nami nyumbani. Lakini najua nikifika tu kitu cha kwanza ni kuifungua kompyuta yangu ili niendeleza mambo yangu ya kukaa na tarakilishi. Na zaidi basi nitakaa nyuma ya DSTV niangalie soka au marudio ya Tenisi au vipi, na zaidi ule muziki wa Kwaito mtamu...... Nadhani mtani anajua utamu wa soka. TUACHE HILO.....
KUNA hili jambo nilikuwa najaribu kuwaza dakika chache hizi na hadi sasa naandika naendelea kuwaza. HIVI WEWE UNAMWAMINI NANI HASA KATIKA MAISHA YAKO? Yaani UNAVYOISHI KILA SIKU KUNA MTU UNAMWAMINI SANA? KWANINI?
Unajua katika maisha yetu haya kuna wakati unakuwa na marafiki wengi sana, na wengine wanaweza kukupotosha halafu ukajuta hapo baadaye. Labda utaniuliza mimi namwamini nani. Mwenzangu yupo mtu namwamini anaitwa Yasinta Ngonyani, ni sababu nyingi na ukweli NAMWAMINI SANA. Lakini ukiniambia nikwambia sababu za KUMWAMINI, sitakwambia....
Hebu jiulize wewe unayesoma hapa UNAYEMWAMINI NA KUMWAMBIA MAMBO YAKO, HASEMI KWA WENGINE MAMBO HAYO? au UNAMWAMINI KIASI GANI? Bado mfululizo wa MAWAZO TU. ok naenda nyumbani, nimeimiss tarakilishi yangu aiseh
Markus sina la kusema zaidi ya Ahsante!
ReplyDeleteswali la msingi mseee!
ReplyDeleteKama mie ndo ngekuwa Yasinta ngekutafutia mke :-)
Mi ningekuwa Yasinta.....
ReplyDeleteKaka Chacha kwa nini nimtafutie mke mimi?
ReplyDeleteNa mtani! We ungekuwa Yasinta.....Ungefanya nini?
Swali gumu, ila naungana mkono na Yasinta juu ya swala la kumtafutia mke, kitu hiki kinaweza mfanya Mpangala asimuamini tena Yasinta.
ReplyDeletemi najiamini mwenyewe
ReplyDeleteMambo,me nafikiri umwambie Mungu kama unaamini yupo kwani yeye ana uwezo wa kuongea na kila mtu na acweze kutoa siri zako kwa mwingine.Nimetembelea blog yko leo na nikavutiwa na mada na nyingine nyingi ila tu mda hauniruhusu.Haya kazi njema na mafanikio mema.janeth.
ReplyDelete