June 09, 2010

UNAONAJE HILI katika MAISHA YAKO

Nimekaa katika kaofisi kangu lakini nikajikuta kicha kinakataa kufanya kazi. Najiona waziwazi nimesongwa na mawazo. Ingawaje wapo wanaweza kusongwa na mawazo kiasi hata wakaugua mgandamizo wake kutokana na kuwaza kwa muda mrefu, lakini kwangu ni tofauti. Nimekwisha kuugua sana suala la msongo wa mawazo lakini tiba zangu ni mazoezi, na kufanya kazi mbalimbali, kifupi mwili wangu unahimili vihoma vya kijinga kama hivi.

Ila nawaza sana leo. Nikiwazacho pengine kwasababu tu nawaza kutokana na nilivyo labda, ingawa sijui nipoje Lol... Hapo ndipo nikamkumbuka WILLIAM SHAKESPEARE. Nikakumbuka maandiko yake fulani hivi.

Yaap! Ukisoma kitabu chake cha TIMMOTH OF ATHENS(samahani jina la kwanza lina kawaida ya kunikwepa kulijua, sijui ni TIMMOTH au TIMMON maana ni muda mrefu sijakitia machoni tena. Si unajua cha kuazima hakisitiri wowowo??.....Ngoja tu).

Sasa katika maandiko yale anasema hivi HAKUNA KINACHOCHOCHEA DHAMBI KAMA HURUMA. eti mwenzangu unaonaje hii hoja. Inakuingia kichwani kweli? UKIWA NA HURUMA SANA INACHOCHEA DHAMBI wanungwana? Mimi sijui ila nilizama katika tafakuri anuai, nikajikuta nawaza hiki kipengere.

2 comments:

  1. Wa bambu veve tola likizu uhambaye kunyanja ukapumulilayi na kulya ugali wa mayavu na somba . chondichondi

    ReplyDelete
  2. Kwa sababu Yasinta ameanza kwa kuongea kikwenu, sichangii.

    ReplyDelete

Maoni yako