Nilikuwa nimekaa nimechoka hata sikuwa na hamu ya kublogu leo, lakini kitu ninachokipenda ni lazima angalau nisome rafiki yangu Yasinta alichoandika angalau kujipendelea na kuchangamsha kichwa.
Na kweli wakati nikisoma, ghafla umeingia ujumbe wa simu ya kiganjani kutoka kwa rafiki yangu Joe Pardley, akaniuliza nina habari gani za afrika leo ambayo inanigusa.
Kwakuwa anajua kuwa maswali yake yananighadhibisha. Nitafakari kuna nini. Ndipo akaniambia Nisome kwa dada Chemi Che Mponda..
MASIKINI nilitetemeka kidogo, maana kwa wanautambuzi wanaelewa kuwa ni jambo la kawaida sana. Ndipo nikafahamu mwanamuziki ninaye mpenda na kumsikiliza tungo zake hata kama sielewi lugha yake kiasi fulani, lakini miridhimo ya kimuziki inanikolohua nafsi.
Ndipo nikabainia kuwa OLIVER N'GOMA hatunaye duniani. Nikakumbuka nyimbo nyingi sana. Kwa shukrani maridhawa kwa dada Chemi Che Mponda kwa kutuletea habari hii, kwa hakika sina mengi ya kunena, na labda niseme MUNGU AMEMPENDA ZAIDI. LAKINI NAMI NILIMPENDA PIA.
Mara nyingi ukijikuta huna la kuwaza na kuwazua, tembelea blogu za watu utakuta mengi yatakayokupa maarifa na kuchangamsha ubongo.
ReplyDeleteApumzike kwa amani. Tutakukumbuka kwa njia ya sala pia miziki yako. Amina.
ReplyDelete