January 05, 2009

Gumzo letu na dada Yasinta

Jamani natumaini hamjambo woteeeeeee wa kijiwe cha maswali magumu. Nipo kamili tena nazidi kuwakilisha kama kawaida.
Nadhani wengine mlikuwa mnangoja kujua labda tulipiga gumzo gani na dada Yasinta. Bila shaka mambo ya wanablogu yanafurahisha sana na utamu wa mashairi kama kaka Fadhy poa sana.
Katika kupiga gumzo na dada Yasinta, kuna jambo amenifanya nitafakari sana na wakati mwingine huwa najiuliza nianze vipi.

Gumzo la kawaida kuhusu mambo ya teknolojia, blogu na maisha kama ilivyoblogu yake. Jambo lenyewe linahusu VITABU. Nilimkuta kashika kalamu ya wino anaandika, nikauliza kulikoni mwenzetu huchoki? Akatabasamu na kusema 'kutafakari jambo muhimu lazima uandike ukizingatia kuandika ni jambo muhimu pia". Hapo gumzo likazama kuhusu vitabu maana kama ajuavyo napenda kuandika vitabu kuhusu jamii yetu.
Lakini alikuja na swali hili: "Kwanini huandiki vitabu kama unaweza? Si ni jambo la kukaa na kutafakari tu kisha unaandika kwa uamkini?akaongeza, Au hakuna soko la Vitabu? Basi andika vitabu vya wototo, haiwezekani?"
sijui kama mnanielewa ninachotaka kukisema? Ni jambo la kujiuliza sna katika jamii zetu kwani waandishi wa vitabu wanapotea, wengi waliopo wanaandike vile ambavyo vinadumu kwa muda mfupi.
Ni vigumu kupata vitabu kama RAI YA JENERALI, MAKUADI WA SOKO HURIA achilia mbali vile vya Issa Shivji{mwaka jana katoa Pan africanism or Pragmatism?} kizuri. Kwa kweli dada Yasinta kanipandisha moli kama wamasai.
Ndiyo maana nilisema katika maoni yangu fulani kama Simon Kitururu anapaswa kuandika vitabu vya falsafa, Fadhy naye awe Shaban Robert wetu, mzee wa changamoto nye awepo, dada Koero kama vile kitabu cha THINK BIG{umekisoma?}, Bwaya, Kaluse, Kalama tuleteeni UTAMBUZI wenu jamani. Ni hayo tu

7 comments:

 1. kaka hivi hizo rangu unaweza kusoma kwa raha zako? mimi naona kizunguzungu tu hapa, jaribu kuangalia vizuri rangi zinazokubaliana mkuu!

  ReplyDelete
 2. Duuh!! mkuu nashkuru kwa kunishtua, leo nilimpatia jaribio jamaa mmoja hivi anayetaka kublogu kwahiyo nilimweleza aweke mfano wa rangi ili ajifunze mengi lakini ameboronga kidogo kwahiyo alioona ujumbe wako kanishtua. ASANTE naona sasa imetulia sana mzee. S unajua wengine wanataka kublogu kwa kujaribu lakini nilijua akifanya hovo nitakaa mwenyewe, kama hivi. ASANTE KUNISOMA ENDELEA pia

  ReplyDelete
 3. Bomba la changa moto hili!
  Wasomaji wa vitabu bado tupo:-)

  ReplyDelete
 4. Wasomaji wa vitabu tumejaa tele. Ila tatizo wanunuzi hatununui, tunapenda kununua DVD siyo vitabu. Hapana, tatizo ni wachapishaji, wanatuumiza waandishi wachanga. Aah hapana, tatizo ni kodi ya karatasi kubwa wajameni. Wala, tatizo bado ni waandishi sisi. Tujaribu.

  ReplyDelete
 5. Kuandika vitabu sawa, lakini wasomaji wapo?
  T
  atizo ninaloliona ni kwamba watanzania hawapendi kusomavitabu, naomba nikiri hilo, ajitokeze mtu anibishie.
  sisi tumekuwa ni jamii ya kupiga majungu, fitna, uwongo, kusengenyana na kuhujumiana.

  Tumekuwa ni wavivu wa kufikiri, na hatuko tayari kuongeza maarifa, utakuta mtu kama amesomea mambo ya sheria au udaktari basi yeye na taaluma yake hiyo hiyo hahitaji kuongeza chochote wala kusoma maarifa ya wengine ili kupanua wigo wake wa uelewa, hana muda huo, sana sana labda atazungumzia siasa basi kamaliza.

  magazeti yanayopendwa ni ya udaku yale ya hard news hayananafasi na ndio maana yanachechemea, watu hawataki kuyasoma.

  Ndio sababu waandishi wengi mahiri hawaandiki tena.
  Wako wapi kina Kajubi Mukajanga, Elvis Musiba, Penina Mhando, na wengine nimewasahau.

  nashukuru baba yangu alitujengea utamaduni wa kupenda kusoma vitabu mbali mbali bila kuchagua.

  ReplyDelete
 6. Ukitaka kumficha kitu Mbongo, kiweke kwenye maandishi.

  Bado tuna safari ndefu sana kujenga utamaduni wa kweli wa kusoma na kuandika.

  Gumzo tamu sana hili.

  ReplyDelete
 7. Nipo hoi natamani sana kuandika vitabu. kuna riwaya moja nilikataa kuitoa gazetini inaitwa LAZIMA UNIOE ni ya kawaida sana mahaba na mseto wa vituko vya hapa na pale, pia TAIFA MOJA MTAZAMO MMOJA? humo nilitaka kuweka kidogo sehemu za makala zangu na mwendelezo wa kile ninachoamini kinaisumbua TZ na tunatakiwa kuanza lipi kwa vipi na njia ipi, ili kujenga tifa moja.

  ReplyDelete

Maoni yako