Showing posts with label utamaduni. Show all posts
Showing posts with label utamaduni. Show all posts

March 05, 2018

MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU BUSTANI YA MUNGU- HIFADHI YA KITULO.

1.Hifadhi ya Taifa Kitulo ndiyo eneo pekee Tanzania lenye ndege aina ya tandawala machaka (Denhams Bustard) wenye uwezo wa kuruka kutoka bara moja hadi jingine.
2.Hifadhi hiyo inayopita katika mikoa ya Mbeya na Njombe ilitangazwa rasmi kuwa hifadhi ya Taifa mwaka 2005 ikijumuisha sehemu ya eneo la shamba la mifugo, msitu wa Livingstone na bonde la Numbi.
3.Kitulo ina ukubwa wa kilometa za mraba 442. Awali ilijulikana kama Elton Plateau baada ya Mvumbuzi Fredirick Elton kupita eneo hilo mwaka 1870. Mwaka 1960 Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) lilichukua eneo hilo kwa ajili ya ukulima wa ngano na ufugaji wa kondoo.
4. Ndege aina ya tandawili machaka hawapatikani sehemu nyingine yoyote hapa Tanzania zaidi ya Kitulo.
5.hifadhi hiyo ndiyo eneo pekee ambalo ndege hao hutaga mayai na kuzaliana kwa wingi kabla ya kusafiri kwenda mabara mengine.

March 01, 2018

NGOMA ZETU

MIAKA mingi enzi za babu zetu kulikuwa na ngoma maarufu iliyoitwa GEUZA. Hakukuwa na Ligambusa kama ilivyo sasa walisafiri kutoka Lundu kwenda Mbaha au Hinga kucheza Geuza usiku nyakati za Mbalamwezi na wakarudi nyumbani.
 
Kwa upande wa Ngoma ya Mganda, Maboma yaliyoka hadi sasa ni Mawili na yenye upinzani wa Kama vilabu vya soka. LICHUMA LINDU na LIHEGHELYA KONI majina hayo ni kama yanajibizana .Ni ngumu kuona mshiriki wa boma moja kwenda boma lingine nyakati za mazoezi utafukuzwa na kuonekana kama umeenda kuiba stepu(mtindo Wa uchezaji).

Kihoda ndo kimetia fola nyakati za nyuma Lundu ilikuwa na maboma mawili tu yaani Maji na Uamuzi. Lakini kutokana na ongezeko la watu kikafanya kuonekana wanawake wako wengi na wote wanataka kuonyesha uwezo wao wa kusakata ngoma. 

February 23, 2018

KAMBALE SAMAKI WA AJABU KULIKO SAMAKI WOTE DUNIANI

NA JACOB MALIHOJA
 
NIMEFUATILIA kwa kina samaki wa aina tofauti wa ajabu kama vile Electrical El (Mwenye uwezo wa kuzalisha umeme hadi Volts 900 yaani mara nne ya umeme tunaoutumia majumbani), 

Ngisi mwenye uwezo wa kujibadili rangi kama kinyonga kulingana na mazingira anayokuwepo na mwenye nguvu kubwa za kung'ata kuliko nguvu za kung'ta za simba, au Nyangumi kwa ukubwa wake .. binafsi nampa namba moja Kambale baada ya kugundua ni samaki pengine yaweza kuwa kiumbe wa kwanza kuishi mahali kwa miezi au miaka bila kupata chakula.

February 07, 2018

KUNA HAJA YA KUMSHAMBULIA MFALME WA USWAZI (SWAZILAND) KWA MANENO?


NA KIZITO MPANGALA
KUNA haja ya kupima utaratibu wa maisha yake na maneno aliyolishwa Donald Trump? Ikitokea kwamba mfalme wa Uswazi anahitaji mke mmoja atokee Tanzania, mtajitokeza nafisini hapa?

Mfalme wa Uswazi kuwa na wake wengi ina maana muda mwingi anawaza mapenzi tu kama ashambuliwavyo kwa maneno kutokana na hilo? Kuipima Uswazi na nchi za Ulaya na Muungano wa Mikoa ya Amerika kwamba Uswazi haina maendeleo kama ya nchi hizo kwa kuwa mfalme wake ana wake wengi?


Kwenye maendeleo yaliyo bora zaidi kuliko Uswazi yaani Ulaya na Muungano wa Mikoa ya Amerika wao (wanaume) hawana wanawake? Kipimo cha maendeleo ua Uswazi ni kipi? (Wanajua Waswazi wenyewe) Je, kuna yeyote anakereka na desturi za Uswazi?

January 17, 2018

KUPIGA MARUFUKU MAVAZI YA NUSU UCHI

NA PROFESA ANNA TIBAIJUKA (MB)
Profesa Tibaijuka.

 UKIONA watu wanahangaika na suala la mavazi hasa kukazania yale yanayoficha mwili wa mwanamke ujue wana matatizo yao wamelishwa kasumba ya wageni. Dhana ya kuficha mwili ni kweli haina Uafrika wowote ndani yake. Mwafrika katika asili yake haangaiki kuficha mwili wa mwanamke. Hauoni kama chombo cha kumfurahisha mwanaume bali kiungo muhimu kumruhusu mwanamke kutimiza wajibu wake.

Kwa mfano wakati mwanamke wa kizungu anahangaika kujificha kunyonyesha mtoto Mwafrika asili anatoa ziwa mtoto ananyonya hadharani. Hapa titi ni mali ya mtoto siyo ya mume.

Kwa hiyo kabla ya wakoloni kufika na wamisionari walioandamana nao wakiwa wamevaa nguo ndefu watoto walikuwa uchi wasichana walipewa ngozi kujisitiri sehemu za siri wakivunja ungo na wanawake nao yalikuwa hayo hayo. Kulikuwa hakuna ubakaji kwa sababu hiyo. 

Ni kweli utasema jamii ilikuwa haijaendelea na maskini. Unaweza pia kusema hali ya maendeleo ilikuwa duni.Nguo hakuna. Lakini hoja hapa ninayolenga kupangua ni ile kwamba wanawake wakijifunua kwa kuonyesha uso au mikono au matiti au miguu yao au mapaja wanawakwaza wanaume. Sio kweli. Mbona mababu zetu hawakukwazika hizo enzi nilizoelezea? Mbona hawakubaka watoto na wasichana kama ilivyo sasa?

December 28, 2017

UTAFITI: HISTORIA YA ENEO LA TINGITINGI ZIWA NYASA


...TULIPOFIKA hapa tukiwa tunatafakari sehemu ya kupita Mdogo wetu Thobias (mwenye tisheti nyekundu) akaniambia brother nimekumbuka movie moja inaitwa The Hard Way Is The Only Way. Akanielezea kidogo maana jamaa anapenda movie sana. 

Moja ya msitu ulioko eneo la jiwe maarufu Tingitingi. Karibu na ukuta wa mawe wa wampoto.Hapa ilikuwa tunasikiliza sauti za kanga pori tu na kuona kenge na mijusi wa rangi rangi.

October 21, 2017

TABASAMU NA KITABU


Ragin Mmbanga (kushoto) na Markus Mpangala (Kulia)
Huyu ni rafiki yangu. Anaitwa Ragin Mbaga, ila tuwapo farashani hupendelea kumwita "Mzee wa bustani ya usomaji". 

October 13, 2017

WATALII TOKA ULAYA WATEMBELEA HIFADHI YA LUHIRA

SONGEA, RUVUMA
Watalii toka nje ya nchi wameanza kutembelea hifadhi ya Asili ya Luhira iliyopo katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Takwimu za mwaka 2016/ 2017 zinaonesha kuwa hifadhi hiyo imepokea watalii toka nchi za Ujerumani,Afrika ya Kusini,India,Ufaransa,Italia, Uholanzi na wageni toka mikoa mbalimbali nchini ambao pia wanafanya utalii wa kuchunguza aina ya mimea na ndege katika hifadhi hiyo.

Msimamizi wa Hifadhi hiyo Msonda Simwanza anasema wanajiandaa kuweka mazingira ambayo yatawezesha wanyama kama tembo,simba na wanyama wengine adimu kuishi katika hifadhi hiyo bila kuleta athari kwa wanyama na binadamu.

September 29, 2014

UJENZI WA SOKO KUU NYASA

SOKO KUU LA WILAYA YA NYASA KATIKA HATUA ZA MWISHO KUKAMILIKA.

MLO KAMILI NYASA. MASWALI NIYAPATIAYO MAJIBU SASA

Nikiwa mdogo nilikuwa najiuliza sana mafunzo tuliyopewa shuleni kuhusu chakula bora. Nikirejea nyumbani niliona kama hakuna chakula bora na labda tulipaswa kuwa na chakula kingine. Niliona tunanyimwa haki ya chakula bora labda kile kilichoungwa vizuri yaani mboga yenye viungo, mafuta na kadhalika. Lakini jambo moja sikujua ni kwamba kumbe chakula nilichokula kilikuwa bora zaidi.

Vyakula vingi tunavyotumia havina kemikali nyingi bali vyote ni kutoka shambani na kupikwa jikoni. 
Kama samaki basi tunapata moja kwa moja kutoka ziwani na kupelekwa jikoni kwa mapishi. Tofauti na miji mingi ambayo hutegemea samaki kuitoka ziwani lakini hungojea kwa muda mrefu na kumharibu samaki. 
Kwa upande wa Dagaa nayo hali ilikuwa ileile ni ubora wa hali ya juu wa chakula bora.
Vyakula vingi ni vile vinavyotoka shambani moja kwa moja na jambo ambalo linawadia wengi kuwa na afya bora, akili na uwezo wa kufanya kazi nzito.



 NYASA yetu ni NZURI sana

November 04, 2013

TAMASHA LA UTAMADUNI HANDENI NA MIPANGO KABAMBE YA KIMAENDELEO




Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
ILI kujenga jamii bora na yenye kujua tamaduni zao, kunahitajika kuandaliwa matamasha muhimu yenye dhamira ya kweli katika kona mbalimbali za nchi yetu. Huo ni mpango mzuri na wenye tija.


Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani.

Katika suala hilo, wale wadau wanaotarajia au waliowahi kuandaa matamasha ya aina hiyo ni dhahiri wanatakiwa waungwe mkono badala ya kukatishwa tamaa.
Kwa sasa, tamasha ambalo linatajwa katika vinywa vya watu wengi ni lile la Handeni, linalotarajiwa kufanyika Desemba 14, wilayani Handeni mkoani Tanga.

Tamasha hilo la utamaduni na michezo linatambulika kwa jina la ‘Handeni Kwetu,’ jina lililotokana na mtandao ‘blog’ ya Handeni Kwetu.
Mratibu wa Tamasha la Handeni, Kambi Mbwana, pichani.
Vyovyote litakavyotajwa na wadau wa matamasha duniani kote, ili mradi linatimiza na kutoa majibu halisi ya namna ya kutangaza na kukuza utamaduni wa Tanzania, si vibaya na njia ya kulitangaza mbele ya jamii.

Katika mazungumzo yaliyofanyika mapema wiki hii, mwishoni mwa wiki iliyopita, Mratibu Mkuu wa tamasha hilo, Kambi Mbwana, anasema kuwa lengo la kuandaa tamasha hilo ni kushirikiana na serikali na wananchi wote kujua mbinu imara za kuutangaza utamaduni wetu.


Mbunge wa Handeni na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt Abdallah Kigoda, pichani.
Anasema kwa maeneo kama Handeni na kwingineko, kumekuwa na changamoto kubwa za wananchi kuacha utamaduni wao na kufuata wa wenzao jambo linalotakiwa lipingwe vikali.

“Nilikaa chini na kutafakari namna gani ya kuwaunganisha watu wote katika tukio moja na kuwa sehemu ya wao kuangalia ngoma zetu, nyimbo zetu na mbinu za kijamii kwa ujumla wake.

“Naamini katika umri wa taifa letu la Tanzania, kuna mengi yametokea na yaliwahi kutokea hasa wakati wa ukoloni, hivyo naamini siku hiyo tutajua ni kiasi gani watu wa asili ya Handeni walikuwa na mchango kwenye jamii yao,” alisema Mbwana.

Mbwana ambaye ni mwandishi wa habari na mmiliki wa ‘blog’ ya Handeni Kwetu (www.handenikwetu.blogspot), anasema kwamba kwa kukutana watu wote ni sehemu ya kuangalia namna ya kulitumikia taifa letu la Tanzania na kubuni mbinu za kujikomboa kiuchumi.

Mdau huyo wa mambo ya utamaduni, michezo na sanaa kwa ujumla wake ukiwamo muziki, anasema kwamba Handeni ni miongoni mwa wilaya zenye changamoto kubwa hivyo kuna haja ya wadau wote kukutana kwa pamoja na kuangalia namna ya kuzitatua, hasa kwa kupitia tamasha hilo.

“Huu si wakati wa kuangalia Mkuu wa Wilaya (DC) Muhingo Rweyemamu anafanya nini au Mbunge Abdallah Kigoda na viongozi wote wa serikali, ila jambo la muhimu ni kushirikiana nao kuleta maendeleo.
“Mtu wa kwanza katika maendeleo ni mwananchi mwenyewe, hivyo naomba kuwakaribisha Watanzania na hata wale wasiokuwa Watanzania kukutana pamoja na sisi kwenye tamasha hili,” alisisitiza Mbwana.

Aidha, Mbwana anatumia muda huo kuwaomba wadau wote, wakiwamo viongozi wa serikali, mashirika na kampuni kujitokeza kudhamini tamasha hilo litakalokuwa la aina yake. Tamasha la Utamaduni la Handeni Kwetu linafanyika kwa mara ya kwanza, likipangwa kuanza saa tatu asubuhi hadi saa 12 jioni, ambapo vikundi mbalimbali vya sanaa vitashiriki.

Ili kuleta hali ya kimkoa, Mbwana anasema juhudi zinafanyika kupata vikundi katika baadhi ya wilaya za Mkoa wa Tanga ili kuimba nao, kucheza nao na kushiriki nao katika jambo la kimaendeleo. Mdau huyo wa habari anasema kwamba hadi sasa wadau kadhaa wamejitokeza kudhamini tamasha hilo linalotikisa katika maeneo ya Handeni na Tanzania kwa ujumla.

Anawataja wadau hao kuwa ni pamoja na Yusuphed Mhandeni, ambaye ni Mchumi wa CCM Kata ya Makumbusho kwa kupitia Kampuni yake ya Yusuphed Trans, yenye magari yanayotoka Dar es Salaam kwenda Mkata, wilayani Handeni, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, Country Business Directory (CBD) na Michuzi Media Group.

Wengine ni duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind & Arters chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog na Taifa Letu.com.

Mbwana anasema kwamba kwa kupitia tamasha hili, wadau wote watapata fursa ya kutangaza biashara zao, ukizingatia kuwa tamasha hili linatarajia kukutanisha watu wengi zaidi sehemu moja. “Tunaomba udhamini kwa watu wote ili tushirikiane katika kufanikisha tamasha hili la kihistoria, huku tukiamini kuwa wenzetu wa Kilindi, Korogwe tutakuwa nao pamoja.

“Maandalizi yanaendelea kuhakikisha kuwa tunafanya kitu cha tofauti katika tamasha hilo, nikiamini kuwa mguso huu utaendelea kushika kasi na habari hizi njema kuenea nchini kote,” alisema. Mbwana anasema kwamba wazo la kufanyika kwa tamasha hilo limepewa baraka na viongozi wote, akiwamo DC Rweyemamu na Mbunge, Abdalah Kigoda, ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara.

Anasema kuwa kwa kufanyika kwa tamasha hili ni muendelezo wa mipango mingi mizuri ya kimaendeleo itakayoandaliwa kwa kushirikiana na Watanzania wote, hususan wananchi wa Handeni. Mwisho kabisa Mbwana alitumia muda huo kuwakumbusha wafanyabiashara mbalimbali wilayani Handeni na Tanga kwa ujumla, kuingia moja kwa moja katika tamasha hili la aina yake.

October 09, 2013

WATANO WAJITOKEZA KUWEZESHA TAMASHA LA UTAMADUNI HANDENI



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WADAU watano, ikiwamo Kampuni ya usafirishaji ya Phed Trans inayomilikiwa na mdau wa muziki na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Mhandeni, maarufu kama (Yusuphed Mhandeni), wamejitokeza kudhamini Tamasha la Utamaduni linalotarajiwa kufanyika Handeni mjini, mkoani Tanga, Desemba 14 mwaka huu.
Kambi Mbwana, Mratibu wa tamasha la Handeni
Wengine waliokubali kuwezesha tamasha hilo kwa namna moja ama nyingine ni Katomu Solar Specialist, Business Country Director (BCD) duka la mavazi la Chichi Local Ware, SmartMind & Partners ambayo ipo chini ya ANESA COMPANY LIMITED, ambapo katika tamasha hili, watadhamini kwa kupitia kitabu cha ‘NI WAKATI WAKO WA KUNG'AA’, kilichoandikwa na Albert Nyaluke Sanga, bila kusahau kampuni utengenezaji matangazo ya Screen Masters ambapo pia inamiliki mtandao wa Saluti5.com, ikiwa chini ya Mkurugenzi wake Said Mdoe.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kuwa wadau hao ndio wa kwanza kujitokeza kuwezesha kwa tukio hilo, huku mazungumzo yakiendelea kwa wengine wenye nia ya kudhamini tamasha hilo.

Alisema ishara njema imeanza kujitokeza kuwa wadau na makampuni mengi zaidi yanaweza kuingia kwa ajili ya kuhakikisha kuwa tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza na kuweka historia katika harakati za kukuza utamaduni kama ishara ya kuleta maendeleo.

“Tunashukuru kwa kampuni hizi kuwa za kwanza kuthibitisha kushiriki na sisi kwa namna moja ama nyingine juu ya kufanyika kwa tamasha hili, hivyo naamini kwa pamoja tutafanikisha na kuwezesha kufanya kile tunachokusudia.

“Bado juhudi zinafanyika kuingia kwa wadhamini wengi zaidi ikiwa ni njia ya ushirikiano kati yetu sambamba na wadau hao kuwa na nafasi kubwa ya kutangaza biashara zao kwa Watanzania wote, hususan wakazi na wananchi wa Handeni kwa ujumla wake,” alisema Mbwana.

Aidha, Mbwana alitumia fursa hiyo kuwashukuru walioanza kujitokeza kudhamini tamasha hilo na kuzitakaka kampuni, taasisi, mashirika mbalimbali pamoja na watu binafsi wenye nia ya kukuza na kuthamini utamaduni wajitokeze ili kuhakikisha kuwa Tamasha hilo linafanyika kwa mguso na kufikisha kile kilichokusudiwa kwa hadhira.

Tamasha hilo limeanza kugusa hisia za watu wengi kutokana na kuwa na mipango thabiti ya kulifanya kwa mafanikio, ikiwa ni njia pia ya kuwakutanisha wananchi kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kufikiria mambo ya kimaendeleo, huku likiandaliwa na Raha Company and Entertainment.

May 31, 2013

MAJIMBO YA UMOJA WA MAJIMBO YA MAREKANI-BARUA


Na Pete Mhunzi, Marekani

Salaam zenu. Mimi kwa jina ninaitwa Pete M. Mhunzi, Mmarekani, Mswahili wa buku. Nilisoma makala yako kuhusu wanasiasa wakiwa pamoja na wajasiriasiasa. Kweli umenena lenye busara kubainisha hulka za viongozi wengi dunia nzima. Nakushukuru.

Madhumuni ya barua hii zaidi ya kupongeza ni kusema machache juu ya neno "jimbo" haswa linalotafsiriwa kwa Kiingereza.  Ulimtaja Rais wetu Barrack Obama katika makala yako kuhusu CUF na kushindwa kwake huko mkoani Tabora. Ulitaja mji wa Honolulu lakini haupo katika Chicago kwa sababu Chicago pia ni mji.  

Honolulu ni mji uliopo kwenye kimojawapo cha visiwa vya Hawaii.  Visiwa hivyo vyote vinatambulika "jimbo".   Chicago ni mji uliopo bara katika jimbo la Illinois.  

Kuna majimbo hamsini katika taifa la Marekani kila moja likiwa na gavana.  Chini ya rais ambaye ana wadhifa ya taifa zima gavana anaongoza serikali ya jimbo ambamo alichaguliwa katika upigaji kura.

Nimeongea kwa upana na urefu juu ya neno hilo "jimbo" pamoja na diwani wa kata ya kati, huko Arusha naye ni mjomba wa mke wangu, kwa jina anaitwa Abdulrasul Tojo.  Tukagundua maana ya "jimbo" katika mfumo  wa siasa za Tanzania ni tofauti sana na maana ya "state" katika mfumo wa siasa za Marekani, yaani taifa la Marekani kwa vile kuna mabara mawili yanayoitwa Marekani.

Tukipima maana kwa ukubwa wa eneo la ardhi la taifa, jimbo hufuata taifa zima halafu ndani ya jimbo kuna "county"  ama  "province" (jimbo la Louisiana peke yake).

Halafu miji ambayo huongozwa na meya anayechaguliwa katika upigaji kura. Bado sielewi vizuri maana ya "jimbo" katika mfumo wa siasa Tanzania!   Nitatia nanga barua hii kwa kushukuru tena mawazo yako ambayo yamenichemshia bongo isitoshe kuridhisha kiu changu cha Kiswahili fasaha.  Asante, asante sana.

Wakatabahu, 
Pete M. Mhunzi
Retired Professor of History
petemhunzi@gmail.com