December 28, 2017

UTAFITI: HISTORIA YA ENEO LA TINGITINGI ZIWA NYASA


...TULIPOFIKA hapa tukiwa tunatafakari sehemu ya kupita Mdogo wetu Thobias (mwenye tisheti nyekundu) akaniambia brother nimekumbuka movie moja inaitwa The Hard Way Is The Only Way. Akanielezea kidogo maana jamaa anapenda movie sana. 

Moja ya msitu ulioko eneo la jiwe maarufu Tingitingi. Karibu na ukuta wa mawe wa wampoto.Hapa ilikuwa tunasikiliza sauti za kanga pori tu na kuona kenge na mijusi wa rangi rangi.


Nchi hii ina historia toka maeneo ambayo unakutana na wasimulizi waliohifadhi kumbukumbu za miaka mingi. Wasimulizi hawa hawajawahi hata kukutana na mtaalamu yeyote wa masuala ya wahifadhi kumbukumbu katika Taasisi yoyote kama ilivyo wale wanahistoria au watu wa Maliasili. Shughuli za binadamu zinazofanyika maeneo haya zitasababisha wanyama kama ngedere kutoweka.

Ukitaka kujua habari za “Dragon” aliyeko maeneo ya Jiwe la Stima au Tingitingi ni miongoni mwa historia iliyopo hadi sasa. Mabaki na mapango yaliyotumiwa na mababu kujisitiri wakati vita.

Picha ya chini nikiwa na Kizito, Thobias katika Forodha ya Lundu hapa Nyasa.

Honorius Mpangala
Desemba 28/2017
Lundu, Nyasa

No comments:

Post a Comment

Maoni yako