COMMUNITY DEVELOPMENT
OFFICER GRADE II) – NAFASI 22
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Waajiri wafuatao:- Halmashauri
ya Manispaa ya Morogoro, Mtwara, Sumbawanga, Simanjiro, Halmashauri ya Mji
Njombe, Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba, Newala, Nkasi, Bukoba, Sengerema,
Rufiji, na Mpanda na Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
71.1 MAJUKUMU YA KAZI
Maafisa Maendeleo ya Jamii Dalaja la II watapangiwa kazi
katika ngazi za Kata au Makao Makuu ya Halmashauri na kazi zao zitakuwa
zifuatazo:
· Kuandaa na kupendekeza mipango na mikakakti ya kubadili
fikra za watu ili waweze kuwa na mawazo ya maendeleo sawia na Sera za Serikali
na wakati uliopo
· Kupitia mbinu shirikishi kuwezesha jamii kuanzisha miradi
ya kijamii kama vile:-
- Usafi wa mazingira
- Ujenzi wa nyumba bora
- Ujenzi wa shule
- Ujenzi wa zahanati
- Kuchimba au kuzifanyia matengenezo barabara hasa za
vijijini
- Ujenzi wa majosho
- Uchimbaji wa visima vifupi
44
- Utengenezaji wa malambo
· Kuhamasisha matumizi endelevu ya mazingira
· Kusambaza na kuhamsisha matumizi ya teknolojia sahihi kama
vile uvunaji wa maji ya mvua, majiko sanifu, matumizi ya mikokoteni
· Kuhamasisha watu kutumia huduma za mafunzo ya Vyuo vya
Maendeleo ya Wananchi
· Kuwasadia wanachi vivijini kuandaa maandiko (Project Write
ups) ya kuombea fedha za kuendesha miradi yao
· Kuhamasisha, kuandaa na kutoa elimu kwa umma kuhusu uraia
na Utawala bora
· Kukusanya, kutunza, kutafsiri na kusambaza takwimu na
kumbukumbu muhimu kwa ajili ya matumizi ya jamii
· Kuwezesha wananchi kupambana na mila zenye madhara kwa
afya za wanchi hasa wanawake na watoto wa kike, kuenea kwa virus vya UKIMWI na
magonjwa ya mlipuko.
· Kuelimisha viongozi wa Serikali za Vijiji, Dini na
Mashirika yasiyo ya Kiserikali kuhusu Sera mbalimbali za Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto na kutumia Sera hizo
· Kutoa taarifa za hali ya jamii kwa ngazi mbalimbali
71.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa Shahada au Stashahada ya Juu ya
Maendeleo ya Jamii kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali katika fani
zifuatazo:-
Maendeleo ya
Jamii (Community Development)♣
Elimu ya Jamii
(Sociology)♣
Masomo ya
Maendeleo (Development Studies)♣
Mipango na
Usimamizi wa Miradi (Project Planning and Management)♣
Maendeleo na
Jinsia (Gender and Development)♣
71.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D
kwa mwezi.
72.0 MLEZI WA WATOTO MSAIDIZI (CHILD CARE ASSISTANT) –
NAFASI 5
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Manispaa ya Singida na
Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga.
72.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kulea watoto katika vituo vya kulelea Watoto wadogo mchana
· Kutoa mafunzo kwa akina mama juu ya malezi bora ya watoto
wadogo wenye umri kati ya miaka 0 hadi 8
· Kusaidia shughuli za kinga za magonjwa ya watoto
vijijini/sehemu au eneo la kituo
· Kuwa kiongozi wa kituo cha malezi ya awali ya Watoto
wadogo
45
72.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu mafunzo ya
mwaka mmoja ya malezi ya awali ya watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 0 hadi
8 kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali au wenye cheti cha mwaka mmoja cha
mafunzo ya Ustawi wa Jamii.
72.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B
kwa mwezi.
62.0 MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI II (COMMUNITY DEVELOPMENT
ASSISTANT GRADE II) – NAFASI 52
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Manispaa ya Mtwara na
Kigoma/Ujiji. Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Babati, Pangani, Mkinga,
Sengerema, Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Halmashauri ya Mji Njombe,
Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Kibondo na Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
62.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuwa kiungo kati ya wanakijiji, Afisa Mtendaji wa kata na
watumishi wengine wa Serikali katika kutekeleza shughuli za maendeleo
· Kuhamasisha wanakijiji katika kazi za kujitegemea
· Kubainisha na kuratibu matumizi ya rasilimali kwa miradi
ya kijiji
· Kukusanya, kutunza, kutafsiri na kusaidia wanakijiji
kutumia takwimu na kumbukumbu mbalimbali kwa shughuli za maendeleo ya kijiji
· Kutoa taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo kila
mwezi kwa uongozi wa kijiji na kwa Afisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Kata
· Kuwahamisha na kuwawezesha wananchi kulinda na kuhifadhi vyanzo
vya maji
37
· Kusaidia kuunda vikundi vya kijamii na kimaendeleo
· Kuratibu shughli za Asasi zisizo za kiserikali na kijamii
· Kuandaa tararifa za utekelezaji kazi vijinjini za kila
mwezi, robo, nusu na mwaka mzima
· Kuratibu shughuli za kupambana na UKIMWI
62.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV/VI wenye Stashahada ya
Maendeleo ya Jamii kutoka katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii (Buhare au
Rungemba) au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
62.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara
TGS.C kwa mwezi
63.0 AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA II (WARD EXECUTIVE
OFFICER GRADE II) – NAFASI 106
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Manispaa ya
Dodoma, Morogoro, Mtwara, Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Bunda, Mafia,
Biharamulo, Newala, Kondoa, Masasi, Mtwara na Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
63.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa
Idara zote katika kata na atashughulikia masuala yote ya kata
· Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati
mbalimbal.i ya uzalishaji, mali, kuondoa njaa na Umasikini.
· Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.
· Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo
ya kata, vijiji na Mtaa.
· Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria
ndogondogo katika Kata yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibu na kusimamia
shughuli za Uchaguzi katika Kata.
· Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia
maendeleo ya eneo lake.
· Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine
katikangazi ya Kata.
· Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na
kuziwasilisha kwa mkurugenzi na nakala kwa Katibu Tarafa.
· Atakuwa mwenyekiti katika vikao vinavyowahusisha wataalamu
na watendaji wa vjiji, na NGO’S katika kata yake.
· Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote
zinazokusanywa katika vijiji, vitongoji, na kata yake.
38
63.2 SIFA ZA MWOMBAJI.
· Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa yenye mwelekeo wa Sayansi
ya Jamii (Social Sciences) Utawala, (Public Administration and Local
Gorvernment), Sheria au Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.
63.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara
TGS D. kwa mwezi.
64.0 AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA III (WARD EXECUTIVE
OFFICER GRADE III) – NAFASI 91
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Manispaa ya
Singida, Kigoma/Ujiji na Songea, Halmshauri ya Wilaya ya Chato, Songea,
Handeni, Kibondo, Mkinga, Tunduru, Mbeya, Mkuranga, Kibaha, Kwimba, Njombe, Rufiji,
Bukoba, Mwanga, Sengerema na Mpanda
64.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa
Idara zote katika kata na atashughulikia masuala yote ya kata
· Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati
mbalimbali ya uzalishaji, mali, kuondoa njaa na Umasikini.
· Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.
· Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo
ya kata, vijiji na vitongoji.
· Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria
ndogondogo katika Kata yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibuna kusimamia shughuli
za Uchaguzi katika Kata.
· Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia
maendeleo ya eneo lake.
· Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine
katika ngazi ya Kata.
· Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na
kuziwasilisha kwa mkurugenzi na nakala kwa Katibu Tarafa.
· Atakuwa mwenyekiti katika vikao vya vinavyowahusisha
wataalamu na watendaji wa vjiji, na NGO’S katika kata yake.
· Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote
zinazokusanywa katika vijiji, vitongoji, na kata yake.
64.2 SIFA ZA MWOMBAJI.
· Kuajiriwa waliohitimu kidato cha nne au sita na kuhudhuria
mafunzo ya Stashahada yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social Sciences)
Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment), Stashahada ya Sheria au
Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na
Serikali.
64.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS C
kwa mwezi. 39
65.0 AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA II (VILLAGE
EXECUTIVE OFFICER GRADE II) – NAFASI 57
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Waajiri wafuatao:- Halmashauri
ya Wilaya ya Bunda, Kondoa, Tandahimba,Wilaya ya Mbeya, Babati, Mkuranga,
Simanjiro, Newala na Ruangwa
65.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atakuwa Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Kijiji na
Kamati zake katika Mipango ya Maendeleo ya kijamii na Utekelezaji wa Mipango ya
Maendeleo.
· Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Kijiji na atasimamia
mapato na matumizi ya Serikali ya kijiji
· Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora
katika Kijiji.
· Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango
ya Maendeleo ya kijiji
· Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Kijiji.
· Atatafsiri Sera, ataratibu na kusimamia utekelezaji wa
Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Kijiji.
· Ataratibu na kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika
eneo lake na kuziwasilisha kwenye Halimashauri ya Kijiji na baadae kwenye kata
.
· Ataongoza vikao vya maendeleo ya Kijiji vitavyowahusisha
wananchi na wataalamu waliopo kwenye eneo lake.
· Atahamasisha wananchi katika kampeni za kuondoa njaa,
umasikini, na kuongeza uzalishaji mali.
· Atasimamia matumizi bora ya Nguvu kazi.
· Atakuwa Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu Katika
Kijiji.
· Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi,
wataalamu mbalimbali na NGO waliopo katika kijiji.
65.2 SIFA ZA MWOMBAJI.
· Kuajiriwa wenye elimu ya kidato cha IV na VI waliohitimu
Stashahada ya kawaida katika fani yoyote yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii
(Social Sciences) Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment),
Stashahada ya Sheria au Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.
65.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS C
kwa mwezi.
66.0 AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (VILLAGE
EXECUTIVE OFFICER GRADE III) – NAFASI 207
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Waajiri wafuatao:- Halmashauri
ya Manispaa ya Singida, Halmashauri ya Mji Njombe, Halmashauri ya Wilaya ya
Chato, Handeni, Mkinga, Sengerema, Tunduru, Babati, Masasi, Mtwara, Mwanga,
Kwimba, Rufiji, Ngara, Tarime na Mpanda 40
66.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atakuwa Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Kijiji na
Kamati zake katika Mipango ya Maendeleo ya kijamii na Utekelezaji wa Mipango ya
Maendeleo.
· Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Kijiji na atasimamia
mapato na matumizi ya Serikali ya kijiji
· Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora
katika Kijiji.
· Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango
ya Maendeleo ya kijiji
· Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Kijiji.
· Atatafsiri Sera, ataratibu na kusimamia utekelezaji wa
Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Kijiji.
· Ataratibu na kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika
eneo lake na kuziwasilisha kwenye Halimashauri ya Kijiji na baadae kwenye kata.
· Ataongoza vikao vya maendeleo ya Kijiji vitavyowahusisha
wananchi na wataalamu waliopo kwenye eneo lake.
· Atahamasisha wananchi katika kampeni za kuondoa njaa,
umasikini, na kuongeza uzalishaji mali.
· Atasimamia matumizi bora ya Nguvu kazi.
· Atakuwa Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu Katika
Kijiji.
· Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi,
wataalamu mbalimbali na NGO waliopo katika kijiji.
66.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Elimu ya Kidato cha Nne au cha sita
waliohitimu Astashahada (Certificate) katika Fani yoyote yenye mwelekeo wa
Sayansi ya Jamii (Social Sciences) Utawala, (Public Administration and Local
Gorvernment), Astashahada ya Sheria au Sifa nyingine inayolingana na hizo
kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
66.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara
TGS B kwa mwezi.
67.0 AFISA MTENDAJI MTAA II (MTAA EXECUTIVE OFFICER GRADE
II) – NAFASI 36
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Manispaa ya
Temeke, Halmashauri ya Manispaa ya Songea na Sumbawanga
67.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kutoa ushauri katika utekelezaji wa sheria za Serikali za
Mitaa.
· Kutoa ushauri juu ya uanzishaji na uendeshaji wa mamlaka
mpya za Serikali za Mitaa.
· Kutoa ushauri juu ya makadirio ya mapato na matumizi ya
Serikali za Mitaa.
· Kusimamia na kushauri juu ya matumizi bora ya fedha za
Serikali.
· Kutayarisha taarifa za robo mwaka na mwaka zinazohusu
mwenendo wa Serikali za Mitaa.
41
· Kufanya kazi nyingine zitakazoagizwa na Watendaji,
Wasimamizi wa masuala ya Serikali za Mitaa.
67.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa waliohitimu kidato cha nne au sita na kuhudhuria
mafunzo ya Stashahada ya yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social Sciences)
Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment), Stashahada ya Sheria au
Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na
Serikali.
67.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS.C
kwa mwezi.
68.0 AFISA MTENDAJI MTAA DARAJA LA III (MTAA EXECUTIVE
OFFICER GRADE III) – NAFASI 46
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Manispaa ya
Dodoma, Morogoro, Mtwara, Kigoma/Ujiji na Singida na Halmashauri ya Wilaya ya
Rufiji.
68.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atakuwa Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Mtaa na
Kamati zake katika Mipango ya Maendeleo ya kijamii na Utekelezaji wa Mipango ya
Maendeleo.
· Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Mtaa na atasimamia
mapato na matumizi ya Serikali ya Mtaa
· Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora
katika Mtaa
· Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango
ya Maendeleo ya Mtaa
· Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Mtaa.
· Atatafsiri Sera, ataratibu na kusimamia utekelezaji wa
Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Mtaa
· Ataratibu na kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika
eneo lake na kuziwasilisha kwenye Halimashauri ya Mtaa na baadae kwenye Kata.
· Ataongoza vikao vya maendeleo ya Mtaa vitavyowahusisha
wananchi na wataalamu waliopo kwenye eneo lake.
· Atahamasisha wananchi katika kampeni za kuondoa njaa,
umasikini, na kuongeza uzalishaji mali.
· Atasimamia matumizi bora ya Nguvu kazi.
· Atakuwa Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu Katika
Mtaa.
· Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi,
wataalamu mbalimbali na NGO waliopo katika Mtaa.
68.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Elimu ya Kidato cha Nne au cha sita
waliohitimu Astashahada (Diploma) katika Fani yoyote yenye mwelekeo wa Sayansi
ya Jamii (Social Sciences) Utawala, (Public Administration and Local
Gorvernment), Atashahada ya Sheria au
42
Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.
68.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS B
kwa mwezi.
69.0 AFISA USTAWI WA JAMII DARAJA LA II (SOCIAL WELFARE
OFFICER GRADE II) – NAFASI 25
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Waajiri wafuatao: – Katibu Mkuu
Ofisi ya Makamu wa Rais, Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Halmashauri ya Manispaa
ya Morogoro, Singida, Sumbawanga, Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Handeni,
Mkinga, Newala, Tandahimba, Bahi na Chamwino na Halmashauri ya Jiji la Mwanza
69.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuendesha Usaili wa wahudumia (watu wenye ulemavu, wazee,
familia zenye matatizo, watoto na vijana wenye matatizo mbalimbali).
· Kufanya ukaguzi wa mazingira wanayoishi wahudumiwa ili
kupata taarifa zao kamili
· Kuandaa taarifa za usaili na ukaguzi wa mazingira ya
wahudumiwa.
· Kupokea na kukusanya taarifa za Ustawi wa Jamii kutoka kwa
wadau na vituo mbalimbali vya Ustawi wa Jamii.
· Kupokea na kukusanya takwimu zinazohusu huduma za watu
wenye ulemavu, wazee, malezi ya watoto na familia zenye matatizo.
· Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya
uandikishaji vituo vya kulelea watoto wadogo mchana, malezi ya kambo (foster
care) na vituo vya walezi wa watoto wadogo mchana.
· Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya msaada
wa Rais kutoka kwa akina mama, walojifungua watoto watatu au zaidi kwa mara
moja.
· Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya watoto
yatima au wanaohitaji misaada mbalimbali
· Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali
toka kwenye familia za watu wenye dhiki
· Kuhoji na kuandaa taarifa za washitakiwa.
· Kusimamia wahudumiwa katika makazi, vyuo vya mafunzo ya
Ufundi Stadi vya watu wenye ulemavu, Mahabusu za watoto na shule za maadilisho.
· Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi
zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
69.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Shahada ya BA (Social Works or Sociology)
au Stashahada ya juu ya Ustawi wa Jamii (Advanced Diploma in Social Works)
kutoka Chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa na Serikali
43
69.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D
kwa mwezi.
70.0 MSAIDIZI USTAWI WA JAMII DARAJA LA II (SOCIAL WELFARE
ASSISTANT GRADE II) – NAFASI 6
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga,
Ruangwa
70.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kutambua na kuhudumia watu walio katika makundi maalum na
mazingira hatarishi.
· Kukusnya takwimu zinazohusu watu walio katika makundi
maalum na mazingira hatarishi.
· Kuchambua na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali kutoka
kwenye familia na watu wenye dhiki.
· Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi
zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
70.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye cheti cha
mafunzo ya mwaka mmoja ya Ustawi wa Jamii kutoka Chuo kinachotambuliwa na
Serikali
70.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa
mwezi.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na
wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe
barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe
ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha
habari cha barua na juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya
kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza
(Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya
wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo,
nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia
kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za
kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa
kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from
respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina
kwa nyuma.
vii. “Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”,
“Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND
FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma
hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za
kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia
maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba
2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa
hatua za kisheria.
xii. WAAJIRI WOTE WALIOPO NJE YA DAR ES SALAAM WANAOMBWA
KUSAMBAZA MATANGAZO HAYA KWENYE MBAO ZA MATANGAZO NA MAENEO MENGINE.
xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 8 Juni,
2013
xiv. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za
Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au
Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Secretary,
Public Service Recruitment
Secretariat,
P.O.Box 63100
Dar es Salaam.
AU
Katibu,
Sekretariati ya Ajira katika
Utumishi wa Umma,
SLP.63100,
No comments:
Post a Comment
Maoni yako